Empower the Community and Environmental Conservation Organization

Empower the Community and Environmental Conservation Organization

E.C.E.C.O is Non – Governmental organization established in 2011 and get full registration in 2014 with registration number 00007207. 1: ORGANIZATION PROFILE
E.C.E.C.O is non-government and non - profit organization dedicated to transform Tanzanians’ communities from chronic poverty to hopeful standard of life.

Operating as usual

26/04/2017

[4/23, 09:55] Ndosho: JINSI YAKUJITOA KWENYE UTUMIZI WA SIGARA NA DAWA ZA KULEVYA
Iwe ni mvutaji mchanga au mbutaji mahiri au mtumiaji mchanga au mtumiaji mzoefu, kutoka katika utumiaji huo kunaweza kuwa kugumu lakini jinsi utakavyo kuwa unajifunza njia mbalimbali za kuacha, ndio urahisi utakavyo patikana. Ukiwa na nia na mipango madhubuti unaweza kuvunja minyororo ya matumizi ya dawa za kulevya, kuweza kuhimili kiu ya matumizi na kuungana na mamilioni ya watu walio amua kuachana na matumizi hayo kwa manufaa yao.
KWANINI KUACHA UTUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA KUNAONEKANA KUGUMU.
Matumizi ya dawa za kulevya haiathiri maumbile ya mwanadamu tu bali huathiri mwenendo wa akili pia. Chemikali zilizopo kwenye dawa za kulevya humfanya mtu kujihisi yupo vizuri sana. Kutokana na kemikali kukufanya ujisikie vizuri kunakoakisiwa na ubongo, hali hiyo inakufanya uwe mtumiaji wa dawa za kulevya ili kuondokana na msongo wa mawazo, upweke na kuzubaa.
Muda huohuo kitendo cha utumiaji wa dawa hizo huchukuliwa k**a ni kitendo cha kawaida chakila siku ambacho huwezi kukiacha, k**a vile kuvuta sigara asubuhi baada ya kifungua kinywa, unapoenda mapumziko kazini au shuleni au unapokuwa nyumbani baada ya muda wa kazi au masomo.Ili kufanikiwa kujitoa katika utumiaji, unatakiwa kujiepusha na tabia za utumiaji na mienendo inayokuweka karibu na utumizi na watumizi wa dawa za kulevya.
[4/23, 09:59] Ndosho: MPANGO BINAFSI WAKUACHA UTUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA.
Wakati baadhi ya watumiaji wamefanikiwa kujitoa katika utumiaji, watu wengi wanaendelea na jitihada katika kujitoa na utumiaji kwa kuwa na mipango yao wenyewe. Mpango mzuri wakuacha utumiaji wa dawa za kulevya hujumuisha changamoto za muda mfupi na muda mrefu katika uachaji huo. Uachaji unatakiwa uambatane na mahitaji yako muhimu na maalumu ya tabia za utumiaji wa dawa za kulevya.
MASWALI YAKUJIULIZA WEWE BINAFSI!
Chukua muda kujiuliza wewe ni mtumiaji wa namna gani? Ni kwa kipindi gani utahitaji kuvuta au kutumia dawa za kulevya? Na kwanini?. Hii itakusaidia kuweza kupata njia rahisi ya kuacha utumiaji katika njia iliyo salama.
Je wewe ni mvutaji mzoefu? Ni kiasi gani unaweza kuvuta kwa siku?
Je ? Unatumia dawa za kulevya unapokuwa na mawazo au unapokuwa unahisi unyonge?
Je? Kuna shughuli sehemu au watu unaoshirikiana nao katika utumiaji?
Je? Wewe ni mtu ambaye upo wazi kuongea na wataalamu na washauri juu ya utumizi wako wa dawa zakulevya?
Je? Upo tayari kuingia katika mpango maalumu wa kuacha dawa za kulevya?
[4/23, 10:02] Ndosho: ANDAA MPANGO WA KUACHA DAWA ZA KULEVYA (JITAKASE)
Jipangie tarehe ya kuacha utumiaji.
Ndani ya wiki mbili baada ya kupata mafunzo haya, utakuwa ni muda mzuri wa kujiandaa na zoezi la kuacha matumizi ya dawa za kulevya bila ya kupoteza azma yako ya kuacha. K**a unavuta siku za kazi, acha kuvuta, hivyo utakuwa na muda muafaka wakufanya mabadiliko ya kuacha siku zinavyoendelea.
Taarifu familia, marafiki na wafanyakazi wenzako juu ya mpango wa kuacha
Wajulishe marafiki na familia yako kuwa una mpango wa kuacha matumizi ya dawa za kulevya na waeleze kuwa unahitaji msaada wao na kukutia moyo katika uachaji huo. Tafuta mkaribu wako anayetaka kuacha k**a wewe nanaweza kusaidiana katika hali hiyo ya uachaji.
Kabiliana na changamoto utakazo kutana nazo kipindi cha uachaji.
Watu wengi wanao amua kurudia utumiaji wa dawa zakulevya, mara nyingi hufanya hivyo ndani ya miezi 3 tangu waanze zoezi la uachaji wa matumizi ya dawa zakulevya. Unahitajika kupambana na hali ya kutamani kutumia dawa za kulevya kikamilifu bila kukata tamaa. Unashauriwa kuonana na wataalamu wa maswala ya saikolojia na afya ili upate ushauri wa vyakula vyakutia nguvu na kujenga mwili.
Safisha nyumba/ chumba chako, gari au mahala pa kazi.
Ondoa vitu vinavyo husiana na uvutaji k**a vile vikopo vya majivu (ash trays), viberiti na safisha nguo zako kuondoa harufu ya sigara, bangi/ dawa za kulevya.
Endelea kuongea na wataalamu mbalimbali katika kukusaidia njia bora zakuacha utumiaji wa dawa za kulevya na kupambana na changamoto za uachaji wa dawa za kulevya ipasavyo. JITAKASE - USIKATE TAMAA

