16/04/2022
TUJIFUNZE KITU HAPA.
Nimebahatika kupita baadhi ya miji na maeneo japo machache ya Tanzania yakiwapo Arusha, Nachingwea-Lindi, Dodoma, Morogoro n.k
Aidha nimekaa kwa mda mrefu Kidogo katika jiji la Dar es salaam nilikosoma chuo tofauti na hayo maeneo mengine ambayo baadhi yao nilikuwa napita tu.
Kubwa ninalotaka ku-share nawe hapa ni swala zima la utafutaji. Kuna utofauti mkubwa sana kati ya kutafuta riziki na kutafuta maisha(mafanikio).
Katika nyakati tofauti tofauti nimekuwa nikishuhudia watu ambao kimsingi umri umeenda(wamama na wazee) wakisambaza bidhaa rejareja kuviuza (k**a vile mashuka, viatu, vyombo vya ndani n.k).
Wamekuwa wakifanya katikati ya jua kali la jiji la Dar es salaam ili walau kila jioni wawe na uhakika wa kula.
Siwalaumu, ninawapongeza, kwani kupitia kwao nimejifunza kitu kikubwa sana ambayo nimeona niwashirikishe nanyi vijana wenzangu. NI KWA HABARI YA KUPAMBANA ANGALI ASUBUHI KABLA HALIJAKARIBIA KUZAMA JUA. Tukubali kuvuja jasho vijana wenzangu kwa umri huu ili baadae tupate mda wa kupumzika na kujivunia mapambano yetu ya ujanani.
Siku zote tujifunze kutumia muda na fursa kwa faida.
Nirejelea kidogo kwenye Biblia, WAEFESO 5:15-16
"Lakini angalieni mnavyoenenda, siyo k**a wasiyo na hekima, bali k**a wenye hekima... Huku mkiukomboa wakati mana zama hizi ni za uwovu"
Kijana ni mimi na wewe, TUPAMBANE.