David Togolani Mashambo

David Togolani Mashambo

Share

sharing social,economic and religious experience

02/08/2014

Hapo zamani za kale waafrika waliuzwa k**a watumwa kwa ajili ya kwenda kufanya kazi ngumu za uzalishaji.Hali hiyo ya utumwa iliwafanya kukosa uhuru wao wa kuishi na kufanya k**a walivyopenda.Kutokana na ubaya wa utumwa watu wengi waliishi maisha ya kujificha ili wasije kwa bahati mbaya wakaangukia katika balaa hilo la utumwa.Hata hivyo walishindwa kujilinda kutokana na usaliti uliyosababishwa na viongozi wao waliokuwa na ubinafsi na tamaa ya mali.

Leo hatuna utumwa wa namna ile ya zamani lakini utumwa mwingine mbaya zaidi umeibuka kiasi cha binadamu aliyeumbwa kwa sura ya Mungu kuishi na kufanya mambo ya ajabu ambayo si kwamba yanatisha tu bali yanaashiria kuwa binadamu ni kiumbe kilichokosa mwelekeo wa asili.Machafu yanayotendeka k**a ndoa za jinsia moja,mauaji n.k ni ushahidi tosha kuwa hukumu za Mungu haziko mbali kuachiliwa katika ulimwengu huu uliyochanganyikiwa.

Hebu keti chini na utafakari sura ya ulimwengu wa leo.Hakika unaweza kuzisoma ishara kuu za kufungwa kwa historia ya ulimwengu huu.

WEKA MAISHA YAKO MIKONONI MWAKE MUNGU NA KUANZA UPYA SAFARI YA MATUMAINI YA UZIMA WA MILELE NAWE UTABARIKIWA SANA.

MUNGU AKUBARIKI.

01/08/2014

Wakati mwingine maisha yanaonekana kukosa thamani pale unapotambua kuwa jamii iliyo karibu yako haikujali wala kukuthamini.Hali hii imepelekea wengi kuchukua hata maamuzi yasiyo sahihi na wala yasiyo na ulazima wowote wa kukatisha umri wao kabla ya wakati wake.

Habari njema ni kwamba hukuja katika dunia hii kwa bahati mbaya.Yuko Mungu aliyeruhusu kuzaliwa kwako ili aweze kutimiza makusudi yake kwa ajili ya utukufu wake.Wewe ni wa thamani kubwa mbele za Mungu mwenye mamlaka dhidi ya kila tatizo linalokukabili katika maisha yako.

Mpe maisha yako leo kwani yeye ni rafiki wa kweli anayeweza kukupa matumaini,nguvu,afya na hatimaye uzima wa milele ambao ndiyo tumaini letu kubwa hasa katika nyakati hizi za miisho ya ulimwengu huu wenye dhambi.

Bwana akutie nguvu za kusonga mbele huku ukimtegemea yeye aliye wokovu wetu.AMEN

28/07/2014

Mwanadamu ameumbwa katika sura mbili za maisha ambazo ni maisha ya kujumuika k**a sehemu ya ulimwengu usiyo na Mungu na sura nyingine ni mwenendo wake unaoonyesha matarajio na tumaini kwa uwezo mkubwa usiyoonekana kwa macho ya ulimwengu.Hali hii ndiyo imfanyayo mtu kutofautishwa na mnyama.Na endapo mwanadamu ataonyesha sura moja tu ya ulimwengu,bila shaka atakufa bila tumaini la uzima wa milele.

Want your school to be the top-listed School/college in Tanga?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Website

Address


P. O BOX 5395 SAHARE
Tanga