PANDA SPORT

PANDA SPORT Kwa mkusanyiko wa habari za michezo,makala,uchambuzi na mahojiano ya soka.

SOONMuda wowote kuanzia sasa tunaweza kumpokea Mtoto wa Dada, Mpwa wetu Bugatti akirejea kwenye timu yake ya Moyoni na s...
19/08/2026

SOON

Muda wowote kuanzia sasa tunaweza kumpokea Mtoto wa Dada, Mpwa wetu Bugatti akirejea kwenye timu yake ya Moyoni na sisi k**a Wajomba zake tumemsamehe Mtoto wa Dada, Mjomba ni MamaπŸ˜€

β€œKuna vitu tumeviona nasi k**a Klabu tutawaandika Bodi ya Ligi kuwa kuna maboresho wanapaswa kufanya kwenye huu mfumo mp...
19/08/2026

β€œKuna vitu tumeviona nasi k**a Klabu tutawaandika Bodi ya Ligi kuwa kuna maboresho wanapaswa kufanya kwenye huu mfumo mpya wa Video ili kufanya bora zaidi, tutatoa maoni yetu kufanya kuliko hivi sasa”

- Crescentius Magori, Mwenyekiti wa Bodi Simba SC.

Tayari huko FVS imeshafanya yake na Ibrahim Jabaar ametolewa nje kwa kadi nyekundu kosa la kupiga kiwiko.Simba wanacheza...
19/08/2026

Tayari huko FVS imeshafanya yake na Ibrahim Jabaar ametolewa nje kwa kadi nyekundu kosa la kupiga kiwiko.

Simba wanacheza pungufu mara ya pili mfululizo ya kwanza ilikua tukio la Duchu dhidi ya Kagera Sugar

Baraza la Michezo la Taifa, BMT, limetoa ufafanuzi kwa umma, wanachama na wadau wa Klabu ya Simba kuhusu utekelezaji wa ...
19/08/2026

Baraza la Michezo la Taifa, BMT, limetoa ufafanuzi kwa umma, wanachama na wadau wa Klabu ya Simba kuhusu utekelezaji wa Katiba iliyorekebishwa ya klabu hiyo iliyoidhinishwa tarehe 18 Februari, 2026, hatua inayokuja baada ya mashabiki na wanachama wa klabu ya hiyo kulalamima kuhusu utekelezaji wa katiba mpya.

Taarifa iliyotolewa leo Agosti 19, 2026 na Katibu Mtendaji wa BMT, Neema Y. Msitha, imeeleza kuwa marekebisho ya Katiba ya Simba yalipitishwa na Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu ya Simba mnamo Novemba 30, 2025, na kuwasilishwa kwa Msajili wa Vyama na Vilabu vya Michezo kwa uchambuzi na kuidhinishwa kwa mujibu wa sheria na kanuni husika ambapo baada ya uchambuzi huo, BMT kupitia Msajili ilikabidhi rasmi Katiba hiyo kwa Simba ili ianze kutumika.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Serikali imefafanua kuwa ilikamilisha wajibu wake wa kuidhinisha na kukabidhi Katiba hiyo na kuanzia hapo, wajibu wa kutekeleza Katiba na kukamilisha mabadiliko yaliyopitishwa na wanachama ni wa Klabu ya Simba yenyewe na kusisitiza kuwa utekelezaji wa maamuzi yaliyomo katika Katiba hiyo haupaswi kufanywa na Serikali kwa niaba ya Klabu, kwa kuwa ni maamuzi yaliyofanywa na wanachama kupitia Mkutano Mkuu na kuidhinishwa kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo, Serikali inatambua kuwa utekelezaji wa mabadiliko hayo unaweza kuibua masuala ya utaratibu unaohitaji ufafanuzi. Kwa hiyo, BMT na taasisi nyingine husika za Serikali ziko tayari kuipokea Klabu ya Simba kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa utaratibu pale inapohitajika, kwa mujibu wa mamlaka ya kila taasisi.

Hivyo, Serikali inatoa wito kwa Klabu ya Simba kutumia vyombo na taratibu zake halali kukamilisha utekelezaji wa Katiba iliyoidhinishwa, na kuwasilisha rasmi kwa mamlaka husika masuala yoyote yanayohitaji ufafanuzi.

Serikali itaendelea kutekeleza jukumu lake la kuendeleza sekta ya michezo kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu, huku ikilenga maendeleo ya vilabu na sekta ya michezo kwa ujumla wake.

