Karume Institute of Science and Technology - KIST

Karume Institute of Science and Technology - KIST Karume Institute of Science and Technology (KIST) is a parastatal organisation under the Ministry of

MAADHIMISHO YA WIKI YA KITAIFA YA ELIMU, UJUZI, NA UBUNIFU 2026 , TANGA. (SIKU YA  6).Wanafunzi wa skuli mbali mbali za ...
21/08/2026

MAADHIMISHO YA WIKI YA KITAIFA YA ELIMU, UJUZI, NA UBUNIFU 2026 , TANGA. (SIKU YA 6).

Wanafunzi wa skuli mbali mbali za Mkoani Tanga, wametembelea banda la Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), na kupata maelezo kuhusu huduma zinazotolewa na Taasisi.

19/08/2026

MAADHIMISHO YA WIKI YA KITAIFA YA ELIMU, UJUZI, NA UBUNIFU 2026 , TANGA. (SIKU YA  4).Naibu Mkuu wa Chuo cha usafirishaj...
18/08/2026

MAADHIMISHO YA WIKI YA KITAIFA YA ELIMU, UJUZI, NA UBUNIFU 2026 , TANGA. (SIKU YA 4).

Naibu Mkuu wa Chuo cha usafirishaji (NIT) anehusika na Mipango, Fedha na Utawala Dkt. Zainabu Mshana, amefika katika banda la Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Karume (KIST) katika maadhimisho ya wiki ya elimu, ujuzi na ubunifu katika viwanja vya Skuli ya Usagara Tanga Mjini.

Dkt.Zainabu amesaini kitabu cha wageni katika banda la Taasisi ya Karume na kupata maelezo ya fani zinazotolewa na Taasisi.

MAADHIMISHO YA WIKI YA KITAIFA YA ELIMU, UJUZI, NA UBUNIFU 2026 , TANGA. (SIKU YA  4).Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Tekn...
18/08/2026

MAADHIMISHO YA WIKI YA KITAIFA YA ELIMU, UJUZI, NA UBUNIFU 2026 , TANGA. (SIKU YA 4).

Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Karume (KIST), Dkt.Mahmoud Abdulwahab Alawi, ameshiriki katika ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya elimu, ujuzi na ubunifu katika viwanja vya Skuli ya Usagara Tanga Mjini.

Dkt.Mahmoud amesaini kitabu cha wageni katika banda la Taasisi ya Karume na kupata fursa ya kutembelea baadhi ya mabanda ya Taasisi mbambali za elimu ya juu zilizoshiriki katika madhimisho hayo.

18/08/2026
MAADHIMISHO YA WIKI YA KITAIFA YA ELIMU, UJUZI, NA UBUNIFU 2026 , TANGA. (SIKU YA  3).Mkuu wa Chuo cha Bahari Daresalaam...
18/08/2026

MAADHIMISHO YA WIKI YA KITAIFA YA ELIMU, UJUZI, NA UBUNIFU 2026 , TANGA. (SIKU YA 3).

Mkuu wa Chuo cha Bahari Daresalaam (DMI), Prof.Tumaini Gurumo, ametembelea banda la Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume(KIST) katika viwanja vya Skuli ya Usagara Tanga Mjini.

Prof.Gurumo alipata maelezo kuhusu fani zinazotolewa katika Taasisi ya Karume, na kupongeza bunifu zilizotengenezwa na wanafunzi.

MAADHIMISHO YA WIKI YA KITAIFA YA ELIMU, UJUZI, NA UBUNIFU 2026 , TANGA. (SIKU YA  3).Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Tekn...
18/08/2026

MAADHIMISHO YA WIKI YA KITAIFA YA ELIMU, UJUZI, NA UBUNIFU 2026 , TANGA. (SIKU YA 3).

Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), Dkt.Mahmoud Abdulwahab Alawi, akipata maelezo ya kazi za ubunifu zilizotengenezwa na wanafunzi wa Taasisi ya Karume, alipotembelea banda la Taasisi katika viwanja vya Skuli ya Usagara Tanga Mjini.

MAADHIMISHO YA WIKI YA KITAIFA YA ELIMU, UJUZI, NA UBUNIFU 2026 , TANGA. (SIKU YA  2).Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Us...
17/08/2026

MAADHIMISHO YA WIKI YA KITAIFA YA ELIMU, UJUZI, NA UBUNIFU 2026 , TANGA. (SIKU YA 2).

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Usagara Tanga, wametembelea Banda la Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), kwa lengo la kujua huduma zinazotolewa na Taasisi ya Karume katika maonesho hayo, aidha walipata fursa ya kufahamu fani zinazotolewa , pamoja na kujionea baadhi ya Bunifu zilizotengenezwa.

TUPO - DOLE - KIZIMBANI - ZANZIBAR .Tarehe 15 Agosti, 2026, Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Zanzibar  wametembelea ...
15/08/2026

TUPO - DOLE - KIZIMBANI - ZANZIBAR .

Tarehe 15 Agosti, 2026, Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Zanzibar wametembelea Banda la Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST) katika maonesho ya Wakulima (NANENANE) yanayoendelea Viwanja vya Dole - Kizimbani Wilaya ya Magharibi "A" Mkoa wa Mjini Magharibi.

Wananchi hao wamepatiwa maelezo mbalimbali ya kozi zinazotolewa katika Taasisi ya Karume, pamoja na kujionea bunifu zilizofaywa na Wanafunzi wa Taasisi hiyo.

Karibu katika banda letu tukuhudumie.

KARIBU - DOLE - KIZIMBANI -  TUKUHUDUMIE.Leo tarehe 14 Agosti, 2026, Wanafunzi kutoka Skuli mbalimbali za Unguja, wamete...
14/08/2026

KARIBU - DOLE - KIZIMBANI - TUKUHUDUMIE.

Leo tarehe 14 Agosti, 2026, Wanafunzi kutoka Skuli mbalimbali za Unguja, wametembelea Banda la Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), katika maonesho ya Wakulima (NANENANE) yanayoendelea Viwanja vya Dole - Kizimbani Wilaya ya Magharibi "A" Mkoa wa Mjini Magharibi.

Wanafunzi hao wamepatiwa maelezo mbalimbali ya kozi zinazotolewa katika Taasisi ya Karume, pamoja na kujionea bunifu zilizofaywa na Wanafunzi wa Taasisi hiyo.

Karibu katika banda letu tukuhudumie.

Address

Mbweni
Zanzibar

Opening Hours

Monday 07:30 - 16:00
Tuesday 07:30 - 16:00
Wednesday 07:30 - 16:00
Thursday 07:30 - 16:00
Friday 07:30 - 16:00

Telephone

+255242230222

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Karume Institute of Science and Technology - KIST posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to Karume Institute of Science and Technology - KIST:

Share

Category