Vifrem Entrepreneurship Training Agent

Vifrem Entrepreneurship Training Agent

Non Government Organization conerning with providing education about health, enterpreneurship, psychology, agriculture and livestock keeping advice

Operating as usual

27/08/2019

Farming Enterpreneurship Tanzania - FET

UFUGAJI BORA SAMAKI AINA YA SATO

1.0 UFUGAJI WA SAMAKI
Ø Ni kitendo cha kuzalisha samaki katika mabwawa, matenki au Mifereji kwa lengo la chakula au kujipatia kipato

1.1 UMUHIMU WA UFUGAJI WA SAMAKI
Ufugaji wa samaki unazo faida mbalimbali ambazo ni:-
Ø Kujipatia chakula bora na cha kutosha kwa ajiri ya familia na jamii.
Ø Njia bora ya kujiajiri na kujiongezea kipato kutokana na mauzo ya samaki.
Ø Hutoa fursa ya matumizi ya ardhi isiyofaa kwa ajili ya kilimo.
Ø Ufugaji wa samaki hutoa nafasi ya kilimo mseto cha samaki na mazao/mifugo kwa wakati mmoja katika eneo moja, hivyo kutoa mavuno mengi.

1.2.0 MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA UFUGAJI WA SAMAKI;
1.2.1Mtaji
Ø Mkulima anashauriwa kuhakikisha kuwa ana mtaji kabla hajaamua kufanya ufugaji wa samaki, kiwango cha mtaji kitategemea ukubwa wa mradi husika.

1.2.2 Soko
Ø Ni vyema kujua upatikanaji wa soko pamoja na washindani wako kabla ya kuanzisha shughuli hii, japo kwa nchi yetu soko la samaki ni kubwa sana, hii inatokana na uhitaji mkubwa wa samaki katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

1.2.3 Elimu
Ø Mkulima anapaswa kuwa na elimu ya kutosha kuhusu samaki na jinsi ya kufuga ili aweze kuendesha mradi kwa urahisi, hivyo mkulima anaweza kutafuta mtaalam kutoka vyuo vya serikali au binafsi.

1.2.4 Upatikanaji wa mbegu(vifaranga) pamoja na chakula.
Ø Mkulima anashauriwa kuwa na uhakika wa upatikanaji wa mbegu bora na chakula cha kutosha kwa ajili ya kulisha samaki.

1.2.5 Eneo la kufugia samaki
Ø Ni vyema pia kutafuta eneo zuri kwa ajili ya kuchimba bwawa la kufugia samaki kwa kuzingatia upatikanaji wa maji kwa wakati wote wa msimu wa ufugaji, aina ya udongo, usalama na upatikanaji wa miundombinu husika (barabara, nishati ya umeme).

2.0 AINA YA SAMAKI;
2.1 Utafiti umefanyika katika nchi nyingi na kuonelea kuwa samaki aina ya perege/ngege/sato [tilapia] anafaa kufugwa katika mabwawa kulinganisha na aina nyingine.

2.2 Samaki wa aina hii wana sifa nzuri sana kwani; huishi kwenye maji yenye joto la kadri katika nchi nyingi, wanaweza kuzaana kwa wingi katika mabwawa, hula majani na chakula kingine chochote kinachopatikana kwa urahisi shambani au nyumbani, hukua kwa haraka, uvumilia sana changamoto za bwawa hii ikiwa ni mabadiliko ya joto, hewa ya oksijeni, na pH, pia nyama ya samaki hawa ni tamu na yenye ladha nzuri.

2.3 Kuna aina nyingi za sato(tilapia) k**a vile Sato mwekundu, Sato wa Msumbiji, Sato mweupe na Sato wa Mwanza.
Sato hawa hula mimea na majani, huhitaji chakula kingi na huzaana sana, wana doa moja kubwa kwenye pezi la mgongoni. Sato hawa hula vijimea vya plankiton, hukua kwa haraka na wana mistari kwenye mikia. Aina nyingine za samaki zimechanganyikana na kuwa machotara hivyo siyo rahisi kuwatambua.

2.4 Sato wa Mwanza ni moja kati ya aina ya tilapia inayoshairiwa kufugwa na wataalamu wengi kwa kuzingatia sifa mbalimbali tofauti na aina nyingine.

