Ntenga Secondary School

Ntenga Secondary School

Comments

NINA PAKUMBUKA SANA HAPO BY Timotheo Mngulu
Mungu uwalinde wanafunzi wote pamoja na walimu wao
Duh miaka insogea umri unaenda tumetoka hapo 2010 nawakumbuka masela zangu popote mlipo salami nyingi kutoka kwa Fadhili a.k.a f.a
Je, unawaza nini?
Hellow! Intake ya 2008-2011
Mpooooooh???
Kayaaaaa
I WIIL NEVER FORGET
Kaya nikaya
Kiukwel shule imependeza
Efkey

A page for Ntenga Secondary Students

Operating as usual

11/06/2020

#TBT Kumbukizi toka mkataba: Pichani wa Kwanza Meza kuu toka kushoto, Aliewai kuwa waziri wa fedha kipindi hicho Mh. Daniel Yona Nzira akikabidhi cheti kwa Moja ya wanafunzi wetu katika sherehe Yao maalumu ya kuwaaga wahitimu elimu ya form four Mwaka 1999. Wapili toka kushoto aliewai kua Mwalimu Mkuu Wa shule ya Ntenga kwa wakati huo. Ndg *Kayus Mduda
#Nteseco

20/03/2020

Moja Kati ya wanafunzi wetu kwenye halfa mbali mbali.. Tunatoa rai kufwatilia taarifa na maelekezo Juu ya kujilinda na Huu ugonjwa wa uliopo Corona #COVID19 Tunawatakia mapumziko Mema. Stay safe!

[12/02/19]   We have now reached 700 Likes on our page.. Thank you all for your LIKES 🙏🏾 #Nteseco

[07/12/19]   We have recently reached over 600 likes on our Ntenga Secondary School page! Thank you to everyone who likes our page and help us reach over 600 likes. With your help we would love you to help us reach the next milestone of 700.. Ahsanteni sana. #Nteseco

14/06/2019

Shule yetu pendwa..
14June2019

21/04/2019

TANZIA

Tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya msiba wa Ndungu, Rafiki, na dada yetu mpendwa Lightness mgallah. (Form four '09) Tunatoa pole kwa Familia na wote walioguswa na msiba huu. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehem mahala Pema peponi..

We were so blessed to have someone like you in our community, you will be dearly missed🌹. RIP Lightness 🕯

27/01/2019

HakiElimu

Unaiwezeshaje shule iliyo karibu na wewe kuwa na mazingira rafiki kwa watoto wenye mahitaji maalum?

05/12/2018

Comment hapa mwaka uliohitimu kidato cha nne Ntenga Sec ukutane na marafiki zako wa kipindi hicho #classmates mjikumbushe matukio, visa na mikasa mabali mbali ya kusisimua wakati huo katika maisha ya shule
#unforgetablemoments
#schoollifemate

13/11/2018

Wangapi walitumia hii kitu na kutengeneza hii kitu enzi za shule???
#UnforgetableMoments

09/11/2018

HakiElimu

Tutafakari na hili

Je wanafunzi wenye mahitaji maalum wanajifunza k**a wanafunzi wengine katika shule zetu nchini? Karibu tutafakari katika Video hii yenye dakika moja ikiwa ni sehemu ya kampeni yetu mpya inayoangalia Elimu Jumuishi. #JeTupoPamojaKweli

04/11/2018

Ntenga Secondary School

KILA LA KHERI WADOGO ZETU - KIDATO CHA NNE (NSS)
Tunawatakia mtihani mwema vijana wetu wa kidato cha nne wa Ntenga Secondary school (NSS) pamoja na shule nyingine kote nchini katika ngwe hii muhimu sana ya kulivuka daraja hili ambalo ndio haswa daraja kuu la elimu ya Tanzania, mara nyingi ukifanikiwa kuvuka salama hapa kuna nuru ya kufika mbali zaidi kitaaluma.
Mwenyezi mungu akawape wepesi wa kuyakumbuka yote mliyojifunza na kujibu kwa ufasaha na ufanisi mkubwa pindi muwapo katika chumba cha mtihani, hali kadhalika awaondolee homa ya mtihani (examination fiver) pamoja na kuwapunguzia kujiamini kulikopitiliza (over confidence) ili mpate kufaulu vyema.
NO HANDS UP!!! wana NSS...

