05/12/2024
Al-Swiddiq Education Center
Nursery, Primary & Madrasa
05/12/2024
Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Dan Mastwe, Juma Rajabu
Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Swadaqaty Shenkome, Haidary Shamte
28/04/2023
Mzigo upo sokoni Kwa mahitaji ya Gazi hizo piga 0623963964
Zanzibar
Assalamu Alaikum. Al-Swiddiq Education Center ni shule ya kusaidia jamii hususani jamii ya inayo ishi katika mazingira magumu na mayatima. Inajitolea kufundisha watoto na kuwapatia huduma ya chakula ili waweze kujifunza. Watoto wanao faidika na huduma zetu ni kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea na wanapata elimu ya baby class, nursery, primary na Madrasa(Islamic Class) Pia taasisi haija wasahau vijana ambao wamehitimu elimu za ngazi mbalimbali au kutoroka shuleni kwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali ambayo inawafanya waweze kujiajiri na kujitegemea vilevile inafundisha mafunzo ya Computer na Lugha za kigeni kwa watoto, vijana na hata wafanya kazi ili kuwajengea uwezo.
Taasisi hii imeanzisha na kikundi cha vijana ambao wamehitimu elimu katika vyuo mbali mbali na fani mbali ambao wanafanya kazi kwa kujitolea. Lakini taasisi inakabiliwa na changamoto nyingi sana za uendeshaji hasa hasa suala la jengo kwani kwa sasa inatumia majengo ya kukodi na hayana hadhi ya kutolea huduma hizo, Taasisi inasumbuliwa na suala la usafiri(School Bus) kwani inatumia gharama kukodi magari kwa ajili ya usafiri wa watoto kwani watoto wengine Wana mbali na wanahitaji kusaidiwa, Tasisi hii inakabiliwa na ukosefu wa vifaa k**a vile computer, vikalio, vitabu, mapembea, photocopy mashine na baadhi ya vifaa vya ofisini na kujifunza.
Hivyo tunakuomba uweze kutusaidia katika kutatua changamoto zinazo tukabili na hata kutusaidia kutafuta Wafadhili wa kutusaidia iwe mtu binafsi, ENGs, Tasisi za kimataifa, Shirika, Serikali na hata Tasisi za Dini.
Kwa maelezo zaid wasiliana nasi kwa:-
+255772143880
[email protected]
[email protected]
Tupo Kisauni Zanzibar
Tanzania East Africa
All you are welcome at our center
16/12/2018
بسم الله الرحمن الرحيم
Assalamu Alaikum.
Uongozi wa Al-Swiddiq Education Center unapenda kuwajuilisha Wazazi na Walezi wote kuwa uandikishaji wa Wanafunzi Wapya unaendelea. Shule inapokea wanafunzi wa Baby Class, Nursery, Primary na Madrasa. Tunapokea wanafunzi kuanzia wa Baby Class mpaka darada la nne(S.T.D IV). Shule inazingatia mila, desturi, silka na mwenendo wa dini ya kiislamu. Shule ina walimu wenye sifa na weledi katika kazi, Usafiri wa Uhakika, na Chakula kizuri kwa wanafunzi. Shule ipo kisauni mitondooni karibu na sheli mpya ya United Petroleum mkabala na kiwanda cha matufali. Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba zifuatazo:-
0772143880, 0778209002, 0718007756, 0623963964.
E-Mail: [email protected] or [email protected] au tembelea www.alswidduq.com
Wahi mapema kuja kumuandikisha mtoto kwa elimu bora ya dini na dunia sambamba na malezi bora.
"Excellence Is Our Priority(Ubora Ni Kipaumbele Chetu".
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the school
Telephone
Website
Address
Kisauni/Unguja Zanzibar
Zanzibar