11/04/2017

Empower the Community and Environmental Conservation Organization's cover photo

[02/01/17]   Drug Abuse Resistance Education Program

KARIBU TUSHIRIKIANE KATIKA PROGRAM YAKUTOA ELIMU DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA

13 - 18 FEBRUARY 2017.

Hii ni wiki yakukumbushana juu ya athari za dawa za kulevya kwa vijana na wazee. Kwa kushirikiana na asasi ya Foundation for Drug Free World ya nchini Marekani, tunakusudia kutoa ukumbusho juu ya athari za dawa za kulevya Tanzania. Mradi huu unakusidiwa kufikia Mikoa miwili, Dar es Salaam na Tanga.

Utafiti uliofanywa na tume yakudhibiti dawa za kulevya Tanzania kuanzia 2011 - 2013 unaonyesha kuwa aslimia 5 - 12 ya vijana/wanafunzi wanatumia dawa za kulevya, hii inaweza kuchangia pia uzoroteshaji wa elimu katika mikoa yenye viwango vikubwa vya matumizi ya dawa za kulevya k**a vile Dar es Salaam na Tanga.

Inakadiriwa kuwa watu 500,000 - 600,000 wanatumia dawa za kulevya nchini Tanzania hali inayopelekea kuongezeka kwa umasikini wa kipato na afya mbovu kwa vijana wengi.

Ni jukumu na kila mmoja kuchukua nafasi hii kuwakumbusha ndugu, jamaa na marafiki jui ya athari za dawa za kulevya.

Wanaotaka kushiriki nasi tunawakaribisha sana. Vikundi k**a vya jogging na vikundi vingine vinakaribishwa sana kushiriki nasi

29/11/2016

VIJANA NA UTUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA.

Tafiti nyingi zinaomyesha kwamba, vijana wengi wameanza kutumia dawa za kulevya wakiwa na umri mdogo, na wengi wakiwa mashuleni au mitaani.

