Itete Primary School Alumni Association

Itete Primary School Alumni Association

Comments

HONGERENI SAANA WANABUSOKELO.

Is the association which brings together graduates of ITETE primary school from different parts of east Africa, and from various parts of the world,

Are you a graduate of Itete primary school If YES, you are, by virtue of this, a member of Itete primary school alumni association and, as such, you have a stake in the affairs of your school

Itete primary school alumni would like to keep close contact with you and to send you information about what is currently happening at your School as well as regarding other school graduates. To provide you

Operating as usual

03/04/2017

Uyole Cultural Tourism Enterprises

Tourist information centre

20/04/2015

Wana alumni ambao ukiwatizama leo huwezi kudhani k**a ndio hawa. Hii ni siku ya mahafali wahitimu wa 2005 wakitumbuiza katika ngoma, unakumbuka nini miaka hiyo?

18/04/2015

Hii ni moja kati ya picha ambayo wana alumni walipiga kipindi wako shuleni itete. Je wadau hawa ni kina nani?
Kumbukumbu ya itete ps

surveymonkey.com 22/03/2015

MEMBERSHIP REGISTRATION FORM FOR ITETE ALUMNI Survey

surveymonkey.com To join the Alumni Association, complete and submit the form below. All fields are required.

[03/21/15]   ITETE ALUMNI ASSOCIATION
TAARIFA FUPI YA UTENDAJI.
Tunamshukuru Mungu ambaye ametukutanisha tena kupitia umoja huu. Tunajua ni muda mrefu umepita tangu baadhi yetu tuhitimu na kwa nyakati tofauti, lakini umoja huu umefufua mahusiano na ukaribu wetu ambao ulikuwa ukififia siku hadi siku.

Taarifa hii imegawanyika katika sehemu kuu tano;
1. Malengo
2. Mafanikio
3. Changamoto
4. Matarajio
5.Hitimisho

1.MALENGO
Tulipoanzisha umoja wetu tarehe 16/01/2015 na kuchagua viongozi wetu wa muda, tuliweka malengo kadhaa yakiwemo haya yafuatayo;
>kutembelea shule yetu mara mbili kwa mwaka
>kukumbukana na kusaidiana katika nyakati zote(furaha na huzuni)
> kupanua uwanja wa mawasiliano kwa kuwa na page Facebook na group watsap
>kuwatembelea walimu wastaafu

2. MAFANIKIO
Tunamshukuru Mungu ametuwezesha kufanikisha haya machache ndani ya kipindi hiki;
>Tumefanikiwa kuitembelea shule yetu mara moja. Shukrani za pekee kwa ndugu zetu waliotuwakilisha katika hili
>Tumefanikiwa kwenda kughani msiba wa ndugu yetu kipenzi marehemu BARAKA MWAKAJILA
>Tumefanikiwa kufungua page ili kupanua wigo wa mawasiliano na kufanya umoja ujulikane hata na wale ambao hawako what's app
>Tumefanikiwa kuwatembelea walimu wote wastaafu wakiwemo mwasumbwe, mwamaso, mwakasitu, igumi na mwalumuli.

3. CHANGAMOTO
Daima mwanzo ni mgumu, na kwakuwa umoja wetu ndo unaanza tumekumbana na changamoto kadhaa mpaka sasa lakini hatukati tamaa maana tunajua ugumu wa kuasisi jambo ndo mafanikio makubwa ya baadaye. Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na
>Tofauti ya ratiba za kazi na masomo miongoni mwa wanachama jambo ambalo linafanya baadhi ya wanachama kukosa matukio na vikao muhimu
>kukosekana kwa vyanzo mbadala vya mapato ili kupunguza mzigo kwa wanachama

4. MATARAJIO
Tunatarajia kuwa na ziara nyingine ya kuitembelea shule yetu katika mwezi wa tisa (September), ili watu wengi wapate nafasi ya kushiriki maana tunaamini kuwa walio masomoni, mwezi huo wengi watakuwa likizo. Na tayari vikao vya maandalizi vimeanza.

