04/11/2022
Tiwa moyo na hii tena katika Jina la Yesu ...
*NGUVU YA KIBALI KUTOKA KWA BWANA*
--------------------------
Sikia,
Kibali ni kitu cha ajabu sana,,, tena zaidi sana kiwe ni kibali Kutoka kwa BWANA mwenyewe!---aisee utaishi wa raha sana!!!
Somo hili ni pana mno ila LEO Nataka nikutazamishe jambo moja juu ya kibali hiki kinachotoka kwa Bwana.
Iko hivi ,,,,
""" _*ILE KWAMBA UNACHO KIBALI KUTOKA KWA BWANA,, HAIMAANISHI KILA MTU ATAKUKUBALI*_ """".
Umenielewa ninachosema????
---usije ukasema mbona natukanwa , nanenwa vibaya ,,,
Mbona watu hawa hawanikubali, wananichukia tu ,,,Mbona kazi yangu haipendwi na marafiki zangu hawa,,,Mbona ! Mbona! Mbona! Mbona hivi na vile ,,, basi mimi Sina Kibali!!!
LA HASHA!!!
Mimi nakwambia kibali unacho,,,ila hujajua sifa za kibali cha Mungu!
Moja ya sifa hizo ndio ambayo naieleza hapa,,,,,
Kuwa
""" *SI KILA MTU ATAKUKUBALI ,PALE MUNGU AKIKUKUBALI* !!!""""
Unapaswa uelewe hilo,,,
Haya mazingira yalimkuta Mwokozi wetu YESU Kristo
Ona...
"" _Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, AKIMPENDEZA MUNGU NA WANADAMU_ """
[ Luka 2: 52 ]
Ona hapo,,,↑↑↑
Swali !
Je, k**a Yesu aliwapendeza wanadamu *WOTE* (maana alipata kibali kwa Mungu),,, *NI WANADAMU GANI TENA AMBAO* walimpiga, walimtukana, walimsengenya na hata kumuua ❓❓❓❓❓
..basi tambua kuwa pamoja na kuwa alipewa kibali kwa Bwana,,,lakini *SI_WOTE WALIOMKUBALI*!!!!--------wapo walioendelea kumpinga katika mambo yake yote---hata nduguze walithubutu kumpinga!
Jambo jema ni hili,
Kibali cha Bwana kinapokuwa juu yako *UTAFANIKIWA KATIKA MAMBO YAKO YOTE*!(siyo mambo baadhi , ni YOTE)---umenisikia???????
haijalishi watu 100 watakupinga juu ya hatua yako moja unayotaka kuipiga ,,,,lakini BWANA ATAKUPA KIBALI kwa mtu mmoja TU atakayekuwezesha KUIFANIKISHA HATUA YAKO HIYO!!!!
Watakupinga wakitarajia kukuona umekwama ,,,chaajabu wanakuona UMEVUKA ng'ambo!!!
--- *wanajiuliza UMEVUKAVUKAJE hapo,,??????,,,*.ukiwasikia unawajibu """" NINAYE MTOA KIBALI---- ndiye Mungu Mkuu !
Oooooooh JESUS! JESUS! JESUS!
*IMO NGUVU KUBWA NDANI YA KIBALI CHA BWANA*,,,,----asikwambie Mtu aisee .
©Mwl. Maswaga, A.C
Njombe, Tanzania~ Now!
🙏🏼🙏🏼🙏🏼