14/04/2025
Mkaguzi Mkuu wa Elimu Zanzibar Bi. Maimuna Fadhil Abas amewataka Walimu Wakuu kuandaa mikakati ya kuwawezesha Walimu kuanzisha mpango wa utakaowawezesha Wanafunzi kusoma vizuri, kuandika na kuhesabu.
Wito hua ameutoa kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na Walimu Wakuu katika Mafunzo ya SBI yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kituo Cha Walimu Michakaini na Wingwi Kisiwani Pemba.
Amesema Mafunzo ya SBI yatawawasaidia Walimu kusaidiana wenyewe na kuepusha dharau baina yao.
Aidha amesema Mafunzo hayo ya SBI yatasaidia kuwaandaa Wanafunzi wa Msingi kuingia Sekondari wakiwa na uwezo na kupunguza mzigo kwa Walimu wa Sekondari.
Akielezea zaidi kuhusu umuhimu wa mafunzo hayo Bi. Maimuna amesema yatawapa Walimu fursa ya kuangalia changamoto zao zinazowakabili nakuzitafutia suluhisho.
Nae Mkuu wa Kitengo Cha Mafunzo kazini. Ndg. Rashid Masheko Ali amesema lengo la Mafunzo hayo ni kuwasaidia Walimu waweze kujiendeleza wenyewe wanapokua maeneo yao ya kazi.
Amesema ili kuwapa hamasa walimu, Kitengo kitatoa zawadi kwa Walimu ambao watayafanyia kazi kwa vitendo mafunzo hayo.
Kwa upande wake Mratibu Idara ya Mafunzo ya Ualimu Mwalimu. Khamis Yahya amesema Mafunzo ya SBI yatawasaidia Walimu kuweza kushirikiana na kufanya mambo yao kwa pamoja.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano (OCIE )