06/07/2021
Assalamu Alaikum. Al-Swiddiq Education Center ni shule ya kusaidia jamii hususani jamii ya inayo ishi katika mazingira magumu na mayatima. Inajitolea kufundisha watoto na kuwapatia huduma ya chakula ili waweze kujifunza. Watoto wanao faidika na huduma zetu ni kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea na wanapata elimu ya baby class, nursery, primary na Madrasa(Islamic Class) Pia taasisi haija wasahau vijana ambao wamehitimu elimu za ngazi mbalimbali au kutoroka shuleni kwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali ambayo inawafanya waweze kujiajiri na kujitegemea vilevile inafundisha mafunzo ya Computer na Lugha za kigeni kwa watoto, vijana na hata wafanya kazi ili kuwajengea uwezo.
Taasisi hii imeanzisha na kikundi cha vijana ambao wamehitimu elimu katika vyuo mbali mbali na fani mbali ambao wanafanya kazi kwa kujitolea. Lakini taasisi inakabiliwa na changamoto nyingi sana za uendeshaji hasa hasa suala la jengo kwani kwa sasa inatumia majengo ya kukodi na hayana hadhi ya kutolea huduma hizo, Taasisi inasumbuliwa na suala la usafiri(School Bus) kwani inatumia gharama kukodi magari kwa ajili ya usafiri wa watoto kwani watoto wengine Wana mbali na wanahitaji kusaidiwa, Tasisi hii inakabiliwa na ukosefu wa vifaa k**a vile computer, vikalio, vitabu, mapembea, photocopy mashine na baadhi ya vifaa vya ofisini na kujifunza.
Hivyo tunakuomba uweze kutusaidia katika kutatua changamoto zinazo tukabili na hata kutusaidia kutafuta Wafadhili wa kutusaidia iwe mtu binafsi, ENGs, Tasisi za kimataifa, Shirika, Serikali na hata Tasisi za Dini.
Kwa maelezo zaid wasiliana nasi kwa:-
+255772143880
[email protected]
[email protected]
Tupo Kisauni Zanzibar
Tanzania East Africa