09/09/2025
Ndugu Wazazi wa wanafunzi wanao tarajia kuhitimu darasa la saba 2025!
Kwanza kabisa, hongereni sana kwa hatua kubwa ya kuhitimu elimu ya msingi! Hii ni hatua ya kujivunia sana, lakini pia ni mwanzo wa safari nyingine muhimu sana – safari ya elimu ya sekondari.
Tunapenda kuwa karibisha sana NTONZO sekondari kwaajili ya kozi fupi ya Pre-Form One, itakayo anza tarehe 15/9/2025 na kumalizika tarehe 19/12/2025 kwa gharama ysa 200,000/= tuu
Kwa nini uchague kujiunga na Pre-Form One Ntonzo sekondari?
âś…Mazingira Bora ya Kujifunza
Shule ya Ntonzo ina vyumba vya madarasa vilivyo na utulivu na vifaa vinavyohitajika. Kuna walimu waliobobea ambao wamejitoa kukuandaa vyema kabla hujaanza Kidato cha Kwanza.
âś…Maandalizi Madhubuti
Kupitia Pre-Form One, utajifunza masomo ya sekondari mapema, jambo litakalokusaidia kuanza Kidato cha Kwanza ukiwa tayari kabisa – kwa uelewa, ujasiri na kasi ya kusoma.
âś…Walimu Wenye Uwezo na Moyo
Tunao walimu wanaojali mafanikio ya kila mwanafunzi mmoja mmoja. Wanajitahidi kuhakikisha kila mwanafunzi anaelewa, hata kwa kutumia muda wa ziada.
âś…Shule ya Kufaulisha
Ntonzo inatambulika kwa matokeo bora ya mitihani ya taifa na maadili mazuri ya wanafunzi tangu kuanzishwa kwake. Tunakuandaa kitaaluma na kinidhamu kwa maisha ya baadaye.
âś…Malezi Bora na Maadili
Mbali na masomo, tunawalea wanafunzi wetu kwa maadili mema ya kidini, nidhamu ya hali ya juu, na kuwajenga kuwa raia wema wa baadae.
ndugu Mzazi na mwanafunzi,
Usikose fursa hii muhimu ya kujitayarisha mapema kwa elimu ya sekondari katika mazingira salama, yenye walimu bora, na rafiki kwa mwanafunzi.
Jiunge na sini kwa masomo ya Pre-Form One sasa.
Kwa maelezo zaidi, fika shuleni au wasiliana nasi kupitia namba zifuatazo:
0758657459
0623243643
0710834649
📍 Shule inapatikana mbeya, pembezoni mwa barabara kuu iendeyo Tukuyu km6 kutoka njiapanda uyole.
Karibu sana – Ntonzo sekondari hapa ni chaguo sahihi!