Zoezi la kuanza utumiaji qa dawa za kulevya au vileo k**a vile bangi, co***ne na pombe, huanza k**a masikhara au utani tu tena wakati mwingine bila kutumia nguvu kubwa ya ushawishi. Kwakule kuwa mnasoma pamoja, mnakula pamoja na matembezi yenu mnaluwa pamoja inakuwa sababu ya kushawishi au kushawishika kuingia katika utumiaji wa dawa za kulevya.

Kitu ambacho vijana wengi wanaotumia dawa za kulevya wanakiogopa ni picha yao katika jamii itaonekana vipi, hili hujitokeza hasa kwa wale wanaoanza kutumia, hali hii hupelekea kuwa na usiri mkubwa sana na huchukuwa muda kujua kuwa sasa nduguyo au mwanao anatumia labda kutokana na mabadiliko ya kimwili, kiafya na kimienendo.

Ni mara chache sana kuona vinaja hawa wanafikiria afya zao, wao qanafikiria hivi hapa baba akiniona itakuwaje?, askari akinik**ata itakuwaje?, mwalimu akijua hii soo itakuwa hapakaliki kabisa, hawadikirii hivi nikipata kqnsa ya koo itakuwaje, nikipata homa ya manjano itakuwaje, matatizo ya ini na vvu maisha yangu yatakiwaje? Ni upi mustakbali wa maisha yangu ya sasa na baadae?

Hivyo tunalojukumu kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa tuwatoa elimu kwa ndugu zetu, jamaa na rafiki zetu, majirani zetu na kwa kila mmoja kwa nafasi yake juu ya athari za utumiaji wa dawa za kulevya.

Ni ELIMU ndio itakayo wakomboa vijana wenzetu... Jitakase Anza Sasa

09/09/2016

Empower the Community and Environmental Conservation Organization

http://www.drugfreeworld.org/newsletter/2016-05-truth-about-drugs-tanzania.html?utm_campaign=df

Share it with others

09/09/2016

Bringing The Truth About Drugs to Tanzania’s Youth

http://www.drugfreeworld.org/newsletter/2016-05-truth-about-drugs-tanzania.html?utm_campaign=df

Share it with others

drugfreeworld.org How one man who suffered the deep personal loss of a close family member at the hands of drug abuse is waking up the youth of his nation to the truth so they can halt the problem.

06/09/2016

Empower the Community and Environmental Conservation Organization

Demand Reduction or Supply Reduction - or Both?

Katika vita ya kupambana na dawa za kulevya kuna njia maarufu mbili zinazotumiwa na watu mbalimbali pamoja na taasisi mbalimbali za serikali na zisizo zakiserikali, njia hizo huitwa Kupunguza Uhitaji (Demand Reduction) na Kupunguza Upatikanaji/Usambazaji (Supply Reduction).

KUPUNGUZA UHITAJI (DEMAND REDUCTION)
Njia hii mara nyingi hututmiwa na vyombo visivyo na mamlaka yakuk**ata na kufikisha mahak**ani washukiwa wa usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya. Njia kuu inayotumika katika kupunguza uhitaji wa dawa za kulevya ni ushawishi kwa watumiaji na wasiotumia dawa za kulevya kuacha au kutotumia dawa hizo.

Elimu hutolewa mara nyingi katika njia za kupunguza uhitaji wa utumiaji wa dawa za kulevya. Hapa watu wanakuwa na nafasi yakubadilisha tabia zao pamoja na mienendo yao ili kuona kua hakuna umuhimu wa kutumia dawa za kulevya na athari zake ni kubwa sana kwa afya za watumiaji, kwa familia zao pamoja na na mustakbali wa Taifa.
Kwa hapa kwetu Tanzania ni vijana wengi sana wametumbukia katika matumizi ya dawa za kulevya bila kujua na kutambua kwanini wameingia katika hali hiyo, wengine wamekuwa wakidhani kuwa wanaweza kupunguza au kutatua kabisa amatatizo mbalimbali yanayowakabili kwa kutumia dawa za kulevya na kinyume chake wanaongeza matatizo badala yakuyapunguza.

