Vijana tz jitambue34

Vijana tz jitambue34 vijana kutumia fursa ili kujukwamua kiroho ,kimwili na kiuchumi

Kijana kuna jambo ambalo nahitaji kusema na wewe kwamba unatakiwa utabuwe kuwa kesho yako inaandaliwa Leo jinsi unavyo p...
07/07/2020

Kijana kuna jambo ambalo nahitaji kusema na wewe kwamba unatakiwa utabuwe kuwa kesho yako inaandaliwa Leo jinsi unavyo pambana Leo ndivyo tutakuona kesho nakukuita jina lingine la mpambanaji au mtajiri /mwenye mafanikio biblia inasema Mungu wetu anatuwazia mema kwahiyo jambo ambalo nataka nikutie moyo aujachelewa pambana ili kuijenga kesho yako huku ukimwomba Mungu

24/11/2019

FAIIDA 10 KUWEKEA MALENGO

1. Hukupa mwongozo

Awali ya yote, malengo hukupa mwongozo na mwelekeo maishani mwako. Malengo hukuwezesha kubaini kitu unachokilenga, na hukufanya uelekeze nguvu zako kwenye kitu husika.

Badala ya kushika hiki na kile au kuwa huyu na yule, malengo yatakuwezesha kufahamu unatakiwa kufanya nini au kuwa nani.

2. Hukuwezesha kufanya maamuzi

Baada ya kujiwekea malengo utaweza kubaini ni maamuzi gani yanafaa na ni yapi hayafai kulingana na malengo uliyojiwekea.

Pia utaweza kufahamu mambo ya msingi maishani mwako, hivyo utaweza kufanya maamuzi kulingana na mambo hayo.

Mtu mwenye malengo huwa makini kwenye maamuzi yake kwani analinda asije akafanya maamuzi yatakayoathiri lengo lake.

3. Hukuwezesha kutawala baadaye yako

Unapokuwa na malengo na mipango stahiki ya kuyatimiza, ni wazi kuwa moja kwa moja umeshatawala baadaye yako.

Kuweka malengo ni jambo zuri ambalo litakuwezesha kufahamu aina na mfumo wa maisha yako ya baadaye. Jambo muhimu ni kuhakikisha kuwa unaweka mipango sahihi na inayotekelezeka ya kutimiza malengo yako.

Ni muhimu kuhakikisha kila siku kuna kitu kinachofanyika ili kukamilisha sehemu fulani ya malengo uliyojiwekea maishani.

“Malengo ni ramani ya barabara inayokuongoza na kukuonyesha ni nini kinawezekana kwenye maisha yako”
Les Brown
4. Hukuwezesha kujikita kwenye mambo muhimu

Kuna mambo mengi kwenye maisha yetu ya kilasiku, lakini siyo yote ni ya muhimu kwenye kutimiza ndoto zetu.

Ukiwa na malengo ni rahisi kubaini mipango au mambo yasiyokuwa na umuhimu kwa kutazama yale yote yanayokinzana na malengo yako.

Haijalishi unalipenda jambo fulani kwa kiasi gani, k**a linakinzana na malengo yako, basi huna budi kuliacha.

5. Malengo hukuhamasisha

Unapotazama uzuri na ubora wa malengo yako unapata matumaini na hamasa kubwa.

Hamasa huzidi pale ambapo unaanza kuona ukikamilisha malengo yako ya muda mfupi; hili hukuhamasisha kufanya bidii zaidi ili kuyafikia yale ya muda mrefu.

Ni wazi kuwa chanzo kizuri cha hamasa, ni kujiwekea malengo na kuanza kuyatimiza.

“Jenga ndoto zako wewe mwenyewe, la sivyo mtu mwingine atakuajiri kujenga zake.”
Farrah Gray
Soma pia: Nukuu (Quotes) 50 Zitakazo Kuhamasisha Maishani Mwako.

6. Hutusaidia tusipoteze muda

Mtu mwenye malengo kamwe hawezi kupoteza muda. Ukiwa una malengo ni wazi kuwa muda wako wote utakuwa umegawanywa kwenye kuyafanyia kazi na kuyatimiza malengo yako.

