19/08/2021
Pagali Primary School
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Pagali Primary School, Elementary School, Pagali, Zanzibar City.
19/08/2021
Uongozi wa Pagali Primary School unawatakia waisalamu wote Eid Mubaarak
TANGAZO
KWA WALE WOTE WALIO FAULU VIPAWA NA MICHIPUO KWA SKULI ZA SERIKALI ILI KUWEZA KUJUA SKULI WALIZOPANGIWA WATEMBELEE TOFUTI YA WIZARA YA ELIMU
AU
BOFYA LINK IFUATAYO:
https://moez.go.tz/documents/mchepuo2020.pdf
Source: Wizara ya Elimu Zanzibar
TANGAZO
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali inawatangazia wananchi wote leo ifikapo Saa 10 jion itatoa Matokeo kwa wanafunzi waliofaulu Vipawa na Michipuo kupitia ZBC Radio.
N.B kwa wanafunzi wa Skuli za private waliofaulu Vipawa na Michipuo wafike Wizara ya Elimu kuanzia kesho tarehe 4/2/2021 kuchukua barua zao.
Source
Page ya wizara ya elimu
26/01/2021
Matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Pili, Darasa la Sita na Darasa la Nne.
Bofya Link ifuatayo:
*TAARIFA YA MHESHIMIWA SIMAI MOHAMMED SAID WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR KWA UMMA LEO SIKU YA IJUMAA TAREHE 15 JANUARI 2021*
Ndugu Wananchi
Wazazi na Walezi
Walimu na Wanafunzi
Assalamu Alaykum;
Ifuatayo ni Taarifa Maalum kuhusu uratibu na uendeshaji wa Masomo kwa mwaka 2021. K**a mjuavyo kuwa skuli zote za Serikali na Binafsi zitafunguliwa rasmi Siku ya Jumatatu ya Tarehe 18 Januari 2021 na kumaliza Muhula wa masomo tarehe 10 Disemba 2021.
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imepanga Kalenda ya Masomo mwaka 2021 kuwa na Mihula miwili ambayo itakuwa na shughuli zifuatazo:
Jumla ya Wiki za Masomo 43
Jumla ya Wiki za Mapumziko 07
Jumla ya Siku za Masomo 213
Jumla ya Siku za Mapumziko 42
Jumla ya Siku za Maadhimisho ya Kitaifa 13
INDHARI/ZINGATIA
Siku za Mwezi Mtukufu wa Ramadhan Masomo yataanza Saa 1:30 Asubuhi hadi Saa 4:30 Asubuhi kwa Mkondo wa Asubuhi na kwa Mkondo wa Mchana Masomo yataanza Saa 5:00 Asubuhi hadi Saa 8:00 Mchana na Skuli zenye Mkondo Mmoja Masomo yataanza Saa 2:00 hadi Saa 7:00 Mchana.
Ndugu Wananchi, Wazazi na Walezi, Walimu na Wanafunzi
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali inawaomba kuzingatia mambo yafuatayo ili kufikia lengo lililokusudiwa la kutoa Elimu Bora kwa Jamii.
i. Skuli zote za Serikali na Binafsi kuhakikisha kuwa zinafuata Mitaala na Mihutasari rasmi iliyoidhinishwa na Serikali na kukamilishwa kwa wakati uliowekwa ili wanafunzi wamalize masomo yao kwa muda uliopangwa.
ii. Tunawaomba Wazazi, Walezi, Walimu na Wadau wengine wa elimu washirikiane kwa pamoja katika malezi ya watoto wetu ili kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora itakayowajengea ufahamu na kuwawezesha wanafunzi kuikabili vyema mitihani yao ya mwisho wa mwaka na kupata maarifa ya ziada kutokana na elimu hiyo.
iii. Skuli binafsi zinashauriwa kuzingatia ada zao za masomo kulingana na hali ya maisha iliyopo kwani Skuli zetu zipo kwa lengo la kutoa huduma kwa jamii na kuendelea kuisaidia Serikali katika lengo lake la kutoa elimu bora kwa watu wote.
