MAARIFA YA KIISLAM| Ukumbusho.
📌 Funga siku ya Saba (7).
عَنْ عَلِیِّ بْنِ الْحُسَیْنِ ع قَالَ: لَیْسَ لَکَ أَنْ تَتَکَلَّمَ بِمَا شِئْتَ لِأَنَّ اللَّهَ یَقُولُ وَ لا تَقْفُ ما لَیْسَ لَکَ بِهِ عِلْمٌ وَ لَیْسَ لَکَ أَنْ تَسْمَعَ مَا شِئْتَ لِأَنَّ اللَّهَ عَزَّ وَ جَلَّ یَقُولُ إِنَّ السَّمْعَ وَ الْبَصَرَ وَ الْفُؤادَ کُلُّ أُولئِکَ کانَ عَنْهُ مَسْؤُلًا [١].
Imamu Zainul Aabidin - as: "Hupaswi kuzungumza kila ukitakacho, kwa sababu Allah anasema {Wala usiyafuate usiyo na Ujuzi nayo}..
Na hupaswi kusikiliza kila ukitakacho, kwa Sababu Allah aliyetukuka anasema: {Hakika Masikio na Macho na Moyo, vyote hivyo vitahojiwa (vitasailiwa) [1]".
1. 📚 Suratul Israa": 36.
2. 📚 Wasail Shia: 15/171.
t.me/ahlul_bait14
babulitra
Ukurasa huu ni Maalum kwa ajili ya kufikisha Ujumbe wa Allah (s.a.w.w.) kwa Mafundisho ya Maasumina (as), kutoka katika Qur'an na Sunna za Maasumina (as).
NURU YA QUR'AN| Wasia bora kutoka katika Qur'an na Sunna.
✍ Na ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote viliomo katika mbingu na viliomo katika Dunia, Na kwa hakika tuliwausia walio pewa Kitabu kabla yenu, na nyinyi pia, kwamba mumche Mwenyezi Mungu, na mkikataa, basi ni vya Mwenyezi Mungu viliomo mbinguni na viliomo duniani, na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, anajitosha, na Msifiwa. [1].
👉 Imamu Swaadiq (as) anasema: "Wasia bora, na wakuulazimu muda wote, ni usimsahau Mola wako, daima umkumbe na usimiasi, umuabudu uwe umekaa ama umesimama, na wala usipumbazike kwa neema zake bali daima mshukuru..
Na wala usitoke chini ya stara ya rehma zake, utukufu wake na ukuu wake, kiasi ukapotea na kuangukia katika uwanja wa maangamizi, hata k**a utakumbwa na mabalaa, madhara na ukakuchoma moto wa matatizo.
Na tambua kwamba, Mabalaa yake (mola mlezi) yamejazwa ukarimu wake wa kudumu, na matatizo huleta ridhaa yake na ukaribu wake, hata k**a litakuwa ni baada ya muda (vyovyote utakavyokuwa katika mitihani na matatizo, pasina kujali ni muda gani - rehma na ukaribu wa Mungu kwako vipo mbioni, kiasi vikikufika utasahau k**a uliwahi kupitia kipindi fulani kigumu, hivyo mitihan ya hapa na pale ni sehemu ya majaribu ya muumba yenye faraja tele mbeleni)..[2].
1. 📚 Surat Nisaa: 131.
2. 📚 Tafsirul Burhan: 2/185.
t.me/nuruquran.
MAARIFA YA KIISLAM| Kuhusu kumjua Allah (as).
✍ Imamu Baaqir (as): kuhusu Kauli ya Allah (s.w.w.) isemayo: {na yule ambaye katika Dunia hii ni kipofu, basi na Akhera pia ni Kipofu}
Yule ambaye kuumbwa kwa Mbingu na Ardhi, na kibadilika kwa usiku na mchana, na kuzunguka kwa Sayari, Jua na Mwezi, na alama nyinginezo za ajabu (zilizopo katika Ulimwengu huu), (ikiwa vyote hivi) havikumuashiria kwamba nyuma haya pana jambo adhimu kuliko, basi akhera atakuwa ni kipofu - na aliyepotea njia".
📚 Biharul Anuwar: 3/27.
Maelezo: ambaye uumbwaji na mpangilio makini wa ulimwengu mzima, haukumsaidia kuona kwamba nyuma ya uumbaji huu pana jambo Adhim, kwa maana pana aliyemtukufu, makini, mjuzi asiye na mfano, mwenye hekima, wa kipekee, ambaye ndiye mola mlezi na muumba wa ulimwengu huu..