5.HITIMISHO
Mwisho tunapenda kuwashukuru tena wanachama kwa ushirikiano wenu ambao umetufikisha hapa tulipo.
Hu ni mwanzo wa safari yetu hivyo tunaomba ushrikiano wenu zaidi. Hiyo ziara ya September naomba tujitoe kwa michango na kutenga muda wetu kwenda itete. Tunatamani tuende wengi kadri iwezekanavyo.
Uongozi unawatakienyi nyote majukumu mema, mkono wa Mungu usipungue juu ya kila mgusalo! Asanteni

Imeandaliwa na uongozi wa ITETE PRIMARY SCHOOL ALUMNI

14/03/2015

Tulipokuwa tunafika kwa mwalimu mwalumuli, kiukweli alifurahi sana tena sana. Tumepiga sana story akakumbushia mengi ya nyuma pia tukamkumbusha mengi tukaishia kufurahi pamoja, hatuna la ziada tunawapenda sana walimu wetu Mungu awape maisha marefu

01/03/2015

Tulifurahi sana kuwaona wapendwa wetu ikatubidi tukae katika moja ya viunga ili kuweza kushare mawili matatu. Tunawapenda sana tunaisubiri awamu ya pili ya mwezi wa tisa.

28/02/2015

We had northing to give them, ila tukaona tuwasalimu, tuwashike mikono kisha tupige story. Tunawapenda sana WALIMU NA WANAFUNZI WA ITETE

26/02/2015

Tupende kutoa shukrani za dhati kwa uongozi wa shule yetu, bodi ya shule,mkuu wa shule MLM MWASIMANGA na walimu wote kwa kazi mfanyazo na pia kwa kutupokea tulipofika kuitembelea shule yetu. Katika picha no 1, ni walimu event zikiendelea lakini picha no 2 ni picha ya pamoja walimu na wawakilishi wa itete alumni.

23/02/2015

Tupende kutanguliza Shukrani za dhati kwa HAKI ELIMU Dar es salaam, kwa msaada wa hali na mali katika kufanikisha malengo yetu kwa kutupa vitu vifuatavyo ili kusaidia walimu na wanafunzi katika shule ya msingi Itete.

1. Broken promises in primary education copy 44
2. Ugawaji wa walimu wapya je umezngatia mahtaj 66
3. Unafany nn kuboresha elimu 25
4. Mwaka mmoja wa matokeo makubwa sasa je unatekelezwa ipasavyo 50
5. Kuboresha shule zetu 59
6. Ahadi za serikali 2015/2014 copy 29
7.nyarere kuhusu elimu vitabu 15
8. Ruzuku ya wanafunzi 96
9. Kalenda 77.
10. Radio ya solar 1

22/02/2015

Safari yetu ya kutoka TUKUYU MJINI kuelekea ITETE ilikuwa hivi mara baada ya kufika maeneo ya NSYASYA tukakuta wanatengeneza barabara na bahati mbaya mvua ikanyesha ikatubidi kushuka na kusukuma gari maana ilikuwa inakwama kwa sababu ya matope.

[02/21/15]   Ratiba yetu itakuwa k**a ifuatavyo, tutaanza kwa kufika nyumbani kwa mzee wetu mwakajila ili kuweza kusalimia baada ya kufiwa na mwanae mpendwa BARAKA MWAKAJILA aliekuwa mwanafunzi mwenzetu,

Kisha Tutawatembelea walimu wastaafu wakiwemo Mlm MWAMASO, MWASUMBWE, MWAKASITU na IGUMU.

kisha mida ya saa sita tutawasili rasmi ndani ya shule yetu SHULE YA MSINGI ITETE, Get ready for alot of suprizeeeee

k**a kuna mtu tulisoma nae na wajua yupo kule tunaomba namba yake ili tujumuike pamoja nae. Asante.

18/02/2015

Ipi ilikuwa style yako ya kubeba mfuko wa madaftari?

thecitizen.co.tz 18/02/2015

Bye Std VII exams, English; Karibu Kiswahili in studies

thecitizen.co.tz >The newly-launched education system has abolished national examinations for primary school leavers and extended basic education to four years at secondary level—meaning students will sit their final examination after 11 years in primary and secondary school.

18/02/2015

Hapa ndipo ilikuwa na bado ni assembly ground kwa lugha nyepesi paliitwa mstarini.

Muwakilishi wetu tayari yupo mazingira haya kwa ajili ya maandalizi ya ufunguzi lasmi wa alumni katika shule yetu.

