Darasa Huru la Uamsho.

Darasa Huru la Uamsho. Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye ataendelea kuiishi

Hakuna kisima kinachochimbika wala shamba linalolimwa ili kuvuna amani. Amani ni zawadi kuu kutoka kwa Mola wetu, na kil...
03/12/2025

Hakuna kisima kinachochimbika wala shamba linalolimwa ili kuvuna amani.

Amani ni zawadi kuu kutoka kwa Mola wetu, na kila mmoja wetu ana wajibu wa kuilinda na kuitunza.

Kwa hiyo, na tuungane kwa imani zetu mbalimbali, tuliombee taifa letu Tanzania, ili liendelee kudumu katika amani, umoja na upendo.

Kwani Amani ya nchi ni jukumu letu sote. 🙏🏾🇹🇿

Turn from evil and do good; seek peace and pursue it - Psalm 34:14

Si vyema, wala si afya ya kiroho, kwa Wakristo kuwa na utamaduni wa kufanya ibada za maombi nyakati za usiku huku tukitu...
27/09/2025

Si vyema, wala si afya ya kiroho, kwa Wakristo kuwa na utamaduni wa kufanya ibada za maombi nyakati za usiku huku tukitumia vyombo vya muziki vyenye sauti kubwa (maspika, ngoma, vinubi, zeze n.k.).

Kwasababu Maandiko yanasema:

“Lakini wewe, utakapoomba, ingia chumbani mwako, na ukiisha funga mlango, mwombe Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujibu.” (Mathayo 6:6)

“Danieli alipokwisha kusikia ya kwamba hati imeandikwa, aliingia nyumbani mwake, na madirisha ya chumba chake cha juu yalikuwa yamefunguliwa upande wa Yerusalemu; akaanguka magotini kwake mara tatu kwa siku, akaomba na kushukuru mbele za Mungu wake, k**a vile alivyokuwa akifanya zamani.” (Danieli 6:10)

Baba yetu aliye mbinguni hutusikia vizuri tukiwa katika utulivu na unyenyekevu wa moyo na mwili (ndio maana hapo kwa Danieli huoni ikiwa alibebe spika/ngoma/vinubi au zeze ili vimsaidie katika kuomba)

Hata k**a kuna ulazima wa kutumia vyombo wakati wa ibada za usiku, ni wajibu wetu kutumia sauti ya kati isiyowakera watu au jirani zetu.
Na inapofika saa tano usiku, ni hekima kuzima kabisa vyombo ili kuepusha kero na usumbufu usio wa lazima

Methali ya Kiswahili husema:
“Utamu wa ngoma huujua mchezaji na mpigaji, ila asiyehusika kwake ni kelele.”

Hivyo ninasahauri tu, wala sipo hapa kumsemea mtu fulani

Kwasababu swala la kelele za makanisa nyakati za usiku limekuwa gumzo sana kwa nyakati za leo, hata ukitembelea ofisi za wakuu wa Wilaya kesi hizi ni nyingi mno

Lengo langu napenda tuwe mashahidi wa Kristo kwa hekima, upendo, na kuzingatia amani na utulivu wa kwa wote🙌🙏

HIVI UNAITAMBUA SIRI YA KUWA NI VIGUMU SANA KUTHAMINIWA KUTOKANA NA VILE ULIVYO NAVYO.Lakini ni rahisi sana kuthaminiwa ...
19/09/2025

HIVI UNAITAMBUA SIRI YA KUWA NI VIGUMU SANA KUTHAMINIWA KUTOKANA NA VILE ULIVYO NAVYO.

Lakini ni rahisi sana kuthaminiwa na kupewa nafasi kwenye mioyo ya watu kwa sababu ya vile unavyovitoa, na ukishaijua siri hii, basi jambo lililo bora kuliko yote sio kuwa tu na vitu; bali jambo lililo bora zaidi kuliko yote ni kutoa vitu au Muda wako kulingana na huduma yako au kipawa chako ulichojaariwa na Kristo Kwa maana ni kheri kutoa kuliko kupokea.

Matendo ya Mitume 20;35
“Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.”

Watu huwa hawawakumbuki wanaopokea sana; bali watu huwa wanawakumbuka na kuwaadhimisha wale wanaotoa sana; kwahiyo ukishalijua hilo haupaswi kukaa mkao wa kupokea sana.

Bali unapaswa kukaa mkao wa kutoa sana.!