Njia hii ya kupunguza uhitaji na tamaa ya kutumia dawa za kulevya ndio njia ambayo hivi karibuni imekuwa ikitegemewa sana na nchi nyingi duniani, hasa zilizoendelea kwa kuanzisha programu mbalimbali za kutoa elimu kwa vijana wao mashuleni, kwenye nyumba za ibada na kupitia mitandao ya kijamii pamoja na shughuli zinazowashirikisha wazazi na walezi ili kuweza kuhakikisha kua makuzi ya watoto na vijana wao yanadhibitiwa ili wasijiingize kwenye dawa za kulevya kwa kufahamu madhara yake na si kuwasubiri waingie na kuwak**ata kwa vyombo vya dola.

KUPUNGUZA UPATIKANAJI/USAMBAZAJI (SUPPLY REDUCTION)
Njia hii mara nyingi inatumiwa na vyombo vya dola na usalama katika kudhibiti upatikanaji wa dawa za kulevya kutoka katika maeneo mbalimbali ya dunia.

Hapa kwetu Tanzania, TUME YA KUDHIBITI DAWA ZA KULEVYA pamoja na KITENGO CHAKUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA CHINI YA POLISI ni baadhi ya vyombo vilivyo vilivyoanzishwa kupambana na dawa za kulevya nchini. Mara nyingi tumesikia washtumiwa wa kuasafirishwa dawa za kulevya wamek**atwa na kufikishwa mahak**ani lakini mwisho wa kesi zao umekuwa na changamoto kubwa kutokana na sababu mbalimbali.

Katika njia hii kuna changamoto kubwa zakimtandao wa wauzaji na wasambazaji wa dawa hizo kuwa ni watu wenyefedha nyingi hivyo kuweza kuwarubuni kiurahisi maafisa, changamoto za bajeti ya kuwekeza katika mafunzo na vitendea kazi pamoja na changamoto zakimazingira kwani kudhibiti uingizwaji wa dawa za kulevya unahitaji ushirikiano wa karibu na nchi jirani kuhakikisha kuwa hakuna mwanya wakupitisha dawa za kulevya.

USHAURI:
Ili kuhakikisha kuwa vita hii inapata matunda mazuri hakuna budi kuhakikisha kuwa njia zote mbili, yaani DEMAND REDUCTION na SUPPLY REDUCTION zinapewa mkazo sawa katika kuhakikisha tunadhibiti upatikanaji na tunabadilisha mitazamo ya jamii yetu juu ya matumizi ya dawa za kulevya.

Ni wakati sasa serikali na watu mbalimbali kuziunga mkono asasi zinazotoa elimu kwa vijana wetu ili ziwafikie vijana wengi zaidi na kuhakikisha kuwa kunakuwa na program endelevu zakuwakumbusha vijana wajibu wao kwa jamii na taifa lao.

KILA MMOJA ANAWAJIBU WAKUHAKIKISHA KUWA ANAJITAHIDI KATIKA KUHAKIKISHA WATU WANAOKUZUNGUKA WANAELEWA MADHARA YA DAWA ZA KULEVYA!

WATUMIE NA WENGINE UJUMBE HUU!!!

01/09/2016

Mbande Secondary School, DSM

wanafunzi wa Mbande Sekondari wakitoa ya moyoni kuhusu dawa za kulevya, wengine wanaamini kuwa matumizi ya bangi yanaweza kuhalalishwa hapa kwetu kwani huko ULAYA bangi inauzwa kwenye maduka,

[09/01/16]   KAMPENI YA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA MASHULENI,

Ni dhahiri kuwa ndugu zetu wanataabika sana na matumizi ya dawa za kulevya, hasa wanafunzi, wengi wanadanganyika na kuingia katika matumizi ya dawa za kulevya bila kutarajia. Wanazitesa familia zao na kutaabisha ndugu zao.

Tushik**ane kukiokoa kizazi hiki kwa pamoja, share na mwingine!!