[02/18/15]   Wafuatao ndio waliofanya Registration
1. Amos Asajile
2. Richard Emmanuel
3. Joel Andwilege
4. Chishimba Mwasambungu
5. Peter mwasuga
6. Grace mwakapeje
7. Twijisye george
8. M***a william
9. Matilda paul
10. Breath mwantolwa
11. Rehema asajile
12. Bosa abel
13. Shedrack daimon.

bbc.co.uk 17/02/2015

Sera mpya ya elimu yazua maoni Tanzania

bbc.co.uk Sera mpya ya elimu nchini Tanzania iliyozinduliwa inazidi kuzua maoni mchanganyiko

17/02/2015

Hii ndio Tshert yetu ya itete primary school alumni asaociation.

Nani anaweza kutolea maana ya hii logo katikati?

14/02/2015

moja kati ya vitabu vilivyowahi kupendwa ni PAZI NA JOGOO je wakumbuka nini katika kitabu hiki?

01/02/2015

TOKOMEZA ZIRO

Wimbo wa Tokomeza Zero wenye lengo la kuburudisha, kuelimisha na kuitaka jamii kuipa sekta ya elimu kipaumbele kwa maendeleo ya Taifa. Wimbo huo umeimbwa na ...

[01/31/15]   MANENO YA KISWAHILI.

Baada ya kusahau nywila(password) ya kadi yangu ya kiotomotela(ATM) nikaamua kukaa mgahawani(restaurant) jirani na kilipo kiotomotela na kuagiza vibanzi(chips)vikavu na sharubati(juice) baridi sana!Nikiwa nasubiri kuletewa nikafungua kipakatalishi(laptop) changu na kujaribu kufungua diski mweku(local disk) iliyogoma kufunguka kwa wakati huo.Nikafungua diski tepetevu(floppy/hard disk) na kukuta imevamiwa na mtaliga(virus),nguvu ikaniishia nikashindwa hata kushika wala kupalaza kisharazio(cursor).Siku yangu ikaishia hapo na nikaishia kusahau hata vibanzi na sharubati nilivyoagiza.

Tuandikie neno lingine kiswahili na kiingeleza chake

29/01/2015

Itete Primary School Alumni Association's cover photo

29/01/2015

Itete Primary School Alumni Association

29/01/2015

HakiElimu

Tafakari nasi katika tangazo hili la dakika moja. Mwanafunzi kuhitimu darasa la saba bila kujua kusoma, kuhesabu na kuandika, Je ni kosa la Mwanafunzi, Mzazi, Mwalimu au Serikali? K**a wewe ni mtumiaji wa simu yenye mtandao wa whats app tuma ujumbe ulioandikwa Wajibu wetu Sote katika number 0753-107912 nasi tutakutumia tangazo hili bure na ulisambaze kwa wapenda elimu nchini kote.

29/01/2015

Uongozi wa itete alumni association kwa kushirikiana na wadau mbali mbali(walimu, wazazi na wanafunzi) umeandaa mfululizo wa matukio k**a ifuatavyo:-

20/02/2015 (alumni Gathering) Kuonana wana alumni wote mkoani mbeya na kumtembelea mwalimu mwalumuli.

23/02/2015 kuwasili rasmi katika shule ya itete, ambapo events kadhaa zitafanyika.

24/02/2015 ni kilele cha safari zetu tutawatembelea walimu wastaafu(mwl mwamaso, igumi na mwakasitu) ikiambatana na lunch party, Kisha jion kufunga siku kwa kutembelea ziwa kiungululu.

Mabadiriko yoyote tutawafahamisha. Asanteni kwa mawasiliano zaidi 0755993816 musa otete

28/01/2015

MEMBERSHIP REGISTRATION FORM FOR ITETE ALUMNI Survey

Habari, Pole na mihangaiko ya kutwa tunatoa shukrani kwa wale wote mliojaza membership form. Tunawakumbusha wale ambao bado kujaza kabla ya dead line ya tarehe 04/02/2015

Namna ya kujaza hiyo membership fomu fuata maelezo yafuatayo

Click hiyo link kisha itafunguka na kuleta vibox vya kujaza

Hakikisha unajaza sehemu zote, usiache hata moja

Ukimaliza chini kabisa utaclick done inakuwa imefika.
https://www.surveymonkey.com/s/FXYGJYV
Upatapo taarifa hii mtaarifu na ndugu/jamaa/rafiki.

surveymonkey.com To join the Alumni Association, complete and submit the form below. All fields are required.