04/11/2018

Ntenga Secondary School

Tunatoa shukrani za dhati kwa wana NSS na wadau wote mlioshiriki vyema katika page yetu hatimaye tumefikisha likes 500. Tuendelee kupambana na kuweka mikakati madhubuti kupitia page hii kuipeleka shule yetu mama mbali zaidi na kuinua maendeleo ya nyumbani kwetu..
#Mkataakwaomtumwa😀😁😁
Hongereni na Ahsanteni sana
NO HANDS UP!!!

A page for Ntenga Secondary Students

04/11/2018

KILA LA KHERI WADOGO ZETU - KIDATO CHA NNE (NSS)
Tunawatakia mtihani mwema vijana wetu wa kidato cha nne wa Ntenga Secondary school (NSS) pamoja na shule nyingine kote nchini katika ngwe hii muhimu sana ya kulivuka daraja hili ambalo ndio haswa daraja kuu la elimu ya Tanzania, mara nyingi ukifanikiwa kuvuka salama hapa kuna nuru ya kufika mbali zaidi kitaaluma.
Mwenyezi mungu akawape wepesi wa kuyakumbuka yote mliyojifunza na kujibu kwa ufasaha na ufanisi mkubwa pindi muwapo katika chumba cha mtihani, hali kadhalika awaondolee homa ya mtihani (examination fiver) pamoja na kuwapunguzia kujiamini kulikopitiliza (over confidence) ili mpate kufaulu vyema.
NO HANDS UP!!! wana NSS...

12/08/2018

TUJITATHMINI KIDOGO🇹🇿️🇹🇿️🇹🇿️

HEBU!! TUCHANGANUE MAWAZO KIDOGO HAPA..
Dira ya Tanzania 2025 inajielekeza katika kuwezesha jamii yote kupata elimu ya msingi, kuondoa ujinga na kufikia elimu na mafunzo bora ya ngazi ya kati, kwa kuwajengea stadi na maarifa stahiki. Kwamba, elimu ni wakala, nyenzo na mkakati muhimu wa kubadili mitazamo na fikra za watu, ili kujenga taifa la wasomi, waliopandikizwa maarifa kwa ufanisi na umahiri wenye kulenga mahitaji ya ushindani kutatua changamoto zinazolikabili taifa.

Hivyo, mfumo wa elimu umeumbwa kulenga ubora; mbiu ya kipaumbele ikihimiza sayansi, hesabu na teknolojia kuanzia ngazi za chini kwa watoto wote wa kuanzia umri wa miaka 6. Sayansi na hesabu zinapewa umuhimu kwa kuzingatia uhitaji wa soko la teknolojia mpya, bila kupoteza mwelekeo katika mambo ya kijamii. Jamii maskini zikihakikishiwa kupatiwa elimu bora ya awali kwa malengo yanayoilenga elimu ya msingi na sekondari kuwa lazima kwa kila mtanzania k**a kiwango cha awali ambacho kila mwananchi anastahiki kupata pasi na kujali matabaka ya kidini, kabila, rangi wala uwezo wa kifedha. Rasilimali na mahitaji ya elimu yakiongezwa na kusimamiwa vizuri.Ufadhili wa kutosha kuanzia elimu ya msingi mpaka vyuo vikuu naimani malengo yatafikiwa . Katika Elimu ya awali
Mikakati imetajwa, Miongoni mwake ni kufutwa kwa malipo yote kuanzia kindagateni mpaka kidato cha nne, ingawaji bado zipo changamoto nyingi katika hili lakini limesaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza morali ya vijana wengi kuendelea na masomo hasa wanaotoka katika kaya masikini, hali kadhali mpango wa kupunguzwa kwa kiwango - wezeshi gharama za elimu na mafunzo ya chuo kikuu; kuhimiza mahusiano miongoni mwa wadau na taasisi na sekta binafsi bado ni nyezo kuu za elimu nchini japo sera ya elimu bure imetengeneza mazingira yasiyo rafiki kwa jamii kushiriki katika utoaji wa elimu wakati sera hii bado inanonekana haijaweza kujitegemea ipasavyo, budget ni ndogo haitoshelezi wala haiwawezeshi wadau kujitoa kimasomaso kufikisha mpango panapostahili.
Mikakati na mipango ya kurekebisha mitaala kwa kulenga zaidi sayansi na teknolojia; kuhimiza uwiano kati ya vifaa na watumishi/wafanyakazi (walimu); kuhimiza sekta binafsi kuwekeza elimu katika jamii za chini ili kuchota uwezo wao wa ubunifu; kuanzisha program maalumu zitakazolenga kaya maskini hasa katika mustakabadhi wa upatikanaji wa elimu, n.k ni mipango thabiti isiyohitaji kubezwa.