Kwa njia ya kujiwekea malengo hutopoteza muda kwa kufanya mambo ambayo hayakuwezeshi kufikia ndoto na malengo yako.

Haitarajiwi mtu mwenye malengo kuwa mlevi, mvivu, anayechelewa kuamka, anayeshinda kwenye mitandao ya kijamii au vijiwe n.k.

Soma pia: Njia 10 za Kuamka Mapema Asubuhi.

7. Hukuwezesha kufanya uwekezaji sahihi

Ukiwa na malengo ni wazi kuwa utafahamu nini, wapi na lini uwekeze; kwani malengo yako yatakuwezesha kubaini ni uwekezaji gani unaoendana na lengo lako.

Lakini usipokuwa na malengo utawekeza kwenye kila kitu kinachokuja mbele yako na matokeo yake hutoweza kufanikiwa.

8. Malengo hukuwezesha kujitathimini

Unapimaje kufanikiwa kwako k**a huna kipimo cha kupimia kufanikiwa huko? Malengo ni kipimo muhimu kitakachokuwezesha kutathimini k**a umefanikiwa au la.

Ukiwa na malengo ni rahisi kutazama k**a yale uliyoyafanya au unayoyafanya yamekuwezesha kutimiza au kufikia lengo lako.

Ikiwa yamekuwezesha, basi unafanya vizuri; lakini ikiwa hayajakuwezesha kufikia lengo, basi kuna mambo ya kuyatazama upya.

9. Hukufanya upende kile unachokifanya

K**a nilivyotangulia kusema pale awali, kuwa malengo hukuongoza kufahamu unatakiwa kufanya nini, malengo pia yatakuwezesha upende kile unachokifanya.

Ni ukweli usiopingika kuwa ukifanya kitu ambacho unajua kinakamilisha malengo yako utakipenda. Hivyo ni muhimu kuwa na malengo ili yatufanye tupende kile tunachokifanya.

Kwa mfano ukiwa na lengo la kupata kipato cha Sh. 7,000,000 kwa mwezi, ni wazi kuwa utapenda kile unachokifanya kwani kinakuwezesha kutimiza lengo lako.

10. Ujasiri binafsi

Watu wenye malengo wana ujasiri binafsi mkubwa, wanaamini wao siyo k**a watu wengine kwa sababu kuna vitu wanavyoviona tofauti na watu wengine.

Mtu mwenye malengo anajiamini kuhusu maisha yake ya sasa na ya baadaye kwa sababu ana mipango na mikakati stahiki katika maisha yake.
ENDELEA KUFATILIA MASOMO MBALIMBALI YANAYOHUSU VIJANA KUJIKWAMUA KIROHO, KIMWILI NA KIUCHUMI.
MWINJILISTI YUSUPH GENI

26/03/2019

NAMNA YA KUJITAMBUA KIBIBLIA YA KWAMBA UMEFIKA KWENYE KUSUDI LAKO AMBALO MUNGU AMELIWEKA.

Mungu anapotaka kutenda jambo kwako haangalii watu wanasema nini juu yako bali huangalia wewe unataka nini kwake.
Mimi mwenyewe nitaanza kutambulika(waamuzi 14:1-21)
Utakuwa mtu mwenye kuhangaika/Mtu mwenye uhitaji mwingi(Mwanzo 30:1 )
Utakuwa ni mtu unayeshuka na kuomba toba(2Nyakati 7:10)
Utakuwa mtu wa vita dhidi ya uovu wa ibilisi(Hesabu 10:9, Yoeli 2:1)
Utakuwa ni mtu wa kusubiri jibu kutoka kwa Mungu(Yoeli 2:21-26)
MAMBO MUHIMU UNAYOTAKIWA KUYAFUATA ILI UFIKE KILELENI
Kuwa makini na maisha yako ya rohoni na mwilini(Zaburi 1:1, Mhubiri 9:13-16)
Usimpe ibilisi nafasi (Efeso 4:27)
Kuwa na bidii katika kazi zako(Mithali 22:29, Mhubiri 9:10, Wafilipi 4:13)
Lazima uwe na hekima(Mhubiri 7:12)

BY MWIINJILISTI YUSUPH .GENI

25/03/2019

SOMO LA UJASILIAMALI

1. Kuwa mtatuzi wa matatizo

Ujasiriamali ni zaidi ya kupata pesa, ni lazima kwanza utatue changamoto ya mtu ndipo utaweza kupata pesa kutoka kwa mtu husika. Ni muhimu ukafahamu kanuni hii k**a mjasiriamali kwani hutojikita kutafuta pesa bali utajikita kutatua matatizo ya watu.