[01/28/15]   Mtoto: Mwalimu mimi nataka
nisome darasa la
nne kwani hili la3 halinifai.
Mwalimu: Kwa nini unasema
hivo?
Mtoto: Nina akili...
Basi mwalimu kamueleza mkuu
wa shule na
mkuu kaitisha interview kwa
dogo.
Maswali ni haya....
Mwalimu: Kwenye ndege kuna
matofali 20
tukitoa moja tukalidondosha
chini yatabaki
mangapi?
Dogo: Yatabaki 19.
Mwalimu: Nipe hatua za
kumuweka tembo
kwenye friji.
Dogo: Unafungua friji unamuweka
tembo kisha
unafunga.
Mwalimu: Nipe hatua za
kumuweka nyani
kwenye friji.
Dogo: Unafungua friji unamtoa
tembo
ulemuweka..unamueka nyani kisha unafunga
friji.
Mwalimu: Kuna sherehe ya siku
ya kuzaliwa
kwa simba, wanyama wote
wameenda kasoro
mmoja. Ni nani na kwa nini?
Dogo: Ni nyani kwa sababu
tumemuweka
kwenye friji.
Mwalimu: Bibi kizee amevuka
mto unaokuwaga
na mamba na viboko wakali,
aliwezaje?
Dogo: Aliweza kwani mamba na
viboko nao
walienda kwenye sherehe ya
kuzaliwa kwa
simba.
Mwalimu: Ingawa bibi kizee
alivuka mto,
baadae alikufa. Unadhani kwa
nini?
Dogo: Alidondokewa na lile tofali
tulotoa
kwenye ndege na kutupa chini.
Mwalimu mkuu:

ungekuwa wewe mwalimu mkuu ungempanga darasa gani huyu mwanafunzi?

27/01/2015

Wimbo: K**a mnataka mali mtayapata shambani

1. Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafe maishani.

2. Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
Hata k**a nikichanjwa, haitoki homa kali,
Roho naona yachinwa, kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini, kiwafae maishani.

3. Yakawatoka kinywani, maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani, sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani, mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali, itufae maishani? (P.T)

4. Baba aliye kufani, akajibu lile swali,
Ninakufa maskini, baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni, k**a mnataka mali,
K**a mnataka mali, mtayapata shambani.

5. Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
Akili zetu nyembamba, hazijajua methali,
K**a tunataka mali, tutapataje shambani?

6. Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali,
Haya sasa buriani, kifo kimeniwasili,
K**a mnataka mali, mtayapata shambani.

7. Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli,
K**a mnataka mali, mtayapata shambani.

8. Fumbo wakatafakari, watoto wale wawili,
Wakakata na shauri, baada ya siku mbili,
Wote wakawa tayari, pori nene kukabili,
K**a mnataka mali, mtayapata shambani.

9. Wakazipanda shambani, mbegu nyingi mbalimbali,
Tangu zile za mibuni, hadi zitupazo wali,
Na mvua ikaja chini, wakaona na dalili,
K**a mnataka mali, mtayapata shambani.

10. Shamba wakapalilia, bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia, wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia, wakakumbuka kauli,
K**a mnataka mali, mtayapata shambani.

11. Wakanunua na ng'ombe, majike kwa mafahali,
Wakapata na vikombe, mashine na baiskeli,
Hawakuitaka pombe, sababu pombe si mali,
K**a mnataka mali, mtayapata shambani.

12. Wakaongeza mazao, na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao, wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao, wakaandika kauli,
"K**A MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI".
Powered by: Itete primary school alumni association.

Tuimbe pamoja wimbo huu kisha tuambie wakumbuka nini?

26/01/2015

MEMBERSHIP REGISTRATION FORM FOR ITETE ALUMNI Survey

From IT department, Tunaandaa DATA BASE yetu tafadhari jaza fomu hii ONLINE kwa usajili. https://www.surveymonkey.com/s/FXYGJYV au tutumie inbox taarifa zako zote muhimu ikiwemo, jina, umri, jinsia, mahali ulipo, mwaka uliomaliza shule, taja walimi watatu unao wakumbuka. asanteni sana

surveymonkey.com To join the Alumni Association, complete and submit the form below. All fields are required.