Ni matarajio ya Serikali kuwa masuala ya maendeleo ya michezo yataendelea kushughulikiwa kwa kuzingatia utulivu, uwazi, uwajibikaji maslahi ya wananchi na wapenzi wa michezo.

19/08/2026
Kikosi kazi.
19/08/2026

Kikosi kazi.

π—œπ—¦π—₯𝗔𝗛 𝗣𝗔𝗧π—₯π—œπ—–π—ž 𝗠π—ͺπ—˜π—‘π——π—”Kwanza kabisa Israel Patrick Mwenda ni mchezaji halali wa Yanga mwenye mkataba wa miaka miwili Kwa s...
19/08/2026

π—œπ—¦π—₯𝗔𝗛 𝗣𝗔𝗧π—₯π—œπ—–π—ž 𝗠π—ͺπ—˜π—‘π——π—”

Kwanza kabisa Israel Patrick Mwenda ni mchezaji halali wa Yanga mwenye mkataba wa miaka miwili Kwa sasa, Ikumbukwe msimu uliopita Israel alisaini mkataba wa miaka mitatu hivyo ametumikia mwaka mmoja yaani msimu uliopita.

Israel aliondoka kambini toka tarehe 25,May 2026 Bila ruhusa kutoka Kwa kiongozi yoyote yule maana yake alitoroka kazini.Hizo Taarifa ambazo zimetolewa kuwa Israel amesimamishwa na Viongozi wa Yanga kwasababu anahusishwa na kuuza mechi,Kwanza siyo za kweli kabisa.Kwasababu Mara Baada ya mchezo wetu dhidi ya Simba pale Meje Isamuhyo ambao tulitoa sare,Bado mchezaji Israel aliendelea kucheza mechi zilizofuata.

Mechi ya mwisho ya Israel Mwenda kucheza akiwa na jezi ya Yanga ilikuwa ni dhidi ya Namungo FC.Baada ya hapo Israel hakuonekana tena kambini hadi leo hii.Yanga ni taasisi ambayo inaongozwa Kwa kufuata weredi,K**a klabu tuliamwandika barua mara mbili Israel na Viongozi walimpigia sana simu ila mchezaji hakutoa ushirikiano.

Mnamo July 3,2026 Mtendaji mkuu wa Klabu yetu ya Yanga Andre Ntine alimwandikia tena barua ya wito kuja kuripoti makao makuu Jangwani lakini mchezaji Bado hakutaka kutii wito,Hivyo wachambuzi wanapotaka kutoa habari za Israel Mwenda wanapaswa kujua kuwa Yanga haiwezi kumlipa mshahara mfanyakazi ambaye hayupo kazini Kwa utoro.

Yanga hawezi kumzurumu mchezaji haki yake ya mshahara msimu uliopita walikuwa wachezaji watatu k**a Yao Koausi Attohoula,, Dickson Job,, Clement Mzize wote hawa walikuwa majeruhi Kwa muda mrefu na k**a Job na Mzize waliukosa takribani 90% ya msimu uliopita Kwa majeraha lakini klabu iliwaendelea kuwa lipa stahiki zao Kwa wakati kwasababu idara zote za klabu zilikuwa na ripoti yao.

K**a Israel Mwenda alikuwa na changamoto ya kiafya au kifamilia Uongozi wake anaujua wapi alipaswa kufikisha matatizo yake lakini mchezaji alitoroka kambini,Sisi k**a Yanga hatuna shida naye kwasababu Bado ni mchezaji wetu ,Tumemskia Baba yake mzazi leo kuwa Israel Mwenda yupo Dar es salaam,Hivyo tunamwomba aje Makao makuu au aendekambini Avic Town ili tujue tatizo lake ni lipi.

πŸ—£οΈALI KAMWE.

πŽπ…π…πˆπ‚πˆπ€π‹: Klabu ya Simba SC imemtambulisha rasmi beki wa kati, Ibrahim Nindi k**a mchezaji mpya klabuni hapo akirejea kw...
19/08/2026

πŽπ…π…πˆπ‚πˆπ€π‹: Klabu ya Simba SC imemtambulisha rasmi beki wa kati, Ibrahim Nindi k**a mchezaji mpya klabuni hapo akirejea kwa Wekundu hao wa Msimbazi akitokea Singida Black Stars.

Nindi (19) ambaye alipita kwenye timu ya vijana ya Simba SC kabla ya kutimkia Mashujaa, KMC na Singida Black Stars amesaini mkataba wa miaka miwili.

