11/11/2022
KULIKONI? HISTORIA YA ZANZIBAR.
Leo Zanzibar ni sehemu ya Tanzania kwa miaka hamsini na miwili; lakini Mwaka 1503/1504 ilikuwa ni sehemu ya Ureno kwa miaka mia mbili! Mwaka 1698,ilikuwa ni sehemu ya Oman kwa miaka takriba miambili pia! Mwaka 1890 ,Zanzibar ilikuwa ni sehemu(himaya) ya Uingereza kwa zaidi ya miaka sabini na tatu Kwa mkataba wa Heligoland-Zanzibar Treaty .Kunani?
Naadika historia hii ilituone ndani ya hiyo historia ya Zanzibar ambayo kila siku tunaambiwa ndiyo tatizo. Kuna nini humo? Jee ni kweli kuwa matatizo ya Zanzibar yanaletwa na historia?
BENDERA YA ZANZIBAR NA NEMBO YA ZANZIBAR VIPO
WIMBO WA TAIFA:“Mungu ametubarikia Unguja na Pemba yote. Sote tunashangiria…”
Pahala ilipo-Barani Afrika, Afrika ya Mashariki-Tanzania.(United Republic of Tanzania)
Zanzibar ni miongoni mwa visiwa vya bahari ya Hindi.vilivyo katika mwambao wa Kiswahili,ubavuni-sambamba na Tanzania-bara (Tanganyika).
Ncha ya Kaskazini ya kisiwa cha Unguja ipo nyuzi-digirii 5.72,Kusini nyuzi-digrii 39.30 Mashariki-nchani,Nyuzi-digirii 6.48 nyuzi-digirizi Kusini, 39.51 nyuzi-digirizi Mashariki. Kisiwa cha Zanzibar kimetenganishwa na Tanzania-bara kwa Mkondo mwembamba wa kilomita 36.5 sawa na maili 22.7. Zanzibar inaurefu wa wastani km 85 (53 mi) na upana km 39 (24 mi), ikiwa na eneo la wastani wa km mraba 1,464 km2 (565 sq mi).
Unguja ni kisiwa tambarare karibu na usawa wa bahari.Mlima mkubwa kuliko yote ni Masingini wenye urefu wa mita 120 sawa na futi 390. Visiwa hivi hunukia marashi mbalimbali k**a karafuu,hiliki nk. Ni kisiwa chenye miamba na samaki wa kila aina,wataamu kwa ladha, na wanapendeza kwa macho.
Pemba kipo nyuzi-digirii 4.87 kusini, 39.68 mashariki, na ncha ya kusini mwisho ni nyuzi-digirii 5.47,mashariki ni digirizi 39.72. Kisiwa hiki kimetenganishwa na mkondo baina yake na bara kwa upana wa km 56 au maili 35.
Pemba inaurefu wa km 67 sawa na maili 42 na km 23 upana au maili 14 . na eneo la km, 985 km2 (380 sq mi).Mlima mkubwa zaidi ni urefu wa mita95- (312 ft).
VISIWA VIKUBWA VIWILI UNGUJA NA PEMBA.
HADHI-Inajitegemea kwa baadhi ya mamlaka zake za ndani, k**a kilimo nk.
MJI MKUU : Zanzibar city
LUGHA- Kiswahili na Kingereza.
DINI (95%)waislam (kwa sasa)kwa mujibu wa kanisa moja. %4.wakristo .
WAKAAZI- Wazanzibari.
UKUBWA WA ENEO JUMLA NI:
= 2,461 km2
950 sq mi
IDADI YA WATU KWA SENSA YA MWAKA 2012
• 1,303,569
• Sawa na watu
529.7/km2
1,371.9/sq mi
Pato la GDP 2012 estimate
• $860 million
• $656
Fedha inayotumika-Shilingi ya Tanzania (TSH)
Time zone Ukanda wa saa UTC+3) EAT. CODE +255. Internet TLD. .tz
•
Zanzibar ni sehemu ya Tanzania.Ni visiwa vyenye kujiendesha kwa baadhi ya mambo yake ya ndani,mengine yanaendeshwa na Serekali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.Muungano huu ni wa mwaka 1964. Zanzibar ipo bahari ya hindi wastani wa maili 16-36 Mashariki ya Tanzania bara. Ina visiwa vingi vidogo na vikubwa viwili Unguja na Pemba. Mji wake mkuu ni Zanzibar City ,ni mji mkongwe ukiwa chini ya UNESCO ,k**a urithi wa Dunia
Neno au jina Zanzibar linatokana na lugha za kiarabu-Zanjibār (زنجبار), na Kiajemi-Persian- Zang-bār (زنگبار), yakimaanisha “Nchi ya watu weusi”.Binaadamu walianza kuishi Z’bar kwa zaidi ya karne miambili au tatu zilizopita, kabla ya kuzaliwa Nabii Issa. (Jesus)
1000 BC.
Waajemi, na waarabu walisafiri baina ya miji yao na Zanzibar wakitumia pepo za kaskazi na kusi-(Monsoon winds Dec-Feb,Apr-Sep),kwa biashara.Nchi ya Zinj ilianza kutajwa wakati wa Mfalme Suleiman,ikiwa ni sehemu ya dola ya Sheba au Saba,chini ya Malkia Bilqis,ambao walihodhi biashara za bahari ya hindi-viungo (spice) na dhahabu miongoni mwa nyingine,mpaka karne moja BC, ambapo misafara ilianza kupita nchikavu.Hippalus- Mmisri alitoa siri za kuwepo monsoon kwa wazungu.Awali ilikuwa siri ya baadhi ya makabila tu mpaka mwaka 45 BC.Katika kipindi hiki pia makabila mengi ya Afrika yalijongea Zanzibar kufanya maskani.Watu hao walikuwa warefu na waliabudu miti-mizimu na Jua.