Hakuna mtu aliyewahi kuweka alama kwenye hii dunia kwa sababu alikuwa mpokeaji sana.

Lakini watu wote ambao waliowahi kuweka alama kwenye maisha ya watu walikuwa ni watoaji sana wa vile walivyokuwa Navyo.!

Hakuna Mtu aliyewahi kuhesabiwa kuwa amebarikiwa kwa sababu ya vile alivyovipokea tu.

Bali kuna ambao wamedumu wakiwa wanaitwa kuwa wao ni wabarikiwa kwa sababu ya vile wanavyovitoa.!

Aliye na vingi ni k**a vile ni rahisi kudhani ya kuwa huwa anaongezewa; lakini ukweli ni kwamba anayeongezewa zaidi kuliko wote ni yule anayetoa zaidi; kwa sababu hiyo Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi.

Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji na Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa.

Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe.

Mithali 11:24-25
“Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji.
Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa; Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe.”

Hakuna aliye na uhitaji mkubwa sana wa vitu k**a Mtumiaji wa vitu na hakuna mtu aliye na utele wa vitu kwenye maisha yake k**a mtoaji wa vitu

Kwa sababu hiyo watumiaji siku zote ndio wahitaji wa siku zote na watoaji wa siku zote ndio watu wa utele siku zote.!

Mtu wa maana kwenye maisha sio yule anayewaza kupokea sana; bali Mtu wa maana siku zote ni yule anayewaza kutoa sana;

Kwani anayewaza sana kutoa atajua na namna ya kupata vya kutoa sana; lakini anayewaza sana kupokea hataweza kujisumbua hata kuwaza namna ya kutoa hata kile alichokipokea.!

Hautaongezewa zaidi kile ambacho hauna uwezo wa kukitoa zaidi; bali utaongezewa zaidi juu ya mengi uliyo nayo ambayo unaweza kuwa tayari hata kuyatoa zaidi;

Kwani apandacho Mtu ndicho atakachokuwa na uwezo wa kukivuna ikiwa ni kile kile au ikiwa kimeongezeka zaidi; lakini kwa vyovyote vile ni kwamba apandae ni lazima atavuna tu.!

Wakati wowote uwao mzuri kwenye maisha huwa sio wakati wa kupokea; bali wakati mzuri kuliko wakati uwao wote kwenye maisha huwa ni wakati wa kutoa sana ikiwa ni sehemu ya kile ulichokipokea sana au ikiwa ni sehemu ya kile umefanikiwa kuwa nacho sana.!

Pata sana na utoe sana na kwa kufanya hivyo utapokea sana pia.!

Ni kweli hauwezi ukatoa kile usichokuwa nacho lakini pia hakuna ambaye hana uwezo wa kutoa kile alicho nacho na hakuna mtu ambaye hana kitu cha kutoa.!

Wahitaji sana ndio wale wanaopokea sana na hao ndio wahitaji wakubwa sana na wanaofanikiwa kuushinda uhitaji sana huwa ndio wale wanaotoa sana;

Kwa sababu hiyo ni kwamba kwa vyovyote ni labda uwe kwenye wahitaji sana ambao ndio wale wanaopokea sana pasipo hata kutoa au uwe kwenye watoaji sana ambao ndio wale wasiokuwa na uhitaji na ambao wameshaushinda kabisa uhitaji!

Pata sana na ondoa uhitaji wako kwa kutoa sana kwani kuhitaji sana hakuwezi kumfanya mtu atoe hata kile alicho nacho; bali kutoa sana huwa kunaondoa kabisa uhitaji.!

Kumbuka kuwa kanuni ya kupanda haiwezi kujipinga hata kwenye suala la kutaarajia mavuno kwani apandacho Mtu ndicho atakachovuna, kwa vyovyote vile uvunaji sana huwa unatokana sana na upandaji sana.!

Kipimo cha kupokea sana sio kipimo cha kupokea kwenyewe; bali kipimo cha kutoa sana ndicho kinachoamua hata kipimo cha kupokea pia.

Kwa sababu hiyo wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho watapimiwa.

Luka 6;38
“Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.”

Ukweli ni kwamba hapa duniani Hatutamkumbuka Mtu yeyote kwa sababu ya vile alivyokuwa anavipokea sana; bali Kwenye hii dunia Tutalazimika kumkumbuka mtu kwa sababu ya vile alivyovitoa.

