08/08/2026
KARIBU TUKUHUDUMIE - TUPO DOLE - KIZIMBANI - ZANZIBAR.
Leo tarehe 08 Agosti, 2026, Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Unguja, wametembelea Banda la Chuo cha Afya cha Imperial katika Maadhimisho ya maonesho ya Wakulima (NANENANE) yanayoendelea Viwanja vya Dole - Kizimbani Wilaya ya Magharibi "A".
Wananchi hao wamepatiwa maelezo mbalimbali ya kozi zinazotolewa katika Chuo cha Imperial pamoja na kupatiwa baadhi ya huduma za upimaji wa afya bure
Karibu katika banda letu tukudumie!