Au kwa maana ingine, ambaye hakujifunza jambo katika ustadi wa uumbwaji wa ulimwengu na mpangilio wake kwamba kuna mungu asiye na mfano..
Basi Mtu huyu akhera atakuwa ni kipofu zaidi na aliyepotea kwa atakayozidi kukutana nayo..
Ndham ya uumbwaji wa ulimwengu ni ishara na dalili tosha ya kuthibitisha uwepo, na uungu, ukuu, ufalme, wa mwenyezi mungu Allah (s.w.w.), bila ya kuwa na mshirika yoyote.
Bali kwa hili, ni haki yake kwetu, kumtakasa, na kumuepusha na kila aina ya dosari pamoja na kutomshirikisha na chochote kile.
t.me/ahlul_bait14
KUHUSU| Kujibiidhisha kutenda kheri, na kuyaacha yaliyo ya shari.
Imamu Ally (as):
قَالَ ع افعَلُوا الخَيرَ وَ لَا تَحقِرُوا مِنهُ شَيئاً فَإِنّ صَغِيرَهُ كَبِيرٌ وَ قَلِيلَهُ كَثِيرٌ وَ لَا يَقُولَنّ أَحَدُكُم إِنّ أَحَداً أَولَي بِفِعلِ الخَيرِ منِيّ فَيَكُونَ وَ اللّهِ كَذَلِكَ إِنّ لِلخَيرِ وَ الشّرّ أَهلًا فَمَهمَا تَرَكتُمُوهُ مِنهُمَا كَفَاكُمُوهُ أَهلُهُ.
Fanyeni kheri na wala msidharau chochote katika kheri, kwani kidogo chake ni kikubwa, na kichache chake ni kingi..
Na wala asiseme yeyote katika nyinyi: "Hakika fulani, ndio mbora zaid kufanya kheri kuliko mimi", na Wallah ikawa hivyo..
Hakika Kheri na Shari zina watu wake, vyovyote mtakavyoacha kufanya katika viwili hivyo, basi watakutoshelezeni (kuvitenda) watu wake.
📚 Nahjul Balagha - Hekma na. 422.
t.me/nahjualy
MAARIFA YA KIISLAM| Kujiepusha na Shiriki.
✍ Mwenyezi Mungu Allah (s.w.w.): "Enyi watu! Muabuduni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni nyinyi na wale wa kabla yenu, ili mpate kuokoka.
(Mwenyezi Mungu) ambaye amekufanyieni hii ardhi kuwa k**a tandiko, na mbingu k**a paa, na akateremsha maji kutoka mbinguni, na kwayo akatoa matunda yawe riziki zenu.
*Basi msimfanyizie Mwenyezi Mungu washirika, na hali nyinyi mnajua".* [1].
Baada ya kuona hekma ya Uumbaji wa Allah wa Ardhi, Mbingu na Mvua, Mwenyezi Mungu (Allah - s.w.w.) ak**alizia kwa kusema: *{Basi msimfanyizie Mwenyezi Mungu washirika, na hali nyinyi mnajua}.*
👉 Imamu Askari (as) anasema: "Msimjaalie Mwenyezi Mungu Mifano wala msimfananishe (katika uungu na ukuu na chochote) katika Masanamu (na vingenevyo vyenye kutiiwa, kunyenyekewa, kuombwa na kuabudiwa pasina ya Allah - s.w.w).
Ambavyo havina Akili, havisikii, havioni, wala havina uwezo wowote, {na hali nyinyi mnajua} kwamba, haviewezi kuleta chochote katika neema hizi tukufu ambazo amekuneemesheni Mola wenu aliyetakasika (na kila dosari)". [2].
📌 *Hoja ya Msingi:* Kwanini ukiabudu, ukinyenyekee, ukiombe, ukiamini kisicho na uwezo wa kuumba wala kuleta neema k**a ambazo Allah katuneemesha..
Na hali tunajua fika kuwa ni viumbe, vingine tumevitengeza wenyewe, vingine tumeaminishwa tu, vyenyewe havijiwezi bila msaada wa Muumba?
Basi turejee kwa Mola wa Hakii, ambae ni asili ya kila kitu, hana mfano wa mshirika, bali yeye ndiye muumba wa kila kitu.
