10/09/2026
Je, mitandao ya kijamii inawasaidia wasichana kukua au inawarudisha nyuma?
Wiki hii ndani ya msichana shupavu, tutazungumzia jinsi wasichana wanavyoweza kutumia mitandao ya kijamii kujifunza, kujiendeleza, kujenga kujiamini, kutangaza vipaji na ujuzi wao, na kupata fursa mbalimbali zinazoweza kuwasaidia.
Pia, tutajadili changamoto zinazoweza kutokea, k**a vile unyanyasaji mtandaoni (cyberbullying), shinikizo kutoka kwa marafiki, na maudhui yanayoweza kuathiri kujiamini kwa wasichana.
Tutaungana na wataalamu:
- Monica Peter, dada rafiki (mentor) kutoka GLAMI Tanzania , akiongelea jinsi programu za Binti Shupavu na Kisa zinavyowasaidia wasichana kupata maarifa na ujuzi wa kutumia mitandao ya kijamii kwa usalama na kwa manufaa yao.
- Teresa Mbulumi, maarufu k**a Teresa Mbulumi , mwandishi wa habari na mtengenezaji wa maudhui ya kidijitali, akiongelea fursa nyingi alizopata kupitia mitandao ya kijamii, pamoja na changamoto anazoziona kwa wasichana wanapoitumia vibaya.
Tuambie……, unaweza kukaa muda gani bila kuperuzi mtandaoni?