BAMC saut Tanzania 2012 to 2015

BAMC saut Tanzania 2012 to 2015 Page hii maalumu kwa HABARI, MATUKIO, MAKALA na VIPINDI vinavyofanywa na BAMC pamoja na MEDIA nyingine Duniani. Pia NOTES na MATANGAZO yanapatikana HAPA.

Rais Magufuli ameamua kuwasamehe Familia ya Nguza Viking(Babu Seya) na Johnson Nguza(Papii Kocha) kuanzia leo.
09/12/2017

Rais Magufuli ameamua kuwasamehe Familia ya Nguza Viking(Babu Seya) na Johnson Nguza(Papii Kocha) kuanzia leo.

ARUSHA: Mazungumzo mapya kuhusu mgogoro wa kisiasa wa Burundi yameanza jana na kuongozwa na Rais wa zamani wa Tanzania, ...
28/11/2017

ARUSHA: Mazungumzo mapya kuhusu mgogoro wa kisiasa wa Burundi yameanza jana na kuongozwa na Rais wa zamani wa Tanzania, Benjamin Mkapa.
-
Mazungumzo hayo mapya yatakua ni yenye maamuzi, kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na timu ya Mwezeshaji.
-
Mazungumo haya yanatarajiwa kudumu kwa wiki 2 ili kujaribu kutafuta suluhu ya mgogoro huo uliibuka baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia yake ya kuwania muhula wa tatu wa urais mwaka 2015.

RUVUMA: Aliyekuwa Mbunge wa Songea Mjini Leonidas Gama azikwa kijijini kwao Likuyu Fusi. Spika wa Bunge Job Ndungai ahud...
27/11/2017

RUVUMA: Aliyekuwa Mbunge wa Songea Mjini Leonidas Gama azikwa kijijini kwao Likuyu Fusi. Spika wa Bunge Job Ndungai ahudhuria mazishi.
-
Gama alifariki dunia katika Hospitali ya Misheni ya Peramiho alikopelekwa baada ya hali yake kubadilika gafla akiwa nyumbani kwake.
-
Pichani ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha maombolezo.

ZIMBABWE: Emmerson Mnangagwa ameapishwa rasmi kuwa rais mpya, ahutubia na kuahidi ajira. Rais wa Zambia na Botswana wahu...
24/11/2017

ZIMBABWE: Emmerson Mnangagwa ameapishwa rasmi kuwa rais mpya, ahutubia na kuahidi ajira. Rais wa Zambia na Botswana wahudhuria.
-
Kuapishwa kwa bwana Mnangagwa ni mwanzo wa zama mpya baada ya kujiuzulu kwa Robert Mugabe aliyeongoza taifa hilo kwa miaka 38. -
Changamoto kubwa anayosubiriwa aitatue ni ukosefu wa ajira ambapo takwimu zinabainisha kuwa raia wa taifa hilo kwa asilimia 90 hawana ajira.

ZIMBABWE: Aliyekuwa Makamu wa Rais, Emmerson Mnangagwa huenda akaapishwa kuwa Rais wa mpito leo au kesho. Ataongoza hadi...
22/11/2017

ZIMBABWE: Aliyekuwa Makamu wa Rais, Emmerson Mnangagwa huenda akaapishwa kuwa Rais wa mpito leo au kesho. Ataongoza hadi Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka 2018.
-
Mugabe aliamua kujiuzulu kabla ya Bunge la nchi hiyo halijaanza mchakato wa kumuondoa kwa kura ya kutokuwa na imani naye.
-
Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi kuhusu masharti aliyoyaweka Rais aliyejiuzulu, Robert Mugabe ingawa taarifa za awali ziliarifu kuwa alitaka kupewa ulinzi wa kudumu akiwa nje ya kiti cha Urais.

ZIMBABWE: Spika wa Bunge, Jacob Mudenda amesema Rais Robert Mugabe amejiuzulu kabla ya bunge kuanza zoezi la kumpigia ku...
21/11/2017

ZIMBABWE: Spika wa Bunge, Jacob Mudenda amesema Rais Robert Mugabe amejiuzulu kabla ya bunge kuanza zoezi la kumpigia kura ya kutokuwa na imani nae (impeachment).
-
Spika amesoma barua ya Mugabe bungeni kuhusu uamuzi wake huo na kusababisha bunge zima kulipuka kwa furaha.
-
Shangwe na nderemo zinaendelea jioni hii katika mitaa mbalimbali Jijini Harare nchini humo.