1. 📚 Suratul Baqara: 21 - 22.
2. 📚 Tafsirul Burhan: 1/153.
t.me/ahlul_bait14
NURU YA QUR'AN.
وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّهَ كَانَ بِهِ عَلِيمًا.
Na kheri yoyote mnayo fanya Mwenyezi Mungu anaijua.
📚 Surat Nisaa: 127.
t.me/nuruquran.
NURU YA QUR'AN.
وَمَن يَعْمَلْ مِنَ الصَّالِحَاتِ مِن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَٰئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ وَلَا يُظْلَمُونَ نَقِيرًا.
Na anaye fanya mema, akiwa mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini - basi hao wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa hata kadiri ya tundu ya kokwa ya tende.
📚 Suratu Nisaa: 124.
t.me/nuruquran
MAARIFA YA KIISLAM| Hekma katika Uumbaji wa Allah (s.w.w.).
📌 Kuumbwa kwa Ardhi.
Katika kujenga msingi madhubuti wa Itikadi sahihi juu ya Allah (s.w.w.), kuhusu uwepo wake, Ukuu na Ufalme wake, ni kuzingatia katika uumbaji wake na mfumo mzima wa mwenendo wa ulimwengu..
Anasema Allah Mtukufu aliyetukuka: "(Mwenyezi Mungu) ambaye amekufanyieni hii ardhi kuwa k**a tandiko [1].
👉 Kwa nini Allah ameiumba Ardhi katika umbile hili?
Imamu Zainul Aabidin anasema (as): "Ameifanya (ameiumba) ni yenye kuendana na maumbile yenu, yenye kuafikiana na Miili yenu,
Na wala hakuifanya kuwa ni yenye Joto kali kiasi iwaunguze, wala yenye Baridi kali kiasi iwagandishe, wala yenye upepo mkali ikawapeperusha, wala yenye mchanga (udongo) mwingi sana ikawaangamiza..
Wala hakuifanya kuwa laini k**a maji ikawaangamiza, wala hakuifanya kuwa ni ngumu sana ikawazuia katika harakati zenu za kimaisha, na kujenga majengo yenu (Nyumba), na kuchimba makaburi ya Maiti zenu..
Lakini ameifanya kuwa na mchanga (udongo) wenye kuwanufaisha, na wenye kushik**ana nao, na ikashik**ana nayo Miili yenu na Majengo yenu, na akajaalia ndani yake kuwasaidia katika harakat za maisha yenu (kilimo, ujenzi nk), na uchimbaji wa makaburi yenu, na mengi katika munayonufaika nayo, kutokana na hayo akaifanya ardhi kuwa ni tandiko lenu". [2].
Haya ni machache katika hekma ya mengi yaliyomo katika Umbile la Ardhi na Mgongo wake ambalo mwanadamu ananufaika nalo..
Na kila kiungo alichokijaalia Allah ndani ya umbile la Ardhi kinaendana sambamba na mahitaji ya Binadamu na viumbe wengine.
Kila unapozidi kufunua hekima za Uumbaji wa Allah, inakufukia nuru ya uwepo wake, ukuu wake, upekee wake, uwezo wake, nk, katika sifa zake njema.
1. 📚 Albaqara: 22.
2. 📚 Tafsirul Burhan: 1/153.
t.me/ahlul_bait14.
MAARIFA YA KIISLAM| Kumtii Allah - Mola mlezi wa kila kiumbe.
✍ Mwenyezi Mungu, Allah (s.w.w.) anasema:
Enyi watu! Muabuduni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni nyinyi na wale wa kabla yenu, ili mpate kuokoka. [1].
👉 Imamu Askari katika tafsiri ya Aya hii anasema: {Muabuduni Mola wenu Mlezi} yani: Mtiini Mola wenu mlezi katika kile alichokuamrisheni..
Muitakidi (na kuamini kwamba) hapana Mungu apasaye kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allah pekee..
Wakipekee asiye na Mshirika, wala mfano wala wa kulinganishwa nae..
Muadilifu asiyedhulumu, mkarimu asiyefanya ubakhili, mpole asiyepupia, mwenye hekima asiyekosea..
Na kwamba Muhamad ni Mja na Mtume wake, na kwamba, kizazi cha Muhamad ni bora ya vizazi vya manabii, na Ally (Bin Abitaalib) ni mbora katika Familiya Muhamad..
