Mwl Salum Masudi

Mwl Salum Masudi KUKUMBUSHANA KUTENDA HAKI

17/02/2024

Somo la Elimu Ya Dini Ya Kiislamu kwa kidato cha nne 2024

Litakuwa na sehemu A, B na C
BISMILLAHIR RAHMAANIR RAHIM
ELIMU YA DINI YA KIISLAMU
Mifano ya swali la pili (NECTA)
Maswali ya kipengele hiki, yanahusu “NGUZO ZA UISLAMU”, Juzuu 1 & 2 na yanakuwa ya KUOANISHA.
Mfano: No. 1 (SHAHADA)
Oanisha dhana za shahada zilizopo katika Orodha A na asili ya dhana hizo zilizopo katika orodha B.
ORODHA A
ORODHA B

Kiingilio katika Dini ya Uislamu
Ahadi ya utii kwa Mwenyezi Mungu (s.w).
Mafungamano ya Allah (s.w) na Mtume (s.a.w)
Ahadi ya utii kwa Mtume (s.a.w)
Kuikanusha shahada kivitendo katika maisha.
Imani thabiti juu ya Allah (s.w) na Mtume Wake.
Shahada moja
Kutamka shahamba mbili
Ushirikina
Shahada ya kwanza
Utawa
Chimbuko la shahada ya kweli
Ishara ya shahada mbili
Shahada ya pili

Majibu:
Majibu ya swali hili, ni vizuri yapangwe katika utaratibu ufuatao:
Orodha A
(i)
(ii)
(iii)
(iv)
(v)
(vi)

Orodha B
B
D
F
H
C
G

Mfano NO: 02 (Kusimamisha Swala)
Oanisha kifungu cha maneno kilichopo orodha A na yale yaliyomo katika orodha B.
Orodha A
Orodha B

Kupotewa na akili au kulala ndani ya swala.
Kuswali rakaa mbili kuomba msaada kwa Allah (s.w).
Ni miongoni mwa nguzo za swala
Kuosha kila kiungo cha UDHU mara tatu
Mambo ya lazima anayotakiwa Muislamu ayachunge kabla ya kuswali
Matendo yanayozuiwa kwa mwenye Hadathi ndogo
Swalatul-Haajah
Masharti ya swala
Mambo yanayobatilisha swala
Kukaa Tahuyyatu
Kusoma Qur’an
Kuzunguka Al-Kaaba mara saba
Qiyaamul-layl
Sunnah za kutawadha

Majibu: “Rejea maelezo ya mwanzo”

Orodha A
(i)
(ii)
(iii)
(iv)
(v)
(vi)

Orodha B
C
A
D
H
B
E

Mfano NO: 03 “Kutoa Zakat”

Oanisha kifungu cha maneno Orodha A na cha Orodha B.

ORODHA A
ORODHA B

Kutoa huduma au mali kwa mtu yeyote anayehitaji bila ya malipo kutoka kwake.
Miongoni mwa mambo ambayo hukamilisha utoaji wa zakat na sadaqat
Ni kiwango cha mali ambacho kikifikia inastahiki kutolewa zakat
Ni mali ambayo haijuzu kutolewa zakat
Baadhi ya mali zinazojuzu kutolewa zakat
Kiwango cha zakat ya mali ya kuokotwa au kuchimbuliwa chini
Masharti ya zakat na sadaqat
Wanyama wafugwao kwa ajili ya chakula
Farasi na punda
1/5 au asilimia 20 ya mali hiyo
2/5 au 10%
Mbwa na ngamia
Nisaab
Maana ya sadaqat kisheria

Majibu: “Rejea maelezo ya mwanzo”
Orodha A
(i)
(ii)
(iii)
(iv)
(v)
(vi)

Orodha B
H
A
G
C
B
D

Mfano NO: 04 “Kufunga mwezi wa Ramadhani”

Oanisha kifungu cha maneno Orodha A na cha Orodha B.