Kwa mfano k**a kuna tatizo la upatikanaji wa mboga katika mji au eneo unalokaa, ikiwa wewe utaleta mboga katika eneo hilo ni wazi kuwa watu watakupa pesa ili uwape mboga. Hivyo ni muhimu kila mara ukatafuta changamoto ukaitatua, nawe bila shaka utapata pesa za uhakika.

“Pesa ni matokeo ya kutatua shida ya mtu”
2. Kuwa na maono

Hakuna ujasiriamali bila maono. Kuwa mjasiriamali bila maono ni sawa na kuendesha gari isiyokuwa na usukani. Maono katika ujasiriamali yatakuwezesha kukuongoza ufanye nini na kwa muda gani. Ni lazima ujiulize kuwa unataka kuwa nani, lini na unataka kufanya nini baadaye? Jonathan Swift alisema maono ni sanaa ya kuona kile ambacho wengine hawaoni. Ni lazima uwe na lengo na ufanye bidii kulifikia.

“Wajasiriamali waliofanikiwa ni wale walioweza kubadili maono yao kuwa uhalisia”
3. Chagua washirika au timu sahihi

Wakati mwingine utahitaji kufanya kazi na watu au mtu fulani. Ni muhimu kuwa makini wakati wa kuchagua washirika au timu ya kufanya nayo kazi ili kuhakikisha maono yako hayakwamishwi. Kamwe usichukue mtu tu kwa kigezo kuwa ni rafiki au ndugu yako, bali chukua mtu ambaye unaamini anaweza kufanya kitu chenye tija kwa ajili ya kufanikisha malengo yako k**a mjasiriamali.

Soma pia: Makosa 15 Ambayo Kila Mjasiriamali Anatakiwa Kuyaepuka.

4. Toa huduma au bidhaa yenye tija

Hivi leo sokoni kuna bidhaa na huduma nyingi ambazo ni za aina moja, lakini siyo zote zinafanya vizuri. Hii ni kutokana na baadhi ya bidhaa au huduma kutozingatia kuwa na tija kwa wateja wake. Ikiwa unatengeneza bidhaa au huduma fulani hakikisha itakuwa na manufaa makubwa na ya uhakika kwa wateja wako.

Kwa mfano nimewahi kuona vitafunwa vilivyoandaliwa katika mazingira duni na kuwa na dosari mbalimbali k**a vile marashi, vipande vya nywele, mchanga n.k. Ni wazi kuwa bidhaa za namna hii zitakosa wateja kutokana na kuwa na ubora duni.

Kila mara kumbuka kuwa ushindani ni mkubwa, hivyo jitahidi kuongeza tija na ubora wa huduma na bidhaa zako.

5. Fahamu na jali wateja

Ikiwa wewe ni mjasiriamali, basi futa mawazo kuwa wateja wanakuhitaji wewe. Fahamu kuwa wewe k**a mjasiriamali, ndiye unaye wahitaji wateja ili ukuze biashara au huduma yako. Hakikisha mambo haya kuhusu wateja:

Fahamu wanataka nini.
Sikiliza maoni na ushauri wao.
Hakikisha unakamilisha mahitaji yao.
Tumia lugha nzuri na rafiki kwa wateja.
Mfanye mteja aone unamthamini.
Mfanye mteja aone kuwa umetanguliza huduma kabla ya pesa.
Naamini kwa kufanya hivi utaweza kujijengea msingi mzuri wa wateja kwa ajili ya huduma au bidhaa zako kila siku.

6. Tumia pesa vyema

Changamoto ya matumizi mabaya ya pesa inawakabili watu wengi kuanzia kwenye matumizi yao binafsi ya pesa. Watu wengi wanapata pesa lakini zinaisha bila ya kufahamu wamezitumiaje au wamefanya kipi chenye tija.