Na Maswahaba wa Muhamad walioamini miongoni mwao, ni wabora kuliko Maswahaba wa Mitume wote..
Na kwamba Uma wa Muhamad, ni mbora kuliko Nyuma nyingine zote".
Kisha M. Mungu akasema: {Na ambaye amekuumbeni}, Muabuduni ambaye amekuumbeni kutokana na tone la maji dhalili, akaliweka katika kitulizo makini (sehemu ya kurutubishwa mbegu ya mwanaume), mpaka katika makadirio maalum, akaikadiria, na mbora wa kukadiria ni Mola mlezi wa Walimwengu".[2].
1. 📚 Suratul Baqara: 21.
2. 📚 Tafsirul Burhan: 1/152.
t.me/ahlul_bait14
NURU YA QUR'AN.
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَنُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۖ وَعْدَ اللَّهِ حَقًّا ۚ وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّهِ قِيلًا.
Na wale walio amini na wakatenda mema, tutawaingiza katika Bustani zipitayo mito kati yake, watadumu humo milele, ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu iliyo kweli, na nani mkweli zaidi kwa usemi kuliko Mwenyezi Mungu.
📚 Surat Nisaa: 122.
t.me/nuruquran
MAARIFA YA KIISLAM| Ipe haki yake Siku ya Ijumaa.
✍ Fahamu miongoni mwa Mambo muhimu ya Siku ya Ijumaa.
👉 Ndio siku bora aliyoiumba Allah (s.w.w.), Imamu Baaqir (as): "Jua halikuchomoza katika Siku bora kuliko siku ya Ijumaa, hakika mazungumzo ya ndage wanapokutana wao kwa wao husema: Amani, amani leo ni siku njema".[1].
👉 Kujipamba kwa Usafi na Furaha na kila jema katika siku hii, Imamu Swaadiq (as): "Ajipambe mmoja wenu siku ya Ijumaa, akoge, ajipake manukato, atengeze ndevu zake, avae nguo safi, ajiandae na Swala ya Ijumaa, na awe na utulivu na upole katika siku hii, afanye ibada kwa uzuri zaidi, afanye kheri kwa kadri awezavyo, kwani Allah huwatazama walio ardhini na kuwaongezea mema (katika siku hii)". [2].
Zingatia: Usafi unajumuisha mambo yote ya usafi, Kukata kucha, kutengeneza nywele (za nje na ndani) nk.
👉 Ijumaa ni Sikukuu, tenga muda wako kadri uwezavyo kuistarehesha na kuipumzisha Nafsi yako au Familiya.
Imamu Ally (as): "Hakika siku hii Allah ameifanya kuwa ni Idi (skukuu) kwenu, nayo ni bora ya masiku, na ni sikukuu bora". [3].
HAYA NI WAJIBU KWA MUUMINI KUYAFANYA.
👉 Kukoga Ghusli: Imamu Ridhwa alipoulizwa kuhusu kuoga Ghusli ya Ijumaa: "Ni Wajibu kwa kila Wakiume na Wakike, awe Mtumwa au huru". [4]
👉 Kusoma Suratul Jumaa na Munaafiqun katika Swala za Mchana wa Ijumaa, Imamu Swaadiq (as): "Wajibu kwa Kila Muumini ambae ni Shia wetu, Asome katika (Swala za) Usiku wa Ijumaa, Suratul Jumaa na Sabihismarabikal aala, na katika Swala ya Dhuhuri (Swala za mchana) Suratul Jumaa na Munaafiqun". [5].
1. 📚 Alkafi: 3/415.
2. 📚 Alkafi: 3/417.
3. 📚 Wasail Shia: 7/378.
4. 📚 Alkafi: 3/41.
t.me/ahlul_bait14
NURU YA QUR'AN.
وَمَن يُطِعِ اللَّهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُولَٰئِكَ رَفِيقًا.
Na wenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume, hao wa pamoja na wale alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na Masiddiqi, na Mashahidi, na Watu wema, na uzuri ulioje kuwa pamoja na watu hao!
ذَٰلِكَ الْفَضْلُ مِنَ اللَّهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّهِ عَلِيمًا.
Hiyo ni fadhila itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kutosha.
📚 Surat Nisaa: 69 - 70.
t.me/nuruquran
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the school
Telephone
Website
Address
Tanga