09/03/2026
🚨Miongoni mwa binadamu anayeaminika na WANAUME Duniani ndiye ametumika katika utambulisho wa jezi mpya za kimataifa za Young Africans msimu 2026/27.
Fabrizio Romano ni miongoni mwa binadamu anayeaminika na kufuatiliwa na wengi ulimwenguni kutokana na kutoa habari za uhakika za Usajili wa nyota mbalimbali duniani yaani ni SURE ODDS!
Idara ya habari ya Yanga tafadhali itengwe kwa muda kutokana na ubunifu ambao wamekuwa wakiufanya eneo lao hawa ni IDARA YA HEKAHEKA yaani shughuli juu ya shughuli k**a watu wa Uswahilini.
Hili la leo ni kubwa na kauli mbiu yao walisema DUNIA ITAJUA na hakika imejua kwa sababu Fabrizio anafuatiliwa na watu wengi duniani.