Sera ya Elimu na Mafunzo haipo nyuma. Imebeba zaidi ya sentensi 125 za kisera kuhusu mfumo wa elimu, usawa wa kufikia, usimamizi wa sekta, mfumo rasmi wa elimu na mafunzo kwa ngazi zote, mitaala na mitihani, mafunzo ya ufundi stadi, elimu ya kati, elimu isiyo rasmi, na ugharamiaji mafunzo.

Sera inasema malengo ya pamoja ya elimu ni kuendeleza wasifu kutegemeana na utu wa mtu (integrative personalities); kuendeleza na kufurahia utamaduni wa taifa na Katiba ya nchi; kujenga taifa la watu wenye kupenda kujifunza na kutumia stadi na maarifa waliyopata kuboresha hali za maisha yao; kuwajengea kujiamini, na akili ya udadisi, na mtazamo wa kulenga maendeleo; kuwapa elimu inayoendana na mabadiliko ya dunia ili kuweza kukabili changamoto mbalimbali; kuhimiza kupendana, tabia ya kuheshimu kazi ya aina yeyote na kuongeza uzalishaji; kupandikiza tabia ya maadili, umoja wa kitaifa,mahusiano ya kimataifa, amani na haki; kusimamia taifa na matumizi ya mazingira, na kuboresha ufanisi wa elimu katika soko la ajira na mafunzo ya ufundi stadi. Je tunaenda sawa katika malengo haya ya elimu?

Shule za sekondari kwa kidato cha kwanza mpaka cha nne zina changamoto kubwa. Kwa mtazamo wangu, hakuna hatua ngumu katika maendeleo ya mtu (kibaolojia na ukuaji wa kiakili) k**a katika umri wa mwanafunzi anapoingia kidato cha kwanza mpaka cha nne. Ni hatua ya muhimu ya kielimu yenye kuweza kumsaidia mtu kujua mwelekeo wake kimaisha (kusimama au kuanguka). Kwa matokeo ya shule nyingi za serikali ikiwemo Ntenga secondary k**a miongoni mwa shule za kata lakini pia hata shule kongwe bado zinaonekana kuvurunda katika zama hizi wote tulishuhudia matokeo ya kidato cha sita katika shule kongwe ya wasichana ya Jangwani iliyopo jijini Dar es salaam, malengo mahsusi ya elimu yanasiginwa kwa mtaji huu!

Tanzania ilikuwa na Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) 2002 ,2006, na Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) 2004 &2008. Mipango hii ililenga pamoja na malengo mengine, kuongeza uandikishaji shule za msingi na wanaojiunga na sekondari. Mafanikio makubwa yameonekana. Madarasa yamejengwa, na kumekuwepo jitihada za kuzipatia shule walimu. Tukisuasua katika maabara na vifaa vya kutosha. Changamoto ni kubwa na hasa kwa shule za maeneo ya vijijini.

Taarifa za utafiti, zinaonyesha kwamba, kwa ujumla, mabadiliko makubwa ya kielimu yalishuhudiwa kwa miaka ya (2002 & 2006). Baada ya serikali kukwepa kwa muda mrefu, jitihada hizi ambazo zilitakiwa siku nyingi. Taarifa inasema utashi wa kisiasa wa serikali ulikuwa mfano mzuri kutoka kipindi cha pili cha utawala wa Rais Mkapa kuelekea kipindi cha utawala wa Rais Kikwete, Waziri Mkuu Lowasa na Waziri Sitta (Magreth) walionyesha mafanikio.