ORODHA A
ORODHA B

Ni kujizuia kufanya jambo lolote la kawaida
Ni kufunga mja kutokana na kutenda kosa fulani, ikiwa ni kitubio cha kosa hilo.
Ni funga alizozitekeleza Mtume (s.a.w) na kukokotezwa zitekelezwe
Ni funga inayotekelezwa mwezi 9 (Dhul-Hijja) kwa asiyekuwa Hijja
Kufunga siku ya Iddil-Fitri na Iddil-Hajj
Ni lazima kwa mja aitekeleze na ni nguzo miongoni mwa nguzo tano za Uislamu
Funga ya kafara
Funga ya Ramadhani
Funga ya Arafa
Siku zilizoharamishwa kufunga
Maana ya funga kilugha
Maana ya funga kisheria
Funga ya Ashura
Funga za Sunnah

Majibu: “Rejea maelezo ya mwanzo”
Orodha A
(i)
(ii)
(iii)
(iv)
(v)
(vi)

Orodha B
E
A
H
C
D
B

Mfano NO:05 “Kuhiji Makka kwa mwenye uwezo”

Oanisha kifungu cha maneno Orodha A na cha Orodha B.

ORODHA A
ORODHA B

Ni kitendo cha Hajj kuizunguka Al-Kaaba mara saba
Ni kutembea mara saba baina ya vilima viwili (Safa na Marwa)
Ni aina ya Hija ambapo Hajj hunuia kufanya Hija tu bila ya Umrah
Ni maneno ayasemayo Hajj ya kuitikia wito wa Allah (s.w)
Ni mzunguko wa kuaga ambao hufanywa na Hajj anaporejea kwao
Ni moja ya matendo anayoyatekeleza Hajj siku ya mwezi 10 (Dhul-Hijja)
Talbiya
Ifrad
Twawaf
Qiran
Twawaful-Ifaadha
Tawaful-Widaa
Sai
Talqiin

Majibu: “Rejea maelezo ya mwanzo”

Orodha A
(i)
(ii)
(iii)
(iv)
(v)
(vi)

Orodha B
C
G
B
A
F
E

MASWALI YA SEHEMU B “Kujibu kwa ufupi”
Sehemu hii ina alama 54 ambayo inakuwa na maswali sita (06) kutoka katika MADA tofauti tofauti, kuanzia swali la tatu mpaka la nane. Yafuatayo ni maswali katika MADA zinazohusika.
3. FAMILIA YA KIISLAMU
- Talaka na Eda
- Mirathi katika Uislamu
- Ndoa katika Uislamu Kidato cha Nne
- Kudhibiti Uzazi katika Uislamu
- Hadhi na Haki za Mwanamke katika Uislamu

Mfano wa swali:
Waislamu wengi katika nchi ya Tanzania hawajui mambo mengi ya kisheria yanayohusu Uislamu kiasi cha kuzusha migogoro kadhaa katika mirathi, ndoa n.k. Ukiwa k**a Imamu wa Msikiti wa Micheweni:
Elimisha jamii yako kwa kufafanua HAKI tatu zinazofungamana na mali ya mirathi.
Rithisha familia ambayo amekufa mke na kuacha mume, baba yake mzazi na dada yake shaqiqa.

NGUZO ZA IMANI
- Kumuamini Mwenyezi Mungu (s.w)
- Shirki
- Kuamini Malaika wa Mwenyezi Mungu
- Kuamini Vitabu vya Mwenyezi Mungu Kidato cha tatu cha nne
- Kuamini Mitume wa Mwenyezi Mungu
- Kuamini siku ya mwisho
- Kuamini Qadar ya Mwenyezi Mungu

Mfano wa swali
Ukisoma Historia ya Uislamu, utaona Allah (s.w) aliwapeleka Mitume kwa Qaumu mbali, ili kuwaongoza katika njia iliyo sahihi anayoiridhia Allah (s.w). Bainisha sababu tatu zilizopelekea kwa Allah (s.w) kumpelekea Mtume baada ya mwingine kuondoka.

