DIT Mwanza Campus

DIT Mwanza Campus Dar es Salaam Institute of Technology Mwanza Campus,
P.O.Box 2525,
Mwanza.

Dirisha la Udahili kwa Ngazi ya Degree lipo wazi
10/07/2026

Dirisha la Udahili kwa Ngazi ya Degree lipo wazi

08/07/2026

MSIGWA AIPONGEZA DIT, AHIMIZA UBORESHAJI NA UZALISHAJI WA BAJAJI ZA UMEME KWA KIWANGO CHA KIBIASHARA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa, leo tarehe 8,Julai,2026 ametembelea banda la Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), ambapo amepongeza bunifu mbalimbali zinazotengenezwa na taasisi hiyo, hususan bajaji ya umeme iliyobuniwa na wanafunzi kwa kushirikiana na walimu wao.

MBUNGE WA VITI MAALUM  MHE. ASHA FERUZ ATEMBELEA BANDA LA DIT, APONGEZA BUNIFU ZA TEKNOLOJIAMbunge wa Viti Maalum anayew...
07/07/2026

MBUNGE WA VITI MAALUM MHE. ASHA FERUZ ATEMBELEA BANDA LA DIT, APONGEZA BUNIFU ZA TEKNOLOJIA

Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu, Mhe. Asha Feruz, ametembelea banda la Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Akiwa katika banda hilo, Mhe. Feruz amepata fursa ya kujionea bunifu mbalimbali za teknolojia pamoja na bidhaa zinazotengenezwa na DIT, ambazo zinalenga kutoa suluhisho kwa changamoto za kijamii na kuchochea maendeleo ya viwanda nchini.

Mhe. Feruz ameipongeza DIT kwa ubunifu, ubora wa bidhaa na mchango wake katika kuandaa wataalamu wenye ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira, huku akihimiza taasisi hiyo kuendelea kuimarisha tafiti na ubunifu unaochochea maendeleo ya Taifa.

Bidha za Bora kabisa za Ngozi halisia kutoka DIT  Kampasi ya Mwanza
07/07/2026

Bidha za Bora kabisa za Ngozi halisia kutoka DIT Kampasi ya Mwanza

KATIBU MTENDAJI NACTVET  ATEMBELEA BANDA LA DIT, APONGEZA BUNIFU NA UBORA WA BIDHAA ZAKE.Katibu Mtendaji wa Baraza la Ta...
07/07/2026

KATIBU MTENDAJI NACTVET ATEMBELEA BANDA LA DIT, APONGEZA BUNIFU NA UBORA WA BIDHAA ZAKE.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), Dkt. Mwajuma Ibrahim Lingwanda, leo tarehe 7,Julai,2026, ametembelea banda la Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika banda hilo, Dkt. Lingwanda amejionea bunifu mbalimbali za teknolojia pamoja na bidhaa zinazotengenezwa na DIT na kupongeza Taasisi kwa kuendelea kuendeleza ubunifu unaozingatia ubora na kutoa suluhisho kwa mahitaji ya jamii na sekta ya viwanda.

Amesema mafanikio hayo yanaonesha uwezo wa DIT katika kuzalisha wataalamu wenye ujuzi na bunifu zinazochangia maendeleo ya teknolojia, viwanda na uchumi wa Taifa.

Bado siku 3 Dirisha la udahili awamu ya kwanza lifugwe
07/07/2026

Bado siku 3 Dirisha la udahili awamu ya kwanza lifugwe

07/07/2026
04/07/2026

DIT KAMPASI YA MWANZA TUNASHIRIKI MAONYESHO YA 50 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM (DITF) SABASABA,
KARIBU TUKUHUDUMIE TUPO VIWANJA VYA MWL JULIUS NYERERE BARABARA YA KILWA.

PROF. EZEKIEL AMRI ATEMBELEA BANDA LA DIT DITF 2026Naibu Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) anayeshughuli...
03/07/2026

PROF. EZEKIEL AMRI ATEMBELEA BANDA LA DIT DITF 2026

Naibu Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam, Prof. Ezekiel Amri, leo tarehe 3 Julai 2026 ametembelea banda la DIT katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF).

Ziara hiyo imefanyika sambamba na uzinduzi rasmi wa maonesho hayo uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Daniel Francisco Chapo, akiwa mgeni rasmi, pamoja na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akiwa bandani hapo, Prof. Amri amekagua bunifu na teknolojia mbalimbali zinazooneshwa na DIT, na kuwapongeza wabunifu pamoja na watalaamu wa DIT kwa kuendelea kubuni suluhisho zinazochangia maendeleo ya viwanda na kutatua changamoto za kijamii.

Pia amewataka kuendelea kuboresha ubora wa bunifu, kuziunganisha na mahitaji ya soko, na kuhakikisha zinawanufaisha wananchi na sekta za uzalishaji nchini.

Bunifu za DIT zinaendelea kuvutia maelfu ya wananchi katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba 2026.Tembel...
02/07/2026

Bunifu za DIT zinaendelea kuvutia maelfu ya wananchi katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba 2026.

Tembelea banda la DIT ujionee teknolojia na ubunifu unaotoa suluhisho kwa changamoto za kijamii na kuchochea maendeleo ya viwanda na uchumi.

Address

ILEMELA, AIRPORT Road
Mwanza

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30
Saturday 07:30 - 15:30
Sunday 07:30 - 15:30

Telephone

+255738204060

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when DIT Mwanza Campus posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to DIT Mwanza Campus:

Shortcuts

Share