Kwani Dorkasi hatumkumbuka kwa sababu ya vile alivyokuwa navyo bali watu walimkumbuka kiasi cha kumtafuta Mtume Petro kwa sababu ya vile alivyovitoa.!

Una karama, basi itoe sana na kutokea hapo utaweza kupokea sana pia.!

Una hela au vitu,basi tafuta namna iliyo sahihi ya kuitoa au kuvitoa na kwa kufanya hivyo utapokea sana; kwani wapeni watu vitu nanyi mtapewa pia.!

Toa sana ulicho nacho na kutokea hapo utafanikiwa sana kupokea hata kile usichokuwa nacho.!

Ukikwepa kutoa sana utakuwa umefanikiwa kuukaribisha uhitaji sana, na ukihitaji sana hautakuja ufanikiwe hata kutoa sana; kwani kuna atawanyae lakini huongezewa zaidi na kuna azuiae isivyo haki lakini huelekea uhitaji mkubwa sana.!

KUMBUKA KUWA.
Ni ngumu sana kuthaminiwa kutokana na vile ulivyo navyo; lakini ni rahisi sana kuthaminiwa na kupewa nafasi kwenye mioyo ya watu kwa sababu ya vile unavyovitoa, na ukishaijua siri hii, basi jambo lililo bora kuliko yote sio kuwa tu na vitu; bali jambo lililo bora zaidi kuliko yote ni kutoa vitu; maana ni kheri kutoa kuliko kupokea.

Matendo ya Mitume 20;35
“Ninyi wenyewe mnajua ya kuwa mikono yangu hii imetumika kwa mahitaji yangu na ya wale waliokuwa pamoja nami.”

Tuishi hivo kwani kutoa ni kushinda, Uchoyo na Ualafi na Ubifsi na Pupa katika Maisha haya tuishiyo, Ameni

Zingatia hili; Sio kila penye utoaji pana upendo, Lakini palipo na upendo pana utoaji.

Ameni, Ameni
Na Bwana akubariki sana👋

Bwana Yesu Asifiwe! Wapendwa katika Bwana🙏🏾 Kwa niamba ya team nzima ya Dahuum.com napenda kuchukua frusa hii, kuwakarib...
07/05/2025

Bwana Yesu Asifiwe! Wapendwa katika Bwana🙏🏾

Kwa niamba ya team nzima ya Dahuum.com napenda kuchukua frusa hii, kuwakaribisha watz wote katika semina hii ya neno la Mungu itakayo fanyikia KAHAMA katika uwanja wa Magufuli chini ya Mwl. M wakasege, Kuanzia14/5/2025 hadi 18/5/2025. Muda saa 9 alasiri hadi saa 12 jioni. Semina itarushwa LIVE Youtube kwenye channel yetu,Upendo TV na redio mbali mbali. Mungu awabariki🙏🏾.

UNAJUA NI KWANINI DINI NYINGI ZA KI-KRISTO AFRIKA ZINAISHI KATIKA SURA YA KUAMINI KUWA KILA MTU DINI YAKE NI BORA KULIKO...
03/05/2025

UNAJUA NI KWANINI DINI NYINGI ZA KI-KRISTO AFRIKA ZINAISHI KATIKA SURA YA KUAMINI KUWA KILA MTU DINI YAKE NI BORA KULIKO NYINGINE?

Kana kwamba unaweza kukutana na dini ambayo haina waumini zaidi 1000 ulimwenguni ila bado viongozi wa dini hio wanakuambia kuwa wao ndio bora ulimwenguni kwasababu wao ndio wanaoyaishi vizuri mapenzi ya Mungu ulimwenguni kote hakuna Mwingine

mfano nipo jirani na dini moja hapa kwetu Tz ila stotaja jina lake ina matawi 10 tu Tz nzima wala haina branch zingine kokote ila wakianza hotuba zao, husema kuwa ndio dini ya kweli ulimwenguni kote (kitu ambacho huwa najiuliza Je, Mungu huwa anaangalia hii dini pekee ulimwenguni kote (kana kwamba wao tu ulimwenguni kote ndio watakao twaliwa na Kristo? )🤔

Changamoto hii ya makanisa mengi barani Afrika kuamini kwamba dini yao au dhehebu lao ndilo bora kuliko mengine inajulikana k**a msimamo wa kipekee wa kidini (religious exclusivism). Hali hii imesababishwa na baadhi ya mambo yafuatayo:

1. Historia ya uinjilishaji: Ukristo ulipoletwa Afrika, uliletwa na madhehebu tofauti k**a Wakatoliki, Waprotestanti, na Wapentekoste. Kila moja alipokuja aliweka msingi au lilisisitiza kuwa dhehebu lake lina ufunuo wa kipekee na kweli zaidi, jambo ambalo kwa kiasi fulani lilijenga msingi wa ushindani wa kimadhehebu kwa baadhi ya viongozi waliokuwa waliokuwa na uchechefu wa ufahamu.