[01/26/15]   Habari, k**a wewe umesoma Itete primary school na ungependa kuungana nasi katika group ya watsap ya itete primary school alumni association tafadhari tuma jina lako kamili inbox au kwenda namba 0682416629.kisha tutashughurikia ombi lako, asante sana

[01/26/15]   Moja kati ya nyimbo tunazo zikumbuka ni pamoja na huu wa kuingilia madarasani.

Mwenda itete nani? x2
Nimpe barua yangu x2
Kwa mwalimu wangu mwasumbwe wa itete.

sisi wa hapa itete x2
mwalimu katufundisha x2
a, e, i, o, u ndio mwanzo wa maarifa.

Hapo safu ya wapiga ngoma ikiwa na M***a otete ngoma ndogo(perekete), Frank kapyungu ngoma kubwa (ing'oma), filimbi akiwa dada garce reuben na shani adolf.

K**a wakumbuka wimbo wowote wa shule uliosoma waweza andika hata mistari miwili tu.

[01/25/15]   Dear alumni members, friends and teachers am here by to introduce to you my fellow leaders of this association.

Joel andwilege
Chair person

Rehema joel
Secretary

M***a otete
Treasurer

Amosi asajile
Information and communication technology.

Your both welcome to join our family, from alumni chairperson.

25/01/2015

Tulipokuwaa shule ya msingi tulijifunza hadidhi nyingi sana na walimu mbali mbali, je wewe waikumbuka hadidhi gani kati ya hizi?
1. MKWAWA SHUJAA
2. PAZI NA JOGOO
3. MUWA ULIOZAMISHA MELI
4. AWAFU MWENYE NGUVU
5. SIKU YA GULIO
6. WATOTO WAGEUKA MAWE
7. SIZITAKI MBICHI HIZI
8. TOLA ANAKULA GIZANI
9. MKUTANO WA WANYAMA
10. NANI ATAMFUNGA PAKA KENGELE
11. MFALME NGURUMO
12. SADIKI NA CHITEMO
13. JUA NA UPEPO
Ongeza nyingine unayoikumbuka ikiwezekana na mwalimu aliekufundisha.

[01/24/15]   SOME FEW QUESTIONS YOU MIGHT BE ASKING YOUR SELF
1. What are the criteria to join the Itete primary Schools Alumni Association as a member?

Ans: You are eligible to join the Itete primary Schools Alumni Association as a member if you are a former student of itete primary school

2. Is there a required minimum period of study in itete primary school to join Itete primary Schools Alumni Association?

Ans: No. As long as you have studied in itete primary school for any period of time, you are qualified to join the alumni association as a member.

[01/22/15]   Dear member,
I would like to firstly congratulate you on registering as a Itete Primary School Alumni member. One of Itete alumni association’s main objectives is to enhance and maintain links among members of the alumni and the school, there fore roles of the association are:

1. To enhance friendly learning environment, through developmental projects, educational programs, and facilities improvements.

2. To reach, serve and engage all alumni, teachers, parents, of Itete primary school by fostering intellectual connections and peer mentoring. To join our big Family click LIKE

Joel Andwilege Mwakalebela
Alumni chair person.

Location

Category

Products

One of Itete alumni association’s main objectives is to enhance and maintain links among members of the alumni and the school, there fore roles of the association are:

1. To enhance friendly learning environment, through developmental projects, educational programs, and facilities improvements.

2. To reach, serve and engage all alumni, teachers, parents, of Itete primary school by fostering intellectual connections and peer mentoring.

Address


170
Tukuyu
Other Tukuyu schools & colleges (show all)
Kiwira Internet CAFE - Kiwiranet Kiwira Internet CAFE - Kiwiranet
505 TUKUYU
Tukuyu, 53515

We want to reach you no matter were you are or from, for the best services ever through the internet

Bujinga secondary school Bujinga secondary school
P.O.BOX 483 TUKUYU
Tukuyu

#YETU WOTE <3 <3 je unaipenda shule yako? k**a jibu ni NDIO fanya kuLIKE PAGE hii BUJINGA SECONDARY SCHOOL S.L.P 483 TUKUYU

Imanuel Nursery And Farm Imanuel Nursery And Farm
Po Box 153
Tukuyu, 255

We supply Fruit tree seedlings like Avocado, Mango, Macadamia, cashew etc. We also deal with Fish farming, Spice Farming, Vegetable and Fruit Farming.