26/06/2016

Empower the Community and Environmental Conservation Organization

JE? UNASHIRIKIJE KATIKA VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA???

26 June Kila mwaka ni siku ya dawa za kulevya duniani. Ni vijana wengi sana wameathirika na dawa za kulevya hasa katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. Inakadiriwa kuwa ni vijana takirbani laki 5 (500,000) wamejiingiza katika utumizi wa dawa za kulevya Tanzania. Na kila siku wapo vijana wanaoingia katika utumiaji wa dawa za kulevya iwe bangi, co**in, he**in hata ulevi. Athari za utumiaji wa dawa za kulevya bila shaka zimeigusa kila familia kwa sasa, k**a sio mdogo wako atakuwa kaka yako, dada yako, mjomba shangazi, binamu au hata rafiki wa karibu anatumia dawa za kulevya. Hivyo basi yatupasa kila mmoja wetu kuchukua juhudi zakuelimisha kila aliyekaribu nae kuhusu athari za dawa za kulevya katika jamii yetu na mustakbali wa taifa letu kwa ujumla.

Katika kutumia dawa za kulevya tunaweza kuwagawa watu katika makundi manne (4)
1. Addicted: hawa ni watu ambao wametumia dawa za kulevya kwa kiasi kikubwa na kwa muda mrefu hali iliyopelekea maisha yao na uhai wao kutegemea matumizi ya dawa za kulevya kila siku. Watu wa namna hii hawamudu hata kunyanyua mguu au hata kope za macho yao wanapokosa dawa hizo, ili damu yake ianze kazi na mwili upate nguvu atalazimika kutumia dawa za kulevya japo kwa kiasi kidogo. Ikifikia hali hi ni hasara kubwa kwa jamii na taifa kwani, watu wa namna hii watafanya kila njia watakayoweza ili wapate pesa za kununulia dawa hizo.

Mtu anapofikia hatua hiyo hawezi kuacha dawa za kulevya kwa kutaka kwake mwenyewe tu bali kwa matibabu maalumu na kuwa chini ya uangalizi mkubwa sana. Tunao ndugu zetu na amaa zetu waliofikia kiwango hiki cha utumiaji wa dawa za kulevya, ni jukumu letu kuhakikisha kuwa tunawasaidia kuokoa maisha yao kwani tukiwaachia wao wenyewe tutawakosa kabisa.

2. Ambao hawajaathirika sana (Normal users) Hawa ni watumiaji wa dawa za kulevya wa kawaida. Mtu wa namna hii hajaathirika sana na dawa za kulevya kiasi chakumfanya ashndwe kufanya shughuli zake. Ni mtu ambaye dawaza kulevya hazija muathiri sana. Mtu wa namna hii ni rahisi kuacha bila ya athari kubwa za kiafya au kwa matibabu madogo na anarudi katika hali yake ya kawaida muda mfupi sana.

Takwimu zinaonyesha kuwa vijana wengi wapo katika kundi hili na wanakaribia kuhama kwenda kundi la kwanza endapo juhudi za makusudi za kuwaokoa vijana hawa hazitachukulia. Tujitahidi kuhakikisha kuwa ndugu zetu hawa tunawanasihi bila kuchoka ili waache utumiaji wa dawa za kulevya kwani hauna faida kwao wala kwa familia zao, kwa jamii na kwa taifa kwa ujumla.

3. Walio njia panda - wanaoshawishiwa kutumia au hata walio onja. Hili ni kundi la vijana au watu ambao hawajafikia uamuzi wa kutumia dawa za kulevya lakini wapo katika msukumo mkubwa sana kutoka kwa marafiki na watu wa karibu wanaotumia dawa za kulevya, kuwataka watumie tu kwani hazina athari yoyote na ndio ujana bwana.