MUHINDI WA SIMBA NA MWENZIE WAHOJIWA NA POLISI.Taarifa za uhakika zinasema anayedaiwa kuwa Mwanachama wa Simba SC ambaye...
18/08/2026

MUHINDI WA SIMBA NA MWENZIE WAHOJIWA NA POLISI.

Taarifa za uhakika zinasema anayedaiwa kuwa Mwanachama wa Simba SC ambaye anajulikana k**a β€œMhindi wa Simba” anashikiriwa na Polisi kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo kuichafua biashara ya Kampuni ya JAYRUTTY ambayo ni mzabuni wa klabu ya Simba.

Siku za karibuni Mhindi wa Simba na wenzie wamekuwa wakiishutumu Kampuni ya JAYRUTTY kuwa haina uwezo wala sifa ya kuwa Mzabuni wa klabu hiyo namba 1 Tanzania, hali inayotafsiriwa kuchafua biashara ya Kampuni hiyo ya kizawa.

Taarifa zaidi zinasema mtu mmoja (slide ya 3) anatafutwa na Polisi na inasemekana amekimbia sehemu kusikojulikana na Polisi wanamsaka bado.

BIN KAZUMARI MTIPA (Voice of the Voiceless)

SAKATA LA ISRAEL MWENDA Vs YANGA SC Watu wanajiuliza Israel Patrick Mwenda yuwapi? Mbona hakutambulishwa miongoni mwa wa...
18/08/2026

SAKATA LA ISRAEL MWENDA Vs YANGA SC

Watu wanajiuliza Israel Patrick Mwenda yuwapi? Mbona hakutambulishwa miongoni mwa wachezaji takribani 35 sasa ambao Mabingwa wa nchi wamewatangaza?

Kwanza Israel Patrick Mwenda ni mchezaji wa Yanga mwenye mkataba wa miaka 2, yani mkataba wake utaisha msimu wa 2027-2028.

Pili, inadaiwa yapata miezi miwili sasa Israel alishutumiwa kupokea pesa na kutaka β€œKuuza” mechi kutoka kwa timu moja ya Dar es Salaam.

Tatu, alipokea barua kutoka klabuni ikimuelekeza kusimama kazi ili kupisha tuhuma hizo nzito dhidi yake, kitu ambacho alikitii na ameendelea kutii.

Nne, tangu ashutumiwe hajaingiziwa mshahara wake kwa miezi hiyo 2.

Tano, klabu imemuandikia kumtaka arejee kambini na ikimuulizia kwanini haendi kambini.

Sita, mchezaji anasema kwakuwa alituhumiwa β€œKuuza” ni vyema akaandikiwa barua inayomsafisha na tuhuma zile nzito manake jamii inazifahamu. Hajaandikiwa barua ambayo inasema nini matokeo ya uchunguzi na yeye amekutwa na hatia au hapana, k**a hana hatia ni vyema klabu ikamuomba msamaha na kumtaka arejee kambini, sio k**a ilivyo sasa ambapo ana andikiwa barua tu kumuulizia alipo na kwanini haingii kambini.

Saba, mchezaji anasema bila ya barua inayomuelezea hatima ya zile tuhuma hawezi kurudi, wenzie, wafanyakazi na mashabiki watamchukuliaje, atawaangaliaje?

Nane, msimamo wa klabu mpaka sasa unaonekana ni kutomlipa mshahara kwakuwa hayupo kazini.

Kwa mujibu wa mtoa habari jana Rais wa klabu ameongea na Baba wa mchezaji na amekiri tuhuma kwa mchezaji, uchunguzi haujamkuta na hatia, kweli hajalipwa mishahara miezi 2, hawawezi kumlipa mfanyakazi ambaye hayupo kazini, arudi kazini alipwe.


K**a alituhumiwa na kusimamishwa kazi alipaswa kulipwa mshahara wake wote kwa mujibu wa sheria za kazi, kutomlipa mshahara ni makosa, anaishije huyu ana familia na kazi yake soka?

K**a aliandikiwa barua ya tuhuma na kusimamishwa, k**a hajakutwa na hatia, kwanini asiandikiwe barua ya kusema hatima ya uchunguzi na kumuomba msamaha ikimtaka arudi kundini ili kuweka rekodi zake sawasawa k**a mfanyakazi. Picha ya mwanzo, huo ndiyo mtazamo wa wengi kwa Israel Patrick Mwenda kwa sasa

BIN KAZUMARI MTIPA (Voice of the voiceless)

Address

Bugweto
Shinyanga
26

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when PANDA SPORT posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to PANDA SPORT:

Shortcuts

Share

Category