The State University of Zanzibar

The State University of Zanzibar Welcome to the official page of The State University of Zanzibar, established 2001, That consists of ten campuses.

28/09/2026
MAFUNZO ELEKEZI KWA TIMU 10 ZA WABUNIFU VIJANA WA SUZA YAFUNGWAChuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), kupitia Kituo c...
28/09/2026

MAFUNZO ELEKEZI KWA TIMU 10 ZA WABUNIFU VIJANA WA SUZA YAFUNGWA

Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), kupitia Kituo cha Ubunifu wa Uchumi wa Buluu (SUZA Blue Economy Innovation Hub) na Mradi wa SEBEP, kimehitimisha mafunzo elekezi ya siku tatu kwa timu 10 za wanafunzi wabunifu wa SUZA zilizochaguliwa kupitia mashindano ya ubunifu na udukuzi wa kiteknolojia (Hackathon).

Mafunzo hayo yalilenga kuwawezesha vijana hao kuboresha na kuendeleza mawazo yao ya ubunifu, kuyabadilisha kuwa bidhaa au huduma zenye thamani na kuyaandaa kwa ajili ya kuwa miradi yenye fursa za kibiashara na endelevu.

Kwa kipindi cha siku tatu, washiriki walipata mafunzo, mwongozo na ushauri kutoka kwa wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) pamoja na Chuo Kikuu cha TUB cha Ujerumani, katika maeneo mbalimbali ya ubunifu, ujasiriamali, uendelezaji wa bidhaa na huduma, mahitaji ya soko na uanzishaji wa biashara.

Kupitia mafunzo hayo, timu hizo zilipata fursa ya kutathmini na kuboresha mawazo yao ya ubunifu, kutambua mahitaji ya soko, kuendeleza bidhaa na huduma zenye thamani pamoja na kuandaa mifumo ya biashara inayoweza kukua na kuwa endelevu.

Mafunzo hayo pia yamewapa washiriki fursa ya kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu namna ya kuyabadilisha mawazo yao kutoka hatua ya ubunifu na kuyapeleka katika hatua ya utekelezaji, uzalishaji na uanzishaji wa fursa za kibiashara.

Kufungwa kwa mafunzo hayo kunaashiria hatua nyingine katika safari ya timu hizo za wabunifu, huku washiriki wakitarajiwa kuendelea kufanyia kazi mawazo yao kwa kutumia maarifa na ujuzi walioupata katika kipindi cha mafunzo.

Vijana UchumiWaBuluu UbunifuWaVijana AjiraKwaVijana Hackathon SUZAInnovationHub Innovation Entrepreneurship BlueEconomy Zanzibar

MAFUNZO ELEKEZI KWA TIMU 10 ZA WABUNIFU VIJANA WA SUZA YAENDELEAJumapili, 27 Septemba 2026, Kituo cha Ubunifu wa Uchumi ...
28/09/2026

MAFUNZO ELEKEZI KWA TIMU 10 ZA WABUNIFU VIJANA WA SUZA YAENDELEA

Jumapili, 27 Septemba 2026, Kituo cha Ubunifu wa Uchumi wa Buluu cha Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA Blue Economy Innovation Hub), kupitia Mradi wa SEBEP, kiliendelea na mafunzo elekezi kwa timu 10 za wanafunzi wabunifu wa SUZA zilizochaguliwa kupitia mashindano ya ubunifu na udukuzi wa kiteknolojia (Hackathon).

Mafunzo hayo yanaendelea kuwajengea uwezo vijana hao katika kuboresha, kuendeleza na kutekeleza mawazo yao ya ubunifu ili yaweze kuzalisha bidhaa, huduma na miradi yenye thamani na fursa za kibiashara.

Katika hatua hii, wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) pamoja na Chuo Kikuu cha TUB cha Ujerumani wanaendelea kutoa mwongozo na ushauri kwa timu hizo kuhusu uendelezaji wa bidhaa na huduma, ujasiriamali, mahitaji ya soko na uanzishaji wa biashara.

Kupitia mafunzo hayo, washiriki wanaendelea kujifunza namna ya kuyatathmini mawazo yao, kutambua changamoto na mahitaji ya soko, kuboresha bidhaa au huduma zao na kuandaa mifumo ya biashara inayoweza kukua na kuwa endelevu.

