30/09/2023
*ELIMU YA MIKOPO BENKI* USIPUUZE HII
*ELIMU YA MIKOPO BENKI*
Kumekuwa na malalamiko na vilio kwa baadhi ya watumishi kuhusu mikopo wanayopewa na benki.
Wengi wao wanalaumu mikopo hiyo kuwa ni kandamizi kwao badala ya kuwapa unafuu imegekuka kuwakandamiza na kuyafanya maisha yao kuwa magumu.
Hapa tatizo sio mikopo inayotolewa na benki bali shida ipo kwenye elimu juu ya namna bora ya kukopa.
Kwa kukosa elimu hiyo, mtumishi wa umma unapokwenda kukopa benki afisa mikopo atakupa chaguo (option) ambalo litakuwa na faida zaidi kwa benki.
Mfano,
Mtumishi mwenye mshahara wa
Tsh.700,000/=baada ya makato
(take home)
Kwa mtumishi asiyekuwa na elimu ya mikopo, akifika benki atamuuliza afisa mikopo kwa mshahara wa laki 7 naweza kukopa kiasi gani??
Hapa afisa mikopo atakachoangalia kwanza ni chaguo lipi litaingizia benki faida kubwa zaidi!
Atapiga mahesabu, kuzingatia sheria ya 1/3 ya mshahara ibaki kwa mtumishi , atapata 2/3 ya 700,000/= ni k**a 466,666.67 hivi.
Sasa chukulia hapo muda wa chini uwe miaka mitano.
Atakwambia una uwezo wa kukopa hadi 19M, makatao yote itakuwa sawa na Tsh. 443,000 kwa mwezi.
Mtumishi asiyekuwa na elimu ya mikopo akiangalia mshahara wake anajikuta inabakisha 270,000.
Anamuuliza afisa mikopo nikichukuwa hiyo 19M kwa miaka nane je?
Anaambiwa ukichukuwa hiyo 19M kwa miaka nane kila mwezi utakatwa 325,000 na utabakiwa na 375,000/= kila mwezi.
Mtumishi asiye na elimu hii anakubali kuchukuwa 19M kwa miaka nane kwa sababu tu makato ni madogo.
*USICHOKIJUA SASA*
1. Ukichukuwa mkopo wa 19M kwa miaka
mitano marejesho yako ya Tsh 443,000/=
kila mwezi kwa miaka 5 ni sawa na
Tsh. 443,000×12×5= 26,580,000/= na hivyo
mkopo huo utakuwa umeipatia benki faida
ya Tsh 7,580,000.
2 Ukichukuwa kwa 19m kwa miaka nane kwa
marejesho ya Tsh. 325,000/= kila mwezi
utakuwa na jumla ya marejesho
Tsh. 325,000 ×12×8= Tsh.31,200,000/=
hivyo utaipatia benki faida ya 12,200,000.