Development Foundation Programme

Development Foundation Programme

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Development Foundation Programme, Fuoni, Zanzibar City.

16/04/2015

🐓HAMASAAT🐓
Hatua ya mwanzo miongoni mwa hatua za kupata furaha ni swala.. ewe Mola tujaalie tuidumishe hadi tutakapokutana nawe
Tafuta raha yako daima kwa "kukumbatia" msahafu wako
Kwenye uhusiano wako na mtu mwingine: (kwa kadiri unavyotoa, ndivyo kadiri ya hadhari) kila mara ukizidisha kutoa, zidisha mfano wake kwenye hadhari, kwani hiyo itakufanya usizame kwenye bahari ya kitoa chako
{Na ni juu ya baba chakula chao na mavazi yao kwa sharia}
{kwa sharia}: kutokana na hali ya mwanamume, nyepesi au ngumu, halazimishwi mwenye hali ngumu asichokiweza
Akili na hekima:
Alisema Abu dardaa kumwambia Umm dardaa RA: nikighadhibika niridhie, na ukighadhibika nitakuridhia, na tusipofanya hivyo tunaweza kukosana upesi. Nani kati yetu anayetekeleza hayo?
"K**a kazi zinachosha, hakika kukaa bila kazi kunaleta uharibifu"
-omar bin al khatwab
Baadhi ya mambo hayakuumizi lakini yanakufunza,
hakika ulikuwa kwenye nia yako kuliko kawaida
Usishushe thamani ya nafsi yako kwa vile umekubali kukosolewa. Unachotakiwa ni kukubali makosa na kukubaliana na ukweli, na kuzidisha kuomba radhi ikilazimika, lakini hakuna ulazima wa kuiua nafsi yako
Mtu anayeishi kwa matumaini si kipofu wala si mwenye kuota ndoto za mchana, bali anaishi kiuhalisia; anatambua kwamba maisha pamoja na matatizo yake yote kuna suluhisho pembeni mwake
Ufupisho wa maisha
{Atakayefuata uongofu wangu hatapotea wala hatahangaika. Na atayepinga ukumbusho wangu hakika atakuwa na maisha ya dhiki}
Ewe Mola tunakuomba mwisho mwema
Ewe Mola mponye kila mgonjwa, na mfariji kila mwenye simanzi, na mruzuku kila aliyenyimwa, na ikubali toba ya kila mwenye kutubu, na upe furaha moyo wa kila mwenye huzuni, na warehemu maiti wetu na maiti waislamu
TUAMRISHANE
MEMA Inshallah

Photos from Development Foundation Programme's post 18/03/2015

Hafla ya uzinduzi wa ofisi ya mradi wa maendeleo wa waislam(Development Foundation Programme) iliyofanyika siku ya jumapili 15/03/2015 Amani zanzibar

Photos from Development Foundation Programme's post 17/03/2015

Our new Building for The development foundation programme at Amani zanzibar near Nyerere school your welcome

Photos from Development Foundation Programme's post 17/03/2015

Mafundi wakiendelea na shughli za ukarabati wa jengo hilo ambalo inshaallah litatumika kwa shughuli za maendeleo ya waislam

Photos from Development Foundation Programme's post 17/03/2015

Jengo la mradi wa mfuko wa maendeleo wa waislam
(Development Foundation Programme) zanzibar ambalo lipo Amani(Karibu na skuli ya nyerere)

Photos 13/02/2015

Ijumaa Qarim to u all.Please read to knw 10 companion who announced to enter the jannah

10/02/2015

Muengereza mmoja alimuuliza Shekhe wa kiislamu:
"kwa nini mwanamke wa kiislamu hasalimiwi na kupewa mkono na kila mwanamme"
Shekhe akajibu kwa kumuuliza:
"kwani Je kila muengereza anaweza kumsalimia na kumpa mkono malikia wa uengereza?"
Yule muengereza akajibu:
"kuna kanuni maalumu imewekwa inawataja watu wa aina saba tu katika nchi ta uengereza ndio wenye haki ya kumsalimia na kumpa mkono malikia"
Shekh akasema:
"basi na sisi ni kuna kanuni maalumu imwaainisha watu kumi na moja ndio wenye haki ya kumsalimia na kumpa mkono mwanamke"
1.baba
2.babu
3.mume
4.kaka
5.ami
6.mtoto wa kiume
7.mjukuu wa kiume wa mtoto wa kiume
8.mjukuu wa kiume wa mtoto wa k**e
9.baba wa mume
10.mtoto wa kiume wa ndugu wa kiume
11.mtoto wa kiume wa ndugu wa k**e.
Shekhe akaongeza kwa kusema:
"k**a ambavyo nyinyi munafanya hivyo kwa kumheshimu na kumtukuza malikia, basi sisi waislamu kila mwanamke kwetu ni malikia, na kaainishiwa kikanuni watu maalum wa kumsalimia na kumpa mkono ili kudhihirisha ubora na utukufu wake"
Allah Akufurahisheni enyi malikia wetu..
Utume ujumbe huu kwa wanawake wenye tabia tukufu ili waijue nafasi yao na ubora wao..

26/10/2014

Mwaka mpya 1436 Hijriya
Tumuombe Mungu atujaalie uwe ni mwaka mpya wa mafanikio kwa waislamu wote.. na Allah atupe wepesi katika kutatua matatizo yetu. Tumuombe mungu atutoe katika dhulma na tuoneshe nuru.
Aameen.

Markaz DFP Zanzibar: Wazo la leo 10/09/2014

Soma wazo la leo kupitia markazfuonizanzibar.blog

A.a. ni aibu ilioje kuona kwamba sehemu zetu za kusalia (misikiti) zinaongoza kwa uchafu.. ni kioja kuona waislamu ambao walitakiwa wafundishe umma na kuhimizana juu ya kudumisha usafi.

Markaz DFP Zanzibar: Wazo la leo

31/08/2014

A.a. ni aibu ilioje kuona kwamba sehemu zetu za kusalia (misikiti) zinaongoza kwa uchafu.. ni kioja kuona waislamu ambao walitakiwa wafundishe umma na kuhimizana juu ya kudumisha usafi.. leo wao wenyewe ndio wanao dumisha uchafu.. jamani tubadilike.. kila mtu ana waajib wa kuweka mazingira ya usafi msikitini...hassa kwenye vyoo... tuko busy kuponda dini za wenzetu lakini sisi hata usafi unatushida? Hii ni aibu na hata pepo kuipata ni mtihani ikiwa Mungu mwenyewe tunamuomba sehemu ambazo sio safi.. usafi mbele halafu na ufuate mzigo wa dua..

Want your school to be the top-listed School/college in Zanzibar City?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address


Fuoni
Zanzibar City