Soma pia: Njia 10 Zitakazokuwezesha Kutumia Pesa Vyema.

Ni wazi kuwa matumizi mazuri ya pesa ni kanuni muhimu sana kwa mjasiriamali, kwani kwa njia hii utaweza kukuza biashara yako kila siku. Jifunze kufahamu hii ni pesa kwa ajili ya nini, na uitumie kwa mambo ya msingi pekee. Epuka tabia za kibadhirifu na anasa. Ikiwa biashara au uwekezaji wako ni mkubwa, basi unaweza kumwajiri mtu aliye na taaluma ya utunzaji na usimamizi wa pesa.

Unaweza pia kujifunza wewe mwenyewe jinsi ya kutunza na kutumia pesa vyema; unaweza pia kutumia programu za bure za kompyuta k**a vile Wave app kutunza mahesabu yako.

7. Jifunze kusema hapana

“Hapana” ni jibu dogo lakini lenye manufaa makubwa. Ikiwa wewe ni mjasiriamali ni muhimu kuzingatia kanuni hii ya kusema hapana kwani itakutenga na mambo au mipango isiyokuwa na ulazima.

Kuna watu, mipango, vitu au hata tabia ambazo zinaweza kukuathiri vibaya sana kwenye ujasiriamali wako. Hivyo kusema hapana kutakuepusha kwa kiasi kikubwa na mambo haya.

Soma pia: Tabia 10 zitakazobadili maisha yako.

8. Usipuuze nafasi ya teknolojia

Tunaishi kwenye ulimwengu wa sayansi na teknolojia, hivyo wewe k**a mjasiriamali huwezi kujitenga nao. Kwa kupitia teknolojia k**a vile simu na mtandao wa intaneti, unaweza kuwafikia watu wengi zaidi na kuongeza mauzo ya huduma au bidhaa zako.

Hakikisha wewe k**a mjasiriamali unakuwa karibu na wateja wako ili kutatua shida na mahitaji yao; pia hakikisha unajifunza mbinu bora za kufanya biashara kupitia mtandao.

Soma pia: Makosa 8 ya Kuepuka Unapofanya Biashara Kwenye Mtandao.

9. Fahamu soko

Kanuni mojawapo ya kuongeza mauzo yako k**a mjasiriamali ni kulifahamu soko vyema. Hakikisha huduma au bidhaa unayoitoa inakidhi mahitaji na inafika kwenye soko stahiki.

Kwa mfano ikiwa wewe ni mzalishaji wa mayai, lakini eneo ulilopo soko ni duni, basi tafuta eneo jingine ambalo soko la bidhaa hii ni nzuri. Ikiwa wewe huwezi kwenda, unaweza kutafuta mtu kwenye eneo lenye soko zuri akakuuzia bidhaa yako na ukampa gawio fulani.

Kwa kufanya hivi utaweza kulenga soko na kujiongezea faida zaidi wewe k**a mjasiriamali.

10. Ongeza maarifa

Kwanza nikupongeze kwa kusoma makala hii, ni wajasiriamali wachache sana ndiyo hupenda kusoma makala na vitabu mbalimbali ili kuongeza maarifa. Ni muhimu sana kila mara ukajizoesha kujiongezea maarifa, hasa ya ujasiriamali pamoja na kile unachokifanya; hili liitakuwezesha kuwa na tija na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Unaweza kusoma vitabu, majarida na tovuti mbalimbali (k**a fahamuhili.com) ili kuongeza maarifa yako.

11. Jifunze kutokana na makosa

Moja ya kanuni inayozingatiwa na wajasiriamali waliofanikiwa ni kujifunza kutokana na makosa. Makosa ni shule nzuri sana kwa kila mtu hasa wajasiriamali. Ikiwa uliwekeza ukapata hasara, basi jifunze nini hasa kilikuwa chanzo cha hasara ili mbeleni uweze kukiepuka. Usikubali kukwamishwa na makosa, bali yawe ni hamasa kwako ya kuendelea mbele zaidi.

