29/03/2022
Waebrania 11:6
Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
👉 Tunaweza kuwa Wana MAOMBI lakini, je tunampendeza Mungu wetu?
👉 Tunaweza kufunga na kuomba lakini je, tunampendeza Mungu?
👉 Tunaweza kuwa watoaji na kusali Sana, na wingi wa ibada, lakini je, tunampendeza Mungu?
Swali:- Je, tunawezaje kumpendeza Mungu ?
✍️ Tunaweza kumpendeza Mungu Kwa kuamini.
Swali lingine:- Imani ni Nini ?
✍️ Kuwa na Uhakika wa kupata jambo ambalo hata k**a Bado hujalipata lakini wewe ukae kana kwamba unalo kumbe Bado hujalipata
❤️ Hapo ndipo kumpendeza Mungu
Aminaa
Kwa Maombi na USHAURI tupigie Kwa +255673812765 au tuandikie Kwa barua pepe [email protected]
Ubarikiwe na Bwana Yesu