5.
HAKI NA UADILIFU KATIKA UISLAMU
- Dhana ya haki na uadilifu katika Uislamu
- Msimamo wa Uislamu juu ya utumwa

Mfano wa swali
Makafiri wanadai kuwa Uislamu unahimiza na unaendeleza biashara ya utumwa. Ukiwa k**a Muislamu ukipinga hoja hiyo, eleza kwa kutumia hoja sita (06) kuonesha jinsi Uislamu ulivyokomesha biashara hiyo.

6. DOLA YA KIISLAMU MADINAH
- Uanzishwaji wa Dola ya Kiislamu Madinah
- Uendeshaji wa Dola ya Kiislamu Madinah
- Upinzani dhidi ya Dola ya Kiislamu Kidato cha tatu
- Ushindi wa Waislamu (Fat-hu Makka)
- Kutawafu kwa Mtume (s.a.w)

Mfano wa swali
Kutokana na uadui mkubwa wa Makafiri dhidi ya Waislamu ulipelekea kutokea vita mbalimbali, ambavyo mara kadhaa Waislamu walikuwa wanashinda kwa msaada wa Allah (s.w). Bainisha vipengele vitatu ambavyo vinaonesha kuwa ni msaada wa Mwenyezi Mungu katika uwanja wa BADRI.

7. MFUMO WA JAMII YA KIISLAMU
- Misingi na Maadili katika Uislamu
- Sheria katika Uislamu Kitabu cha nne
- Uchumi katika Uislamu
- Siasa na Uendeshaji wa Dola

Mfano wa swali:
Waislamu tunatakiwa tujishughulishe katika kazi mbalimbali za halali ambazo zitatunufaisha na kutuwepesishia katika maisha yetu. Ainisha bidhaa za aina tatu na ukizitolea mifano, ambazo Allah (s.w) amezikataza.

8. HISTORIA YA KIISLAMU BAADA YA KUTAWAFU MTUME (S.A.W):
- Ukuaji na Uendeshaji wa DOLA ya Kiislamu wakati wa Makhalifa
wanne waongofu. Kitabu
- Uanzishwaji wa makundi ya harakati za kuhuisha Uislamu ulimwenguni. cha
- Kuingia kwa Uislamu Tanzania na Afrika Mashariki. Nne

Mfano wa swali:
Umar bin Abdul-Aziz ni miongoni mwa viongozi waliowaongoza Waislamu baada ya kutawafu Mtume (s.a.w). Kutokana na mazuri aliyoyafanya baadhi ya wanachuoni wa Kiislamu wamemuhesabu k**a Khalifa wa tano wa Dola ya Kiislamu. Ainisha mambo sita ya msingi aliyoyafanya kiongozi huyu katika uongozi wake.

MASWALI YA SEHEMU C “Maswali ya Insha”
Sehemu hii inakuwa na maswali matatu (03) na mwanafunzi anatakiwa ajibu maswali mawili tu, ambapo kila swali linakuwa na alama 15, hivyo jumla ya alama zote katika sehemu hii ni alama 30.
Maswali ya sehemu hii yanajibiwa kwa njia ya Insha, kwa kuzingatia kanuni zake. (Utangulizi, Dondoo na Hitimisho).
Mada zinazohusu (zinazopimwa) katika sehemu hii ni tatu (03), ambazo ni:
Nguzo za Uislamu - Kidato 3
Qur’an - Kidato 3 & 4
Sunnah na Hadith - Kidato 2 & 3

NGUZO ZA UISLAMU - Kusimamisha swala Kidato
Zakat cha
Swaumu ya Ramadhani Tatu
Hijja
Mfano wa swali
Funga “swaumu” ni Madrasa maalum inayowafunza Waislamu na kuwaandaa kufikia katika ucha Mungu. Kwa kutumia nukta nne (04), eleza namna ya madrasa hiyo inavyowaandaa Waislamu hao kufikia katika daraja hilo.