Idadi ya uandikishaji imeongezeka katika shule za msingi hivyo kulazimisha kupanua elimu ya sekondari. Uhitaji wa mikakati sahihi ya kisera utaonekana ili kutoa mwongozo katika vipaumbele, matumizi ya rasilimali na utekelezaji wake. Ushauri ukitolewa katika maeneo muhimu matano ambayo yalionyesha changamoto kubwa, ikiwepo serikali ionyeshe malengo mahsusi katika elimu ya sekondari; kulenga katika matokeo na si idadi; walimu na miundombinu sahihi kwa walimu; kipimio cha mafanikio; mitihani inalenga kupima nini; na, lugha ya kufundishia; kiingereza kutumika katika elimu ya msingi, na lugha zingine za kimataifa kufundishwa sekondari, (Suleman Sumra & Rakesh Rajan, (2006), Working Paper No. 4, Secondary Education Tanzania: Key Policy Challenges, HakiElimu).

Tunajifunza kwamba maisha ya mtu yana hatua ambazo zimefuatana na zinahusisha mawazo, tabia, mihemko na mahusiano. Kila hatua hudumu kati ya miaka 2 na 5; ambapo kuna mambo ambayo ni lazima mtu uyamudu katika hatua husika. Chochote ambacho mtu atashindwa kukimudu katika hatua ya umri husika, baadaye huwa ni changamoto kubwa sana ya kimaisha kwa mtu, katika umri na hatua ambayo si wakati wake (Herbert Harris , (2004), The 12 Universal Laws of Success).

Tunapoiangalia miaka 20 -25, ya kila hatua ya mwanadamu, mambo yafuatayo ni lazima yafikiwe. Moja, ni elimu (education),tangu miaka 0 & 25. Mbili, ni hisia na uzoefu (feeling & experience), miaka26 &35. Tatu, nguvu (power) kufanya mambo kutokea, miaka 40-60 au 50&75. Nne, umilele (immortality) kutathimini mafanikio na maanguko, miaka 60 &75, au 75 d ukifanikiwa kufika.
Ni katika umri wa miaka 0 & 25 wa maisha ya mwanadamu ambapo mtu anatakiwa kuwa na uhakika kuhusu elimu yake (awali, msingi, sekondari, kati na chuo kikuu). Ndani ya hatua hii mwanadamu anajifunza kanuni na misingi ya maisha. Unajenga na kupokea mifumo ya maisha. Unapata maelekezo kwa kusoma, kufundishwa, kuandika, kuhesabu, kuwaza ki-maantiki, na kufanya maamuzi. Katika hatua ya elimu unajenga msingi wa mawazo, tabia, mihemko na mahusiano ambapo maisha yako yote mengine yataegemea. Katika hatua ya elimu mtu anajenga tabia ya msingi ya kujitambua, mtazamo wake kuhusu wengine, na dunia kwa ujumla. Katika hatua hii mtu anajenga kuajiamini au hofu; imani au mashaka; ujinga au uelewa; mtazamo chanya au hasi; utegemezi au kujitegemea.

Utegemezi wa elimu toka kwa watu wengine ni changamoto ya hatua ya elimu. Mhusika anatambulika k**a mtoto mwanafunzi hivyo hana mchango mkubwa katika hatua hii. Hivyo, mawazo, tabia, mihemko, uzoefu, na mitazamo chanya na hasi ya wazazi wake, walimu wake, viongozi wake, au watu wa kuigwa katika jamii humjenga mhusika katika mitazamo chanya au hasi ya umri wake wa utoto na utu-uzima-mchanga.