3.0 ENEO LINALOFAA KWA UFUGAJI WA SAMAKI AINA YA SATO:
3.1.1 Upatikanaji wa maji
3.1.1 Maji ni moja ya hitaji muhimu katika ufugaji wa samaki. Eneo litafaa kwa ufugaji wa samaki ni lenye maji ya kutosha kuendesha shughuli zote za ufugaji kwa kipindi husika.

3.1.2 Chanzo cha maji kwenye bwawa kinaweza kuwa; mto, mfereji wa kumwagilia, au chemi chemi. Bwawa linahitaji maji mengi na sio rahisi kujazwa na ndoo. Ili kuhakikisha kuwa bwawa linakuwa na maji ya kutosha muda wote, chanzo cha maji cha faa kuwa cha kuaminika.

3.1.3 K**a mkulima ana maji ya kujaza kwenye bwawa kwa msimu, inawezekana pia kufuga samaki. Lakini mkulima ahakikishe anapanda vifaranga vya samaki mwanzo wa msimu wa maji. Hii itatoa fursa kwa samaki kukua hadi kufikia kiwango cha kuvunwa kabla ya maji kukauka.

3.1.4 K**a wakulima wanatumia chanzo kimoja cha maji ni muhimu kuanzisha utaratibu ambao utawezesha wakulima wote kutumia maji hayo bila matatizo. Wafugaji wa samaki wanaweza kujaza mabwawa wakati wowote kutegemea ni kipindi gani maji hayatumiki sana kwa matumizi mengine.

3.1.5 Ili kuhakikisha kwamba bwawa halitumii maji mengi, ni muhimu kuimarisha kingo za bwawa kwa kushindilia vizuri udongo wakati wa ujenzi wa msingi wa bwawa. Hii ina maana kwamba udongo lazima uwe na kiwango kikubwa cha mfinyanzi. Udongo ambao unatumika kutengenezea vyungu au kufyatulia matofali ni mzuri sana kwa shughuli hii. K**a udongo hauna ufinyanzi wa kutosha bwawa litapoteza maji kwa urahisi na italazimu kuongezwa kwa maji mara kwa mara.

3.2 Aina ya udongo
3.2.1 Inashauriwa kuwa udongo wa tifutifu au mchanganyiko wa tifutifu na mfinyanzi ambao una uwezo wa kuhifadhi maji kwa muda mrefu unafaa zaidi kwa ufugaji wa samaki.

3.2.2 Udongo wa kichanga sio mzuri katika kushikilia maji lakini eneo lenye udongo wa aina hii linaweza kutumika kufuga samaki ikiwa mbinu mbalimbali zitatumika.
Zingatia
· Kwa eneo lenye kichanga lakini lina upatikanaji wa maji ya kutosha mkulima anaweza kutumia mbinu ya kujaza mchanga kwenye mifuko ya saruji iliyokwisha kutumika na kuipanga kwenye kingo za bwawa ili kuimalisha kuta za bwawa. Kwakuwa mifuko inaweza kuoza kutokana na maji, inashauriwa ibadilishwe endapo kingo za bwawa zitaanza kumomonyoka na kuongeza tope ndani ya bwawa.
· Karatasi ngumu ya nailoni yaweza pia kutumika kuzuia kupotea kwa maji na kulinda kingo za bwawa kumomonyoka.
· Ujenzi wa kuta za bwawa kwa mawe au bwawa zima ni njia bora zaidi japo ni gharama ukilinganisha na mbinu nyingine.
Mifuko

3.3 Mambo mengine ya kuzingatia katika uchaguzi wa eneo la kufugia samaki

3.3.1 Eneo liwe na mteremko kiasi ili kusaidia shughuli nzima ya uingizaji na utoaji wa maji kwenye bwawa. Nguvu nyingi zitatumika kuchimba bwawa eneo lenye mwinuko mkali na ni vigumu kujaza au kutoa maji kwenye bwawa lililochimbwa eneo la tambarare

3.3.2 Eneo linatakiwa kuwa na miundombinu bora na lenye kufikika kwa urahisi ili kusaidia usafirishishaji wa mazao, vifaranga na mahitaji husika.

3.3.3 Eneo lisiwe na historia ya mafuriko, hii ni hatari kwa kuwa mafuliko yanaweza kuvunja kingo za bwawa hivyo kuhatarisha shughuli ya ufugaji.