2. Mpango wa adui kupunguza kasi ya umoja wa kiroho: ndio maana Makanisa mengi Afrika hayashirikiani katika shughuli za pamoja za kiroho, kijamii au kiuchumi n.k, jambo linalochochea mashindano badala ya mshik**ano wenye kuweza kumshinda Adui.

3. Uelewa mdogo wa mafundisho ya kiroho: Waumini wengi hawapati elimu ya kina ya Biblia na siolojia, hivyo huwa rahisi kushawishika kwamba kile wanachofundishwa kwenye kanisa lao tu ndicho sahihi pekee ilipelekewa na hapo kale viongozi wa dini tu ndio walio miliki vitabu vya dini Biblia n.k.

4. Uchochezi wa viongozi wa dini: Baadhi ya viongozi huendeleza msimamo wa ubora wa dhehebu lao ili kudumisha uaminifu wa waumini wao, mara nyingine kwa kuwahofisha zaidi dhidi ya makanisa mengine (kwa hofu zao za kuogopa kupoteza waumini n.k).

5. Mafanikio ya kifedha, baadhi ya madhehebu yenye mafanikio ya kifedha yamekuwa yakiona kuwa madhehebu mengine haya Mungu ndio maana hayana fedha kitu kinapelekea kuwaona hao k**a wapinzani badala ya kuwaona k**a washirika wenza katika imani.

Tunasahau kuwa hakuna aliye mkamilisha Mungu katika viwango vya kumfahamu na kumwelewa kwasababu kila mtu hutumika katika nafasi aliyopewa kulingana na neema ya Kristo

Ndio maana Paulo kuna pahali anasema au anatolea ufafanauzi kwa kusema kuwa kila mtu humfahamu Mungu kwa kadri alivyopewa neema ya kumpapasa - Matendo 17:24-27

24. Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono;

25. wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.

26. Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;

27. ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu.

Tunapoanza mwaka 2025, M/Mungu atubariki sana sote kwa pamojaMwaka huu ukawe mwaka wa Mavuno ya hatima zetu tulizopanda ...
01/01/2025

Tunapoanza mwaka 2025, M/Mungu atubariki sana sote kwa pamoja

Mwaka huu ukawe mwaka wa Mavuno ya hatima zetu tulizopanda Mwaka 2024 n.k kupitia jina la Yesu Kristo - Amen🙏🏾

Akiba Sio Pesa Tu, Hata WATU Nao Ni Akiba.Kuna watu ambao  wako karibu na wewe ingawa huwa huna Mazungumzo nao ya mara k...
29/12/2024

Akiba Sio Pesa Tu, Hata WATU Nao Ni Akiba.

Kuna watu ambao wako karibu na wewe ingawa huwa huna Mazungumzo nao ya mara kwa mara katika mfumo wa maisha yako ya kila liku

Ila ukiwahitaji huwa wanakusikiliza, Wanakusaidia Na Kukupa Ushauri

Hao Ni AKIBA YAKO, ambao Mungu amekupatia hivyo chunga sana Usiwapoteze.

Hata k**a ikitokea umekwazana na mtu hakikisha unakuwa Na AKIBA YA MANENO.

Kuna Muda Akiba Ya Pesa Unayoitegemea Inaweza Kuwa Ndogo Kuliko Jaribu Ulokutananalo. Na ukajikuta unahitaji Akiba Ya Watu Wema.

Hata Kwenye BIASHARA Kuna Wateja Wanaonunua Kwako Mara Kwa Mara Halafu Kuna (Wateja wa Akiba).

Hivyo, Hakikisha Kila Siku Unaongeza Namba Kwenye AKIBA YAKO YA WATU Ili Uwe kujiwekea msingi thabiti katika yanayo na Mungu akubariki sana 🙏🏿

Mpendwa, tafuta hela ili Usije kuwadanganya watoto wako kuwa kushika pesa nyingi katika umri mdogo ni dhambi. Kauli hii ...
28/12/2024

Mpendwa, tafuta hela ili Usije kuwadanganya watoto wako kuwa kushika pesa nyingi katika umri mdogo ni dhambi.