Katika hatua hii k**a msingi haukujengwa sawasawa, ni lazima, katika umri fulani wa maisha ya mhusika, mipasuko itaonekana. Mtu hatakuwa na amani, afya bora, furaha, wala hatajikubali. Hataipenda serikali. Anaweza kuwa katili kwa kila kitu. Lakini endapo msingi huu utajengwa kwa dhati, upendo, uaminifu, imani, nidhamu, ujasiri, huruma na mitazamo yote chanya; mtu katika hatua hii atakuwa ameandaliwa vizuri kushuhudia hatua zingine tatu za maisha yake kwa mafanikio makubwa. Hali ikoje? Tunajenga watu 141 kwa daraja sifuri dhidi ya wanafunzi 252 katika Hatua ya Elimu, je tunalenga kweli Dira ya Tanzania 2025 na malengo ya Sera ya Elimu na Mafunzo?

Mosi, tunaporejea kuitafakari Dira ya Tanzania 2025 kwamba elimu ni wakala, nyenzo na mkakati muhimu wa kubadili mitazamo na fikra za watu, ili kujenga taifa la wasomi, waliopandikizwa maarifa kwa ufanisi na umahiri wenye kulenga mahitaji ya ushindani kutatua changamoto zinazolikabili taifa. Pili, tunaporejea kuangalia malengo ya Sera ya Elimu na Mafunzo mathalani kujenga taifa la watu wenye kupenda kujifunza/kujieleimsha na kutumia stadi na maarifa waliyopata kuboresha hali ya maisha; kuwajengea kujiamini, na akili yenye kujiuliza maswali na kutafuta majibu sahihi, na mtazamo wa kulenga maendeleo; kuwapa elimu inayoendana na mabadiliko ya dunia ili kuweza kukabili changamoto mbalimbali. Je ni kwa hali hii ya wanafunzi 141 kupata daraja sifuri katika shule moja?

Napendekeza Idara Maalumu za Ushauri Shuleni ili zifanye kazi ya kushauri na kumsaidia mwanafunzi kwa kina katika Hatua ya Elimu, tofauti na sasa mwalimu ndiyo anakuwa k**a mshauri. Napendekeza kiwepo kitengo maalum katika kila shule, kitengo ambacho kitakuwa na wafanyakazi wenye elimu nzuri ya ushauri, stadi za kazi, saikolojia na elimu ya ujasiriamali, wakifanya kazi ya kumjenga mwanafunzi kufikia maono yake zaidi ya mitihani ya darasani. Kwamba, katika ratiba ya masomo ya shule husika, iwe ni mkakati wa serikali kwamba katika siku maalumu, darasa fulani litaingia katika chumba maalumu, wanafunzi wa darasa husika na walimu mahiri wa maeneo tajwa hapo juu wanaingia na kufanya majadiliano ya kawaida, urafiki na mazingira au mifano halisi ya mada ambayo itawekwa na kujadiliwa kwa pamoja ili kuibua ubunifu, na kujua mitazamo chanya, vipawa na mienendo ya wanafunzi.

Idara Maalumu za Ushauri Shuleni zifanye kazi ya kujenga nidhamu na maadili ya wanafunzi kwa ufanisi, kwa kulenga kuthibiti tabia za matumizi ya simu yasiyo na mipaka; uvaaji wa nguo wenye kichefuchefu; kuwajengea wanafunzi uelekeo sahihi wa vipawa na ubunifu wao hata k**a ni katika uimbaji, iwe ni uimbaji wenye faida kwa maisha ya kijana husika hata katika hatua zingine za maisha, tofauti na sasa kila kijana wa sekondari analazimisha kuchana mistari ya bongo fleva', ambayo baada ya umri fulani, muhusika hopotea katika ramani ya muziki.

Huu ni uchokozi. Mjadala unaendelea. Mawazo yako ni muhimu sana kuhusu Idara Maalumu za Ushauri Shuleni!

Location

Category

Telephone

Address

Ntenga
Same
BOX 263
Other Public Schools in Same (show all)
St Joseph VTC - SAME St Joseph VTC - SAME
Same, PO BOX 8

Chuo cha ufundi cha St Joseph VTC Same Kinawaandaa vijana kwa ustadi wa Maisha yao Umeme, Makenika, Useremala, Gereji, Mafunzo ya hoteli, Udereva na Computer.