3.3.4 Eneo lisiwe karibu na maeneo hatarishi k**a vile viwanda, shughuli za kilimo zenye kutumia kemikali ili kuzuia madhara ya kikemikali.

3.3.5 Eneo liwe karibu na mmiliki ili kuimalisha ulinzi na urahisishaji wa uendeshaji wa shughuli za uzalishaji.

7.0 VYANZO VYA MAJI KWA UFUGAJI WA SAMAKI;
7.1 Ni vyema mkulima kuchagua chanzo cha maji kinachofaa kulingana na mazingira yake pamoja na manufaa kwa mkulima.
7.2 Unaweza kutumia maji ya kisima, chemichemi, ziwa, mto na bomba kwa kuzingatia sheria na taratibu husika.
7.3 Matumizi ya maji ya bomba katika ufugaji samaki ni lazima uzingatie ushauri wa kitaalamu. Lakini mambo yafuatayo yanaweza kumsaidia mkulima kutumia maji ya bomba k**a chanzo cha maji; kabla ya kuweka samaki maji yawekwe kwenye bwawa kwa takribani siku kumi, hii itasaidia kuondoa chlorini kwenye maji, mbolea na tembe za vitamin c zaweza pia kutumika kuharakisha uondoaji wa chrolini katika maji.

7.4 Yote hapo juu yaweza kufanyika katika kuondoa chlorine kwenye maji lakini njia sahihi ni matumizi ya dawa maalumu aina ya ……………… inayopatikana madukani, japo ndani ya nchi yetu ni ngumu kuipata hivyo yaweza kuagiwa kutoka nje ya nchi.

8.0 GHARAMA ZA UCHIMBAJI WA BWAWA:
8.3 Gharama za uchimbaji zaweza kuainishwa katika makundi matatu; ushauri kutoka kwa wataalamu, gharama za uchimbaji na gharama za kuandaa bwawa kabla ya kuweka maji na wakati wa kuweka maji.

8.4 Gharama za uchimbaji wa bwawa zinatofautiana eneo kwa eneo na namna bwawa linavyochimbwa, hii ikihusisha nguvu na vifaa vitakavyotumika.

8.2 Ni vyema kuajiri watu kuchimba bwawa kuliko kutumia vifaa k**a excavator, k**a bwawa ni kubwa sana waweza kutumia vyote kwa pamoja. Bwawa linahitaji malekebisho mengi sana madogo madogo, hivyo matumizi ya watu k**a nguvu kazi katika kuyafanya hayo ni muhimu.

4.0 KUSAFISHA ENEO, UCHIMBAJI WA BWAWA
4.1 Mara eneo linapochaguliwa, ni muhimu kuondoa majani, vichaka na miti yote. Mizizi ing’olewe kabisa kwa kuwa itaoza na kuacha mashimo ambayo yatasababisha maji kuvuja.

5.5 Mara eneo likisafishwa, bwawa lichimbwe kwa vipimo sahihi ili kujua ukubwa wa bwawa. Hii itasaidia katika uchimbaji, kujua ukubwa wa bwawa na idadi ya vifaranga watakao pandikizwa. Ni vyema kutumia kamba ili kunyoosha ukuta wa bwawa wakati wa uchimbaji.

4.3 Matuta yajengwe kwenye eneo lililosafishwa vizuri na ambalo halina mimea wala mawe kwa ajili ya kuzuia kupotea kwa maji. Pia udongo wa juu ambao una majani na mizizi usitumike kwa kutengenezea matuta ya bwawa.

4.4 Matuta yasijegwe katika eneo la kichuguu kuzuia kupotea kwa maji, japo ni vigumu na mara nyingine haiwezekani kabisa kuzuia uvujaji wa maji kwa aina hii.

8.2 Ni muhimu kuhakikisha kwamba matuta yanajishikilia vizuri kwenye ardhi. Hii inaweza kufanyika kwa kuchimba mfereji kuzunguka bwawa katikati ya eneo ambalo matuta yatajengwa.

4.2 Matuta lazima yashindiliwe vizuri kuzuia maji yasivuje. Njia rahisi ni kushindilia matuta kila baada ya kuweka sentimeta 30 za udongo. Hakikisha udongo unaloweshwa na kushindiliwa kwa kutumia kifaa chenye ubapa chini au kipande cha mti. Ushindiliaji wa aina hii ni sawa sawa na ushindiliaji wa sakafu ya nyumba. Ushindiliaji unafanya matuta kuwa imara na kutuamisha maji

4.0 Upana wa tuta la bwawa inategemeana na ukubwa wa bwawa,ni vyema uwe na mita 3 chini na mita 2 juu, mteremko(slope) katika ukuta wa bwawa ni kitu cha muhimu, hii ni kupunguza mmomonyoko,na inamrahisishia mhusika kuingia ndani ya bwawa kwa urahisi.