Kauli hii inaweza kuwatengeneza watoto wako kuwa waoga na wasiojua matumizi sahihi ya fedha. Kana kwamba hata wakiwa wakubwa kila FURSA ya kuwaingizia pesa nyingi watakapo kutana nayo wataiogopa kwa kuhisi ni utapeli tu au ni dhambi.

Kwasababu wazazi wao waliwapandikizia kanuni mbaya vichwani mwao.

Barikiwa sana 🙏

26/12/2024

Hii ni Kiboka kwa Dunia ya Leo🙏🏿

Nini maana ndoto? a)  Ndoto: Ni lugha ya picha ambayo Mungu huitumia kuwasiliana na mwanadamu.    ✍🏾Hesabu 12:6Mawasilia...
24/12/2024

Nini maana ndoto?
a) Ndoto: Ni lugha ya picha ambayo Mungu huitumia kuwasiliana na mwanadamu.
✍🏾Hesabu 12:6

Mawasiliano hayo yanaweza yakawa ni; maonyo, taarifa, tahadhali, mashauri, makatazo n.k

Ambayo yanaweza yakawa ya wakati uliopo, uliopita au ujao.

b) Ndoto: Ni mlango ambao Mungu huutumia kupitisha vitu toka ulimwengu wa roho kuja katika ulimwengu wa mwili.

Note: ndoto ni mlango usiochagua mpitaji ikiwa hauko thabiti katika imani, (usipo kuwa na ufahamu wa kulifunga na kulifungua lango lako la ndoto) namaanisha hata shetani anaweza kuutumia pia

*AINA YA NDOTO*
✍🏾Ndoto zipo za aina tatu ambazo ni:-
01. Ndoto za Ki-Mungu - Ayub 33:14,15

2. Ndoto zinazotokana na mawazo au wingi wa shughuri - Mhubiri 5:3

3. Ndoto za Uongo zinazo tokana na shetani - Yer 23:32.

NJIA ZINAZO TUMIKA KUPAMBANUA NDOTO
01. Karama ya kupambanua Roho - Karama hii ndio kiungo kikuu chenye uwezo wa kupambanua na kutoa tafsiri halisi katika jumbe halisi zilizo katika taswira ya fumbo

Hivyo ni vyema ukimuomba Mungu akujaili karama hii

Kwasababu swala la kutafsiri ndoto halihitaji ujuaji bali linahitaji Karama ili kupata tafsiri halisi

Ndio maana hata akina Yusuph na Daniel hawakuwa wanatumia akili zao Kufasiri ndoto bali walikuwa na muda wa kumuuliza Mungu juu ya hilo

Zifuatazo ni baadhi ya njia zitumikazo kupimia ndoto
A. Neno la Mungu
B. Amani ya Kristo ndani yako Je, inakupa kujitathumini juu ya ndoto hio au husikii kitu chochote ndani yako

Angalizo:
Usifanye haraka kuamini kitu ulichoona kwenye ndoto kabla haujakipima

Ahsante:
Naomba kuwasilisha na M/Mungu atubariki sana 🙏🏿

Usidharau watu, Waheshimu watu kwasababu kuna wengine wanakuja kwako ili kutimiza kusudi fulani katika maisha yako.Ukiwa...
21/12/2024

Usidharau watu, Waheshimu watu kwasababu kuna wengine wanakuja kwako ili kutimiza kusudi fulani katika maisha yako.

Ukiwadharau hao, Umedharau kusudi lako.

ILA CHUNGA SANA
Usiweke tegemezi kwao hatak**a Mungu amewatumia kukuvusha mahali Pagumu chunga sana usije wapa nafasi ya Mungu, endelea kuweka tegemezi lako kwa Mungu aliyewatuma wao kwako.

Barikiwa sana🙏🏿

19/12/2024

Usiache kumshukuru sana M/MUNGU kwa neema na rehema zake kwetu Kwasababu pengine hatukustahili kwa uovu na dhambi zetu kuufikia siku ya leo ila kwa upendo wake ulio mkuu ndio maana hata sasa Bado tu hai

Address

Geita
Mwanza

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Darasa Huru la Uamsho. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to Darasa Huru la Uamsho.:

Shortcuts

Share