Majibu ya swali hili ni vizuriyawe katika mpangilio ufuatao:

Utangulizi: ______________________________________________________________
________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________
Dondoo:_________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

Hitimisho:_______________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

QUR’AN:
- Sura za Makkah na Madinah
- Kukusanywa Qur’an katika msahafu
- Ithibati ya Qur’an kuwa ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu (s.w) Kidato cha 3 & 4
- Sura zilizoteuliwa (Fyl, Humazah, Asr, Takaathur, Bayyinah,
Tyn, Nashrah, Dhuha na A’alaa)
Mfano wa swali
Kwa kuwa mazingira ya kipindi cha Utume cha Makkah na Madinah yalitofautiana, pia sura nazo zinautofauti kwa kuzingatia walengwa, ujumbe, muundo wa sura na mbinu. Chambua tofauti hizi nne.
- Majibu yazingatie maelekezo ya mwanzo.

Ukiisoma suratul-Fyl na kuzingatia maana yake utagundua uwezo wa Allah (s.w) alionao kwa viumbe wake. Kwa mantiki hii, fafanua mafunzo manne (4) tunayoyapata ndani ya sura hii.
- Majibu yazingatie maelekezo ya mwanzo.

SUNNAH NA HADITH
- Uandishi wa Hadith za Mtume (s.a.w)
- Uchambuzi wa Hadith za Mtume (s.a.w) Kidato cha 2, 3 & 4
- Hadith za mafunzo maalum
- Kukubalika kwa Hadith

Mfano wa swali
Mwalimu Hafidh alipofika katika Shule ya AHBAAB alipewa kitabu chenye mchanganyiko wa Hadith sahihi na zisizo sahihi. Unafikiri ni nukta gani atazitumia Mwalimu Hafidh zitakazombainishia Hadith sahihi na zisizo sahihi.
Ukisoma katika Historia ya ukusanyaji, uhifadhiji wa Hadith za Mtume (s.a.w) katika maandishi, utaona zimepitia katika hatua takriban nne. Fafanua hatua hizo kwa kuelezea kila hatua mpaka kufikia kukamilika kwake.
- Majibu yazingatie maelekezo ya mwanzo.
Maelekezo:
Ukiuangalia muundo wa mtihani na mada zinazohusika katika kupima mtihani huu, utagundua kuwa kuna mada ambazo zinatakiwa zitiliwe mkazo kwa wanafunzi ili waweze kufaulu. Mada hizo tunaziita MADA ZA MKAKATI:
Nguzo za Uislamu
Sunna na Hadith
Qur’an
Haki na Uadilifu
Dola ya Kiislamu Madina
Familia ya Kiislamu
Nguzo za Imani
Mfumo wa jamii ya Kiislamu
Historia baada ya kutawafu Mtume (s.a.w)
WABILLAHIT-TAWFIQ

02/07/2023
0.53 $ ,dhahabu ya kijani mwaka huu inapanda na kushuka tuwe makini wajasiriamali
14/09/2022

0.53 $ ,dhahabu ya kijani mwaka huu inapanda na kushuka tuwe makini wajasiriamali

Teachers
16/05/2022

Teachers

Tukifundisha kwa lugha tunayoimudu , wanafunzi na mwalimu kutaondoa udikteta uliotamalaki katika elimu ya kwamba ndiye a...
28/04/2022

Tukifundisha kwa lugha tunayoimudu , wanafunzi na mwalimu kutaondoa udikteta uliotamalaki katika elimu ya kwamba ndiye anayejua peke yake na kutengeneza jamii yenye uwezo wa kuhoji na kutambua fursa zilizopo .

25/04/2022
Skonga
07/04/2022

Skonga

Kumbe hesabu unaweza kufundishia sekondarii kwa Kiswahili.
29/03/2022

Kumbe hesabu unaweza kufundishia sekondarii kwa Kiswahili.

21/03/2022

WWE

Address

Tandahimba

Telephone

+255659294283

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mwl Salum Masudi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to Mwl Salum Masudi:

Shortcuts

Share

Category