6.0 Kina cha bwawa ni vyema kitofautiane, hii ikiwa ni futi 3-4 sehemu ya kina kirefu na futi 1-1.5 sehemu ya kina kifupi. Eneo la kati lichimbwe katika namna itakayowezesha kupata slope ya bwawa katika utofauti wa kina cha juu na chini.

10.1 Bwawa likiwa na kina kifupi, itakuwa rahisi kwa maadui a samaki kuk**ata samaki. Pia bwawa likiwa na kina kifupi litapata joto haraka wakati wa mchana na kupoa haraka wakati wa usiku. Kwa hali hiyo joto la maji litabadilika sana kitu ambacho ni hatari kwa samaki katika bwawa

10.2 Sababu nyingine ya kuwa na kina kinachostahili ni kwamba kwenye mabwawa yenye kina kifupi majani huota kwa kasi. Mimea kwenye bwawa la samaki ina athari sawa sawa na mimea shambani.

10.3 Wataalamu hawashauri kuchimba bwawa la kina kirefu kwa kuwa ni gharama, ngumu kulihudumia na kuvuna samaki…………

5.5 Urefu wa matuta utategemea wingi wa udongo, ukubwa wa bwawa na mfumo wa uvunaji wa samaki.

8.3 Ni muhimu pia bwawa lijengwe katika namna itakayoruhsu kujazwa na kukaushwa kwa maji kila inapohitajika. Hii ina maana kuwa maji yaingie bwawani sehemu iliyoinuka na yaweze kutolewa wakati wa kukausha kupitia sehemu ya chini ya bwawa.

5.4 Ili maji yafike sehemu ya bwawa iliyoinuka, mfereji wa kuchepushia maji kutoka kwenye
kijito utengenezwe.

5,3 Sehemu ya kuingiza maji iwekwe kwenye kina kifupi na ile ya kutolea maji iwekwe kwenye kina kirefu.mpaka kufika hapo naamini umenielewa juu ya UFUGAJI WA samaki.

wasiliana nasi kwa namba 0718405318

[06/17/19]   MADA:NJIA NZURI ZA KUONDOA MAGADI (SALTS) SHAMBANI

Utangulizi
Katika mashamba mengi tatizo la udongo na ardhi kwa ujumla kujaa chumvi au magadi limekuwa tatizo kubwa kwa wakulima wengi kwani magadi au chumvi huleta madhara makubwa sana kwa mazao na hata mazao mengine hufa kabisa pale
yanapooteshwa kwenye udongo wenye magadi mfano wa mashamba yalioadhirika ni Ndungu irrigation scheme, kitivo irrigation scheme, Dakawa, Kiroka na Mkindo irrigation scheme (Morogoro), Kinyasugwe scheme (Dodoma) pia baadhi ya maeneo ya Lower Moshi, Mawala, Kikavu chini, na hivyo kufanya mashamba yalio na tatizo hilo yasitumike katika uzalishaji, makala hii itakusaidia kumuelekeza mkulima kujua namna ya kurudisha ardhi ya shamba lako katika hali nzuri na kuzuia uwezekano wa magadi kuongezeka katika shamba lako na hii itaongeza uzalishaji kwani utaweza kuotesha mazao mengi na ya aina mbalimbali k**a udongo wako utakuwa na hali nzuri ya kuupatia mmea wako maji na madini au (nutrients) za kuuwezesha kukua vizuri na kuzaa sana

AINA ZA MAGADI ZILIZOPO KWENYE UDONGO

Kuna aina nyingi za chumvichumvi zilizopo ardhini na huwa katika viwango tofauti kulingana eneo moja na lingine na tofauti hii husababishwa na asili ya udongo wa mahali husika chumvi hizi ni k**a Sodium ambayo hupatikana kwenye chumvi ya kawaida(NaCl), Potasium, Boron, Magnesium, Calcium, Phosphorous. Madini mengine ni muhimu katika ukuaji wa mmea lakini kwa kiwango kinachotakiwa na huwa ni sumu endapo yatazidi kiwango chake