Kwa haraka haraka watu hawa wanakuwa katika mawazo makubwa na hawajui lakufanya, waingie katika utumiaji wa dawa za kulevya au wasitumie. Endapo tutawaacha hawa ile nguvu ya wanawashawishi ikiwa kubwa, hawa wataangukia katika matumizi ya dawa za kulevya k**a wengnine walivyoingia huko. Hatuna budi kuwashawishi na kuwaonyesha mifano ya dhahiri ya waliotumia dawa hizo na kuangamiza maisha yao na hawakupata chochote.

Elimu ndio nguzo pekee itakayowaokoa watu hawa na ndugu zetu hawa wasiingie katika kundi la watumiaji wa dawa za kulevya. Je UPO TAYARI KUWASIAIDIA NDUGU ZAKO KWA KUWAFIKISHIA ELIMU HII??? NI JUKUMU LAKO ....... ANZA SASA.

4.Wasiotumia kabisa. wapo vijana wengi sana ambao katika maisha yao hawafikirii kabisa kutumia dawa za kulevya pengine kwa kujua athari zake kwao na kwa maisha yao au kwa kuwa hawapebdi tu kujiingiza katika mambo hayo. Hili kundi lazima lilindwe kwa nguvu zote, wasifikirie kabisa na uwamuzi wao ndio uamuzi sahihi unaotakiwa kuigwa na kila mtu. Tywapongeze kwa uamuzi wao na tuwaombe basi wawasiaidie vijana wenzao waliokwisha mezwa na dudu hili waachane na matumizi ya dawa za kulevya.... hakuna mwishp mwema kwa mtumiaji.

DRUG ABUSE RESISITANCE EDUCATION EVENTS 11th - 17th July 2016- DAR ES SALAAAM.
Empower the Community and Environmental Conservation Organization kwa kushirikiana na Foundation for Drug Free World kutoka Marekani inakusudia kufanya mradi/events za kutoa eleimu juu ya athari ya dawa za kulevya Tanzania kwa kuanzia na Dar es Salaam. Elimu hii itapelekwa kwa baadhi ya shule za sekondari, kufanya mikutano na semina na vijana katika halmashauri za Ilala, Temeke na Kinondoni, pamoja na kukutana viongozi wa serikali na mashirika mbalimbali. Itatengenezwa DOCUMENTARY itakayotumika nchi mablimbali duniani.

Kwa yoyote aliyetayari kuchangia chochote katika kufanikisha events hii anakaribishwa, wadhamini wanakaribishwa ili kutangaza biashara zao, wadau wote mnakaribishwa sana.

MAWASILIANO +2673776463/+[email protected]

Videos (show all)

Mbande Secondary School, DSM

Location

Category

Telephone

Address

80502
Tanga
255
Other Education in Tanga (show all)
Academic revolution Academic revolution
Chanika- Handeni
Tanga

Chumbageni Primary School Chumbageni Primary School
Tanga

Chumbageni Primary School is in Tanga, Tanzania. Over 1000 children ages 4 to 13 are enrolled, taught by a staff of 27.

The pain master's The pain master's
Makorora Tanga
Tanga

Galanosi boys high school Galanosi boys high school
Tanga

Our school located at nguvumal street 5km from tanga bus terminal.

The Best Indicies Forex Brokers The Best Indicies Forex Brokers
Tanga
Tanga, 434

https://track.deriv.com/_HJ4paoojYYW2vdm9PpHVCmNd7ZgqdRLk/1/

David Togolani Mashambo David Togolani Mashambo
P.O BOX 5395 SAHARE
Tanga, +255719992280

sharing social,economic and religious experience

Ronagi Health Informtion center Ronagi Health Informtion center
Tanga, 255

Ronagi health information centre is one among which covers different services 'It is located at Tanga.

Vifrem Entrepreneurship Training Agent Vifrem Entrepreneurship Training Agent
[email protected]
Tanga, BOX 483 KOROGWE

Non Government Organization conerning with providing education about health, enterpreneurship, psychology, agriculture and livestock keeping advice

IJUE DINI YA Kiislam IJUE DINI YA Kiislam
Tanga, 53

IJUE DINI YA KIISLAM