iv. Ninazishauri Skuli za Serikali na za Binafsi ambazo wanafunzi wake wanatarajiwa kufanya mitihani ya Taifa ya Kidato cha Sita mwezi wa Mei 2021 kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliosajiliwa wanaruhusiwa kufanya mitihani yao bila ya kikwazo chochote.
v. Wizara inatoa agizo kwa uongozi wa skuli zote za Binafsi zinazotumia usafiri wa mabasi kwa wanafunzi kuhakikisha kuwa wanapakia wanafunzi kwa idadi husika k**a inavyotakiwa na Idara inayohusika na usalama barabarani. Skuli yoyote ambayo itapakia wanafunzi zaidi ya uwezo wa basi husika taratibu za kisheria zitachukuliwa dhidi ya skuli hiyo. Aidha, tunazitaka skuli zote zinazotumia usafiri wa mabasi kuweka alama ya utambulisho wakati wanapowapakia wanafunzi.
vi. Wizara inawashauri Wazazi na Walezi kutowapa vyombo vya moto wanafunzi ambao hawajafikia umri wa miaka 18 ili kuepusha madhara yatakayojitokeza. Wizara pia inazishauri Mamlaka zinazosimamia suala la usalama barabarani zichukue hatua zinazostahiki kwa mujibu wa sheria zilizopo.
vii. Ninaagiza kuwa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kufanyike usafi wa nguvu katika maeneo yote ya majengo ya Taasisi zinazotoa Elimu kuanzia Maandalizi hadi Vyuo vikuu kwa Unguja na Pemba. Pia natoa agizo la kila Jumamosi ya wiki katika maeneo ya dakhalia zote kufanya usafi maalum kutokana na kuonekana kuwa katika hali mbaya. Mwisho nawaagiza walimu wakuu wa skuli zote za Serikali na za Binafsi zipange ratiba zao na pia nawataka Maafisa Elimu kusimamia zoezi hili.
Nawashukuru wananchi wote na wadau wa elimu kwa mashirikiano wanayoyatoa katika kuendeleza juhudi za elimu nchini.
‘Elimu Bora kwa Maendeleo ya Taifa’
Naomba kuwasilisha.
Matokeo ya kidatu cha nne 2020 yametoka
“Ninajutia sana kuipoteza kazi yangu iliyopita. Kwa sababu niliipoteza kwa uzembe wangu. Ni kazi iliyokua inanilipa vizuri na niliipenda mwanzoni.
Ofisi iliniamini kwa sababu nilionyesha uwezo mzuri. Na kipindi kile nilitengeneza connection nyingi sana. Ilifika mahali nikaanza kuizoea ile kazi. Nikapunguza umakini na kutokuzingatia. Nikawa siiogopi tena ile kazi. Niliamini ofisi haiwezi kuniachilia na hata wakiniachilia nitapata kwingine kwa sababu tayari nina connection.
Baada ya mkataba kuisha sikuongezewa mkataba. Sikushtuka kwa sababu nilijua nitapata tu connection.
Unaenda mwaka wa pili sasa sijapata ajira kila connection yangu naambiwa nisubirie bado hawana nafasi. Ninajuta na nimejifunza somo la uwajibikaji kwa maumivu sana.” -Kian
28/12/2020
UTEUZI:
28/12/2020
TANGAZO MAALUM.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt. Idrissa Muslim Hija, anawatangazia walimu, wazazi na wanafunzi wote kuwa Skuli zote zitafunguliwa tarehe 18/01/2021.
Pia Wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha pili wanatakiwa na wao kuripoti Skuli siku hiyo na walimu wawaingize kidato cha TATU.
Yakitoka matokeo kwa wanafunzi waliofaulu wataendelea na kidatu cha TATU na waliofeli watarudia kidatu cha pili.
Hivyo walimu wakuu wote mnatakiwa kuwajua wanafunzi wote wasiofanya mtihani na sababu zao ziwe za msingi ili Wizara ikichukua hatua iwe na takwimu sahihi.
20/12/2020
Sherehe za ndani za wanafunzi ambazo zimejumuisha kuwapa zawadi wanafunzi waliofaulu darasa la sita
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Website
Address
Pagali
Zanzibar City