NAMNA AMBAVYO MAGADI HUDHOOFISHA MIMEA

Madhara yatokanayo na magadi ni makubwa sana na huleta hasara kwa wakulima wengi sana, kitaalamu magadi huzuia mizizi ya mimea kufyonza maji kwenye udongo na kuufanya mmea kushindwa kukua kwani maji ni muhimu katika mfumo wa mimea kujitengenezea chakula chake hata k**a utamwagilia maji ya kutosha katika shamba lenye magadi bado mimea haitaweza kupata maji hayo (salts induce water stress to crops through matrix forces build up between the soil particles and the salts ion and hinder plant water uptake via capillarity and osmosis).

Pia magadi huharibu mfumo wa udongo(soil structure) na kuufanya udongo kuwa mgumu na kuzuia mizizi ya mmea kupenya vizuri kwenye ardhi na hivyo kupunguza udhabiti wa mimea iwapo shambani na kusababisha kuanguka angauka kwa mazao yanapofikia wakati wa kubeba matunda au maua kwani hukosa nguvu za kujishikilia kwenye ardhi na hali hii husababishwa sana uwepo na sodium nyingi shambani na mkulima hupata hasara kubwa sana.

VYANZO VYA MAGADI KWENYE UDONGO

1.Asili ya udongo wenyewe

Baadhi ya maeneo yana udongo wenye asili ya chumvi kwa Tanzania maeneo hayo yanapatikana kwa wingi Dodoma na Singida na hasa wakati wa kiangazi baada ya mvua kukatika unaweza ukaona kabsa mabonge ya chumvi ardhini

2. Maji yanatumika kwa umwagiliaji

Kuna baadhi ya maeneo maji yake huwa na chumvi kiasi kwenye mito na hapa chemichemi na wakulima hutumia maji kutoka kwenye vyanzo hivyo vyenye maji ya chumvi katika kumwagilia mashammba yao, hii huongeza chumvi kidogo kidogo kwenye ardhi na k**a mwendelezo wa kutumia maji hayo utafanyika kwa miaka mitano basi shamba hilo litakuwa limejaa chumvi na halitafaa tena kwa kilimo endapo njia na mbinu stahiki hazitachukuliwa. Mfano skimu ya Mazinde pamoja na Mombo.

3. Utumiaji wa mbolea za viwandani bila maelekezo ya kitaalamu

Tujue ya kuwa sio kila mbolea ya kiwandani inafaa kwenye kila aina ya udongo, pili tunapokuwa tunaweka mbolea shambani lazima tuwatumie wataalamu ili watupe vipimo sahihi vya uwekaji wa mbolea hizi ili ziwe kwa kiwango kinachotakiwa pasipo kuzidisha wala kupunguza , kila shamba lina rutuba tofauti na lingine kwa hiyo ata uwekaji wa mbolea utatofautiana.
Pia kila zao lila vipimo vyake vya kiasi cha mbolea kinachotakiwa, kumbuka ni muhimu kufuata ushauri wa wataalamu kabla ya kuweka mbolea shambani ili kuondokana na matatizo na uweze kuzalisha mazao yenye tija ndio maana mfano, wataalamu kutoka TARI Mlingano wanashauri upime udongo kwanza kabla hujaanza kulima

4. Mfumo mbaya wa utoaji maji shambani(poor drainage system)

Tatizo hili ni kubwa sana hasa pale wakulima wengi wanapoamini kuwa katika kumwagilia shamba lazima aone maji yametuama ndio aridhike kuwa amemwagilia, hili ni kosa kubwa kwani tunatakiwa tujue kuwa mimea hufyonza maji yaliyo ardhini tuu(plants absorb water, and they don't drink water ......... Myth), maji yaliyotuama shambani hupandisha chumvi iliyopo chini kuja juu na baada ya ardhi kukauka chumvi ile hubakia juu ya ardhi na kuathiri mimea

NJIA ZA KUONDOA MAGADI SHAMBANI

Hili ndilo lengo kuu la makala hii ili kumsaidia mkulima kuondokana na tatizo hili, nitaeleza njia za kitaalumu na za gharama nafuu za kuondoa na kupunguza magadi shambani.

