Chuo ifm

Chuo ifm Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Chuo ifm, Education, Zanzibar.

20/08/2026

KARIBU KATIKA BANDA LA IFM TANGA, TUPO KUWAHUDUMIA

10/08/2026
03/08/2026

PROF JEREMIA MAKINDARA ATEMBELEA BANDA LA IFM; AWAKARIBISHA WANANCHI KUJIPATIA MAARIFA NANENANE 2026

Makamu Mkuu wa Chuo – Mipango, Fedha na Utawala, wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Jeremia Makindara, ametembelea banda la chuo katika Maonesho ya Nanenane 2026 yanayoendelea Viwanja vya Nzuguni, Dodoma.

Akiwa katika banda la IFM, alizungumza na wananchi waliokuwa wakitembelea maonesho hayo na kuwahimiza kutumia fursa hiyo kutembelea banda la IFM ili kujifunza na kupata taarifa kuhusu huduma, ubunifu na mchango wa chuo katika maendeleo ya jamii.

IFM inaendelea kuwakaribisha watu wote kutembelea banda letu.
Karibu Nzuguni, Dodoma!

18/07/2026

SAUTI YA MDAU: KWA NINI UCHAGUE IFM?

Ubora wa taasisi huonekana kupitia mchango wake kwa jamii na maoni ya wadau wanaoifahamu.

Bi. Haitham N. Suleiman, mdau wa elimu, anazungumzia nafasi ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) katika kuandaa wataalamu wenye ubora, mchango wa wahitimu wake katika taasisi mbalimbali, pamoja na historia ya chuo katika kutoa elimu, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu.

Zaidi ya hayo, pia anawahamasisha wanafunzi, wazazi na wadau wa elimu kuchagua IFM, mahali sahihi pa kujenga msingi imara wa taaluma na kuchangia maendeleo ya Taifa.

Ni kwa nini mdau huyu anaamini IFM imeendelea kujenga heshima katika sekta ya elimu ya fedha? Tazama video hii...

πŸŽ“ Karibu IFM. Jenga kesho yako kwa elimu yenye ubora.

18/07/2026

KARIBU IFM ZANZIBAR – UJIONEE FURSA NA HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA CHUO

Je, ungependa kufahamu kwa nini IFM inaendelea kuwa chaguo la wengi katika elimu ya juu?

Mkurugenzi wa Kampasi ya IFM Zanzibar, Dkt Talib S Zahor, anakukaribisha kutembelea banda la IFM katika Maonesho ya 7 ya Wiki ya Elimu ya Juu Zanzibar, yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.

Pia Mkurugenzi anaelezea huduma zinazotolewa na IFM, ukuaji wa chuo kupitia kampasi zake, ikiwemo Kampasi ya Zanzibar, pamoja na hatua mpya ya chuo ya kuanza kutoa programu za Shahada ya Uzamivu (PhD) katika fani za Management, ambazo tayari zimeanza kutolewa.

πŸ“ Karibu banda la IFM, tuzungumze kuhusu safari yako ya elimu na taaluma.

13/07/2026

TUMEHITIMISHA SABASABA, DAR ES SALAAM; … SAFARI INAENDELEA ZANZIBAR, MAONESHO YA 7 YA WIKI YA ELIMU YA JUU

11/07/2026

HAFLA YA KUWAAGA VIONGOZI WA SERIKALI YA WANAFUNZI WALIOMALIZA MUDA WAO WA UONGOZI NA KUWAKARIBISHA VIONGOZI WAPYA WA MWAKA 2026/2027

04/07/2026

IFM YALETA FURSA MPYA ZA UTAFITI NA UONGOZI WA KITAALUMA SABASABA 2026

Je, uko tayari kuifikisha taaluma yako katika ngazi ya juu zaidi?

Katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinakukaribisha kutembelea banda lake na kujionea fursa mpya za masomo pamoja na huduma mbalimbali zinazotolewa na chuo.

Miongoni mwa fursa hizo ni programu mpya za Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Menejimenti zenye maeneo yafuatayo:

πŸ“˜ PhD in Management (Accounting and Finance)
πŸ“˜ PhD in Management (Banking and Finance)
πŸ“˜ PhD in Management (Economics)
πŸ“˜ PhD in Management (Information Systems, Technology and Innovation)

Tembelea banda letu, ndani ya Jengo la Wizara ya Fedha, upate maelezo ya kina kutoka kwa wataalamu wetu na ugundue fursa zinazoweza kuinua safari yako ya taaluma na utafiti.

Karibu IFM. Karibu Sabasaba 2026.

23/06/2026

✨ TAMATI YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2026: IFM TUNAFURAHI KUKUHUDUMIA.✨

Wiki ya Utumishi wa Umma imefikia tamati leo hii tarehe 23 Juni 2026. Imeacha kumbukumbu za ushirikiano, mafunzo, ubunifu na huduma zilizowagusa wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.

Katika siku hii, washiriki walipata fursa ya kusikiliza hotuba ya Mgeni Rasmi, Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi, aliyewakilishwa na Mheshimiwa Profesa Riziki S. Shemdoe (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI.

Kwa IFM, maadhimisho haya yamekuwa jukwaa muhimu la kukutana na wananchi, kusikiliza maoni yao, kuonesha huduma na mchango wa chuo katika maendeleo ya Taifa kupitia elimu, utafiti na ubunifu.

Tunawashukuru wote waliotutembelea katika banda letu, tunawakaribisha kuwa nasi katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba 2026) yatakayoanza tarehe 28 Juni 2026 katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam, ndani ya Banda la Wizara ya Fedha.

Address

Zanzibar

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Chuo ifm posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category