630 AD Oman ilisilim na kuwa nchi ya kiislam. Mageuzi makubwa ya kiutamaduni na kiuchumi, yaliitikisa Bara arab na Uajemi.Wengi wa mabaharia na wafanyabiashra walihamia pwani ya Afrika Mashariki; kuanzia miji ya Mogadishu,Somalia hadi pwani ya Cape Delgado ,Msumbiji,wakiendeleza biashara zao baina ya Afrika ,Uajemi na India.
Miji hii ya pwani ikapanuka. Karne ya 6 na 11,ikachanganya damu na utamaduni wa kiafrika,kiarabu na kiajemi. Lamu, Pate, Malindi, Mombasa, Brava, Mafia, Bagamoyo, Rhapta, Kunduchi na Kilwa (10thC),ilikuwa tayari ni miji iliyojengwa kwa mipangilio mizuri ya mitaa inayoeleweka. Nyumba za mbao na mawe na Miskiti inayovutia kabisa! Pia ilikuwa na ulinzi imara dhidi ya Maharamia na majambazi.
701 AD Washirazi wanaingia Zanzibar. Wakazaliana na wenyeji ambao ni Watumbatu na Wapemba waliowahi kufika hapa k**a tulivyosema hapo nyuma, karne ya kwanza BC.Mabaki ya miji ya kishirazi yamegunduliwa huko. Tokea karne ya 9 hadi ya 15th Pemba - Al Huthera, “nchi ya kijani” – ilikaliwa na Waajemi ambao walijenga ngome ya Mkumbuu kwa magharibi, Pujini -mashariki na Chwaka.
908 AD Nchi za Mogadishu na Barava iliasisiwa na ndugu saba wa ukoo wa El Hasa.
975 AD Taifa la Kilwa, mashuhuri kwa biashara ya dhahabu,ulianzishwa na Hassan bin Ali, Mwanamfalme wa kiajemi aliyekuja Afrika Mashariki na wanawe sita,wakaishi Zanzibar, Pemba, Mombasa, Kilwa and Comoro.Hawa ni waanzilishi wa Dola ya Zanzibar.-Zenj Empire: 975 - 1503.Dola tunayojisifia,ilifika Sofala.Iliendelea sana hata kuwa na viwanda vya kutengeneza sarafu zake zenye picha za wafalme wake, mmoja baada ya mwengine tangu wa mwaka 900 A.D.na kuendelea,mpaka walipokuja wazungu!Usultani wa Kilwa ulianguka karne ya 18,lakini biashara iliendelea kutamalaki hata kufika China mnamo mwaka 1000 AD,wakaacha mbegu(watoto)! Na mwaka 1430 ,meli ya kichina ilitia nanga Zanzibar,wakitumia dira yao wenyewe (Chinese charts for the Indian Ocean) ya mwaka1200 A.D.
Kitabu cha kale cha karne ya kwanza Periplus of the Erythraean Sea, kinataja Unguja au Pemba- Menuthias (Ancient Greek: Μενουθιάς),na hata wao walishuhudia safari za baharini baina ya Asia, ghuba ya uajemi,Arabuni na Zanzibar.Kulikuwa na bandari nzuri na salama,matengenezo ya Jahazi zao,kuchota maji ya kunywa,na baadhi ya bidhaa kutoka mwambao wa bara na kuendelea na safari. Pia waliingia kujisalimisha na dhoruba zilpowakumba baharini wakiendelea na safari za kusini na kaskazini ya Afrika k**a Msumbiji na kwengineko.Maingiliano haya yameacha alama mbalimbali mpaka leo zinatumika.Ibada ,lugha,vyakula,miji, nk.Madalali walikuwa ni waswahili- wabantu,ambao nao walitajirika kwa kuunganisha baina ya wauzaji na wanunuzi bidhaa.Baadhi ya wageni hawa waliowa na kuoleana na wenyeji,na wakaongoza baadhi ya miji.
Leo Zanzibar ni sehemu ya Tanzania lakini Mwaka 1503/1504 Zanzibar ilikuwa ni sehemu ya Ureno,wakati Capt Ruy Lourenco Ravasco Marques,alipotambuliwa na Sultani.Na ilibaki hivyo takriban miaka mia mbili.Awali ikiwa ni himaya ya Mreno k**a jimbo lake la Arabuni na Ethiopia,ikiendeshwa na Gavana generali; na mwaka 1571 Z’bar iliwekwa jimbo la Mreno la magharibi, ikipokea amri kupitia Msumbiji,huku udhibiti wake ukilegalega.Amri za ndani zikishikiliwa na mtawala wa ndani-Mwinyi-mkuu,ndipo wakati huu ambapo meli ya kwanza kabisa ya kingereza “Edward Bonaventure” ilitia nanga mwaka 1591.Kipindi hiki wenyeji wakiongozwa na Mwinyi-Mkuu wa Dunga, aliyetumia sheria za kiislam wakati Mreno alipigania sana Ukatoliki,akajenga,makanisa,akaleta na nguruwe. Hii inaweza kuwa ni historia inayomwekamweka mpaka leo Zanzibar.
Mwaka 1635, kufuatia mauwaji yaliyofanywa na waarabu huko Mombasa, Wareno walijenga ngome zao huko Pemba...Inaendelea...