1. Kuzamisha chumvi (Leaching of salts)

Wakati wa kumwagilia shamba unashauriwa umwagilie maji mengi kiasi kuliko yale yanayotosheleza mmea wako ili maji hayo ya ziada yasaidia katika kuzamisha chumvi iliyoko juu wa udongo iende chini zaidi ambako mizizi ya mimea haifiki, njia hii lazima utumie wataalamu wa umwagiliaji (irrigation engineers) ambao watasaidia kitaalamu kuendena na udongo wako na kujulisha ni kiasi gani cha maji inatakiwa umwagilie katika shamba lako ili kuondoa chumvi na kusaidia mimea yako kukua (irrigation and leaching requirements)

2. Uwekaji wa Gypsum (Calcium Sulfate)

Gypsum hufanya kitu kinachoitwa neutralization ambapo hubadilisha chumvi iliyopo ardhini isilete madhara kwa mimea na katika maduka mengi ya pembejeo zinauzwa hizi gypsum kwa ajili ya mashamba ili kudhibiti chumvi na magadi lakini njia hii ni ya gharama kidogo

3. Utumiaji wa Samadi

Mbolea za wanyama na mimea husaidia sana kwenye kuongeza rutuba kwenye ardhi pia katika kuhakikisha na kupungiuza magadi kwenye udongo na njia hii matokeo yake ni polepole lakini ina uhakika na pia samadi ina faida nyingine nyingi katika kuimarisha udongo na kuongeza upatikanaji wa madini kwa mimea

4. Njia ya mafuriko (flooding)

Njia hii hufanywa katika maeneo yenye maji mengi na hasa kipindi cha mvua , shamba lenye magadi hutifuliwa na kufurishwa au kumwagiliwa mpka maji yanatuama (wakati hamna mazao shambani) na baada ya hapo maji hutolewa kwa mifereji maalumu na maji hayo huchukua magadi katika shamba husika

NB. njia hii usiifanye kwenye mashamba yaliosongamana ili maji yaliyo na magadi yasiende kwenye shamba la jirani yako na kumpa hasara

5. Utumiaji wa njia za kisasa za kufanya umwagiliaji k**a drip irrigation, sprinkler system hupunguza uwepo wa magadi kwenye udongo.
Lakini kwa maeneo ambayo yana magadi sana unashauriwa kupanda mazao yanayoshahimili ardhi yenye chumvi

mazao yanayoshahimili chumvi zabibu, mbaazi, Nanasi, Miembe hasa mazao ya miti ndio hushauriwa sana katika ardhi yenye magadi

mazao yasiostahimili udongo wenye magadi

Mahindi, Tikiti maji, Nyanya, Mbogamboga, na mengne mengi.

Location

Category

Telephone

Address


[email protected]
Tanga
BOX 483 KOROGWE

Opening Hours

Monday 08:00 - 18:00
Tuesday 08:00 - 18:00
Wednesday 08:00 - 18:00
Thursday 08:00 - 18:00
Friday 08:00 - 18:00
Saturday 09:00 - 18:00
Sunday 09:00 - 18:00
Other Education in Tanga (show all)
IJUE DINI YA Kiislam IJUE DINI YA Kiislam
Tanga, 53

IJUE DINI YA KIISLAM

Ronagi Health Informtion center Ronagi Health Informtion center
Tanga, 255

Ronagi health information centre is one among which covers different services 'It is located at Tanga.

The pain master's The pain master's
Makorora Tanga
Tanga

The Best Indicies Forex Brokers The Best Indicies Forex Brokers
Tanga
Tanga, 434

https://track.deriv.com/_HJ4paoojYYW2vdm9PpHVCmNd7ZgqdRLk/1/

Chumbageni Primary School Chumbageni Primary School
Tanga

Chumbageni Primary School is in Tanga, Tanzania. Over 1000 children ages 4 to 13 are enrolled, taught by a staff of 27.

Empower the Community and Environmental Conservation Organization Empower the Community and Environmental Conservation Organization
80502
Tanga, 255

E.C.E.C.O is Non – Governmental organization established in 2011 and get full registration in 2014 with registration number 00007207.

David Togolani Mashambo David Togolani Mashambo
P.O BOX 5395 SAHARE
Tanga, +255719992280

sharing social,economic and religious experience

Academic revolution Academic revolution
Chanika- Handeni
Tanga

Galanosi boys high school Galanosi boys high school
Tanga

Our school located at nguvumal street 5km from tanga bus terminal.