ZIMBABWE: Rais Robert Mugabe amekataa kujiuzulu k**a ilivyotarajiwa katika hotuba yake usiku wa kuamkia leo- Asema ataon...
20/11/2017

ZIMBABWE: Rais Robert Mugabe amekataa kujiuzulu k**a ilivyotarajiwa katika hotuba yake usiku wa kuamkia leo
-
Asema ataongoza kikao cha ZANU-PF mwezi Desemba.Kauli yake hiyo imeiingiza Zimbabwe katika sintofahamu kubwa.
-
Kutojiuzulu kwa Rais Mugabe ni kinyume na matarajio ya raia wengi ambao walijimwaga mitaani mwishoni mwa juma lililopita kumshinikiza Mugabe mwenye umri wa miaka 93 kuachia ngazi, baada ya kuiongoza Zimbabwe kwa miaka 37.

ZIMBABWE: Kamati Kuu ya chama tawala cha ZANU-PF imepanga kukutana leo ili kupitisha maamuzi ya kumvua uanachama Rais Ro...
19/11/2017

ZIMBABWE: Kamati Kuu ya chama tawala cha ZANU-PF imepanga kukutana leo ili kupitisha maamuzi ya kumvua uanachama Rais Robert Mugabe. - Taarifa hii inakuja ikiwa ni siku chache tangu kuibuka kwa madai kuwa Rais Mugabe amegoma kujiuzulu kwa hiyari. - Endapo chama cha ZANU-PF kitamvua uanachama Rais huyo basi moja kwa moja atapoteza sifa za kuwa Rais wa Zimbabwe na kuruhusu kuanza kwa mchakato wa mabadiliko ya kiutawala nchini humo.

ZIMBABWE: Mamia ya watu wamekusanyika mjini Harare kushinikiza kujiuzulu kwa kiongozi wa Taifa hilo Rais Robert Mugabe.-...
18/11/2017

ZIMBABWE: Mamia ya watu wamekusanyika mjini Harare kushinikiza kujiuzulu kwa kiongozi wa Taifa hilo Rais Robert Mugabe.
-
Waandamanaji hao wanaungwa mkono na jeshi la nchi hiyo na wanachama wa chama tawala cha ANC.
-
Wakongwe waliopigana vita ya mapinduzi ambao walikuwa wanamuunga mkono Rais Robert Mugabe nao sasa wanasema aondoke.

KUTOKA ZIMBABWE: Rais Robert Mugabe ahudhuria sherehe za mahafali ya Chuo Kikuu Huria-Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi...
17/11/2017

KUTOKA ZIMBABWE: Rais Robert Mugabe ahudhuria sherehe za mahafali ya Chuo Kikuu Huria
-
Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi huyo kujitokeza tangu kuanza kuenea kwa taarifa kuwa Jeshi linataka kupindua Serikali yake.
-
Kwa mujibu wa chanzo ndani ya chama cha ZANU-PF zinasema kuwa chama hicho kinapanga Mkakati wa kumuondoa madarakani kiongozi huyo na k**a atakaidi kuondoka basi watamuondoa siku ya Jumanne.
-
Vikosi vya Wnajeshi na Virafu vyaendelea kurandaranda katika viunga vya Mji mkuu Harare.

KENYA: Chuo Kikuu cha Kenyatta kimefungwa kwa muda usiofahamika baada ya Wanafunzi kufanya vurugu-Walikuwa wakipinga mau...
17/11/2017

KENYA: Chuo Kikuu cha Kenyatta kimefungwa kwa muda usiofahamika baada ya Wanafunzi kufanya vurugu
-
Walikuwa wakipinga mauji ya mwanafunzi wa k**e anayedaiwa kuuawa na Madereva wa Bodaboda na mwili wake kutupwa barabarani na kuzuiwa kwa uchaguzi wa Serikali ya Wanafunzi
-
Wanafunzi hao wameamriwa kuondoka maeneo ya chuo hadi saa tatu asubuhi Ijumaa hii
-
Siku ya Jumatano, chuo hicho kilitangaza kufuta ratiba za masomo kutokana na mgomo wa wahadhiri unaoendelea

Gazeti la Serikali nchini Zimbabwe limechapisha picha kadhaa zinazomwonyesha Rais Robert Mugabe akiwa kikaoni Ikulu na M...
16/11/2017

Gazeti la Serikali nchini Zimbabwe limechapisha picha kadhaa zinazomwonyesha Rais Robert Mugabe akiwa kikaoni Ikulu na Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo, Askofu wa Kanisa Katoliki na ujumbe kutoka Afrika Kusini.
-
Bado mpaka sasa haijaelezwa kikao hicho kimejadili na kuafikiana nini.
-
Taarifa zilizopo zinadai kikao hicho huenda kikaamua hatma ya uongozi wa Rais Mugabe nchini humo.

Address

MALIMBE
Mwanza

Telephone

0655649790

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when BAMC saut Tanzania 2012 to 2015 posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to BAMC saut Tanzania 2012 to 2015:

Shortcuts

Share