Vijana UchumiWaBuluu UbunifuWaVijana AjiraKwaVijana Hackathon SUZAInnovationHub Innovation Entrepreneurship BlueEconomy Zanzibar

 Request for Bids
26/09/2026



Request for Bids

MAFUNZO ELEKEZI KWA TIMU 10 ZA WABUNIFU VIJANA WA SUZAKituo cha Ubunifu wa Uchumi wa Buluu cha Chuo Kikuu cha Taifa cha ...
26/09/2026

MAFUNZO ELEKEZI KWA TIMU 10 ZA WABUNIFU VIJANA WA SUZA

Kituo cha Ubunifu wa Uchumi wa Buluu cha Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA Blue Economy Innovation Hub), kupitia Mradi wa SEBEP, kinaendelea na mafunzo elekezi kwa timu 10 za wanafunzi wabunifu wa SUZA zilizochaguliwa kupitia mashindano ya ubunifu na udukuzi wa kiteknolojia (hackathon).

Mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha vijana kuboresha na kuendeleza mawazo yao ya ubunifu, kuyafanyia kazi na kuyabadilisha kuwa miradi na fursa za kibiashara zenye tija na endelevu.

Mafunzo hayo yanaendeshwa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) pamoja na Chuo Kikuu cha TUB cha Ujerumani, ambao wanatoa mwongozo na ushauri kwa timu hizo katika maeneo mbalimbali ya ubunifu, ujasiriamali, uendelezaji wa bidhaa na uanzishaji wa biashara.

Kupitia mafunzo hayo, washiriki wanapata fursa ya kujifunza namna ya kutathmini na kuboresha mawazo yao, kutambua mahitaji ya soko, kuendeleza bidhaa au huduma zenye thamani na kuandaa mifumo ya biashara inayoweza kudumu na kukua.

Hatua hii ni sehemu ya juhudi za SUZA kupitia Mradi wa SEBEP katika kuwawezesha vijana kutumia maarifa na ubunifu wao kuibua fursa mpya katika Uchumi wa Buluu, kuongeza ajira na kuchangia maendeleo ya kiuchumi Zanzibar.

UchumiWaBuluu UbunifuWaVijana AjiraKwaVijana Hackathon SUZAInnovationHub Zanzibar

KAMATI YA MIRADI SUZA YAPITIA MAENDELEO YA MIRADI YA MAENDELEO YA CHUOKamati ya Utekelezaji na Usimamizi wa Miradi ya Ch...
26/09/2026

KAMATI YA MIRADI SUZA YAPITIA MAENDELEO YA MIRADI YA MAENDELEO YA CHUO

Kamati ya Utekelezaji na Usimamizi wa Miradi ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) imefanya kikao cha kupitia maendeleo, mafanikio na changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya Chuo.

Kikao hicho kimeongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, Prof. Said Ali Hamad Vuai, na kushirikisha viongozi pamoja na wajumbe wanaohusika na utekelezaji na usimamizi wa miradi ya Chuo.

Miongoni mwa miradi iliyopitiwa ni Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi (HEET), unaohusisha ujenzi wa Jengo la Skuli ya Kilimo pamoja na Jengo la Maabara za Sayansi. Miradi hiyo inalenga kuimarisha miundombinu ya kitaaluma na kuboresha mazingira ya ufundishaji, ujifunzaji na utafiti.

Aidha, Kamati imejadili maandalizi ya kuanza kwa Mradi wa BADEA, unaotarajiwa kuanza hivi karibuni na unaolenga kuboresha miundombinu ya Chuo kupitia ujenzi wa majengo mbalimbali.

Kamati pia imepitia maendeleo ya miradi inayotekelezwa kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ikiwemo ujenzi wa Dahalia za wanafunzi na Mkahawa wa Wanafunzi.

Vilevile, kikao kimepitia maendeleo ya Mradi wa Ukarabati wa Majengo ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kwa ajili ya Taasisi ya Masomo ya Bahari, iliyopo Kampasi ya Nkrumah.

Katika majadiliano hayo, wajumbe wameangazia mafanikio yaliyofikiwa, changamoto zinazojitokeza pamoja na hatua zinazohitajika ili kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa ufanisi na kukamilika kwa wakati.

HigherEducation EducationInfrastructure ResearchInfrastructure Zanzibar Tanzania

SUZA YAPITIA SERA NA MIONGOZO YA TAFITIChuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimeendelea na jitihada za kuimarisha ta...
26/09/2026

SUZA YAPITIA SERA NA MIONGOZO YA TAFITI

Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimeendelea na jitihada za kuimarisha tafiti kwa kupitia na kujadili Sera ya Tafiti pamoja na Miongozo ya Uendeshaji wa Tafiti (Research Policy and Operational Guidelines).

Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Shahada za Juu, Tafiti na Ushauri Elekezi, Eng. Dkt. Abdulrahim Haroun Ali, amesema Kurugenzi inaendelea na jitihada za kuhakikisha eneo la tafiti ndani ya SUZA linaimarika na kufikia kiwango kinachostahili kwa Chuo Kikuu.

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, Prof. Said Ali Hamad Vuai, amesisitiza umuhimu wa kuwa na sera na miongozo madhubuti ya tafiti itakayosaidia SUZA kufikia malengo yake katika utafiti, ufundishaji na ushauri elekezi.

Prof. Vuai ameitaka Kurugenzi kupitia sera hiyo na kuhakikisha inaakisi umuhimu wa tafiti katika kukabiliana na mabadiliko ya dunia na changamoto mbalimbali za jamii.

Amesisitiza kuwa tafiti ni msingi muhimu wa ufundishaji bora, akieleza kuwa wahadhiri wanapaswa kuendelea kufanya tafiti ili kuhakikisha maarifa yanayotolewa darasani yanaendana na mabadiliko na maendeleo ya wakati.

Aidha, ameeleza kuwa sera hiyo inapaswa kuweka mazingira yatakayowawezesha wahadhiri, watumishi wa utawala na kitaalamu pamoja na wanafunzi kushiriki na kunufaika na tafiti mbalimbali.

Sera na miongozo hiyo inalenga pia kuweka utaratibu wa namna tafiti zitakavyofanyika, kusimamiwa na kutumika katika kutatua changamoto mbalimbali za Zanzibar, Tanzania na dunia kwa ujumla.

Mwisho, Prof. Vuai amefungua rasmi kikao cha kupitia, kujadili na kutoa mapendekezo kuhusu Sera ya Tafiti na Miongozo ya Uendeshaji wa Tafiti (Research Policy and Operational Guidelines) ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar.

ElimuYaJuu HigherEducation Innovation Maarifa ResearchAndInnovation SUZAResearch Zanzibar Tanzania

MKUTANO MKUU WA JUMUIYA YA WAFANYAKAZI WAENDESHAJI NA WATAALAMU WA SUZA (SUZAATSA)Jumuiya ya Wafanyakazi Waendeshaji na ...
25/09/2026

MKUTANO MKUU WA JUMUIYA YA WAFANYAKAZI WAENDESHAJI NA WATAALAMU WA SUZA (SUZAATSA)

Jumuiya ya Wafanyakazi Waendeshaji na Wataalamu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZAATSA) inawataarifu wanachama wote kuwa Mkutano Mkuu wa Jumuiya utafanyika Ijumaa, 02 Oktoba 2026, katika Ukumbi wa Mikutano, Vuga, kuanzia saa 7:00 mchana hadi saa 10:30 jioni.

Wanachama wote wanaombwa kuhudhuria kwa wakati na kushiriki kikamilifu katika kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Jumuiya.

“Umoja Wetu ndio Maendeleo ya Jumuiya Yetu”

OfficialSUZA

The State University of Zanzibar (SUZA) invites researchers, innovators, academics and students to submit abstracts for ...
24/09/2026

The State University of Zanzibar (SUZA) invites researchers, innovators, academics and students to submit abstracts for the SUZA Symposium on Science, Technology and Innovations.

📅 Submission deadline: 10 October 2026
🔗 Submit here: https://forms.gle/JVzH8E934LKeoaWy8

Join us in advancing science, technology and innovation for sustainable development. Please share widely.

Technology

SUZA STAFF PARTICIPATE IN THE 6TH AFRICAN CURRICULUM ASSOCIATION CONFERENCEStaff from the State University of Zanzibar (...
24/09/2026

SUZA STAFF PARTICIPATE IN THE 6TH AFRICAN CURRICULUM ASSOCIATION CONFERENCE

Staff from the State University of Zanzibar (SUZA) have participated in the 6th African Curriculum Association (ACA) Conference held in Dar es Salaam.

The conference brings together education professionals, researchers, curriculum experts and other stakeholders to share knowledge, research findings, experiences and innovative approaches in curriculum development and education.

SUZA’s participation reflects the University’s commitment to advancing academic excellence, research, knowledge exchange and meaningful contributions to the development of education in Africa.

Research AcademicExcellence DarEsSalaam

Address

Tunguu
Zanzibar City

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when The State University of Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to The State University of Zanzibar:

Shortcuts

Share