“Uzoefu ni kufanya makosa na kujifunza kutokana na makosa hayo”
Bill Ackman
12. Jifunze kwa waliofanikiwa

Watu wengi wameshindwa kufanikiwa kwenye maisha yao kwa sababu wanajifunza kwa walioshindwa. Walioshindwa wana maneno mengi, hasa ya kukatisha tamaa k**a vile hili haliwezekani, hili linahitaji pesa nyingi sana, mimi lilinishinda, linachosha, lina faida ndogo, kuna wengi wanaolifanya, fulani alishindwa n.k.

Wewe k**a mjasiriamali, epuka watu hawa na ujifunze kwa waliofanikiwa, fahamu walitatua vipi changamoto walizokabiliana nazo pamoja na mipango waliyoitumia hadi wakafika hapo walipo.

13. Tumia muda vizuri

Hakuna mtu mwenye zaidi ya saa 24 duniani; lakini mwingine muda unamtosha wakati mwingine analalamika muda haumtoshi. Ni wazi kuwa mpangilio au matumizi mabaya ya muda ndiyo husababisha changamoto hii. Wewe k**a mjasiriamali ni muhimu ukaondoa mambo yasiyokuwa na ulazima kwenye ratiba yako. Tambua ni kitu gani ni cha muhimu zaidi na ukifanye kwa wakati.

Soma: Kanuni 9 za Kufanikiwa katika Matumizi ya Muda.

14. Weka vipaumbele

Wewe k**a mjasiriamali, ni muhimu kuzingatia kanuni hii ya kujiwekea vipaumbele; vipaumbele vitakuwezesha kubaini ni kipi kianze na ni kipi kifuate kutokana na umuhimu wake.

Kwa mfano ikiwa kuna wateja walipata shida kupata huduma au bidhaa yako, maliza kwanza swala hili kabla ya kuendelea kuweka jitihada za kuuza bidhaa mpya. Kwa kufanya hivi utaweza kufanya mambo kutokana na umuhimu wake, jambo ambalo litakuwezesha kukua.

15. Usikate tamaa

Ni wazi kuwa katika safari ya ujasiriamali utakutana na changamoto mbalimbali. Jambo la msingi ni kukumbuka kanuni hii kuwa usikate tamaa. Tumia changamoto k**a chachu ya kukuhamasisha kufanya bidii zaidi na usirudi nyuma.

BY MWINJILISTI. YUSUPH GENI

25/03/2019

NAMNA YA KUFANIKIWA KIMAISHA
Katika makala hii nitakuonyesha vitu vitano (5) ambavyo unapaswa kujiepusha navyo katika maisha yako ili uweze kufanikiwa.

Jambo la kwanza: Epuka kuwa Mtu wa visingizio; Benjamin Franklin aliyewahi kuwa Mdiplomasia kutoka nchini Marekani Enzi za uhai wake aliwahi kusema yafuatayo "If you want something you will find a way, but if you don't want it you will find an excuse" Maana yake Ukiwa na uhitaji wa kitu flani na ukaweka nia juu ya hicho kitu lazima utatafta njia na namna ya kukifanikisha lakini k**a huna nia na wala hukihitaji kitu hicho hata k**a utashirikishwa na ndugu, jamaa ama rafiki lazima utatafta visingizio na namna ya kukwepa. Hivyo epuka kuwa mtu mwenye sababu na visingizio bali jifunze kuchukua hatua pindi uonapo fulsa.

Jambo la pili: Epuka kufanya mambo kwa ajili ya kuwafurahisha watu flani katika maisha yako bali fanya mambo yenye manufaa katika maisha yako; Binadam tunazungukwa na jamii kubwa yanye rika tofauti tofauti wakiwemo ndugu,Marafiki,na watu wennye sifa tofauti tofauti, K**a una malengo ya kufanikiwa katika maisha yako epuka kufanya vitu ili usifiwe na marafiki zako ama upate sifa kutoka kwa ndugu zako, Ila fanya vitu hivyo endapo tu vinakufikisha katika safari yako ya mafanikio, Ustumie muda wako mwingi kufukiria nini n ufanye ili flani afrahi na aksifie,Bali tumia muda wako mwingi kufikiri nini cha kufanya ili ufanikiwe.

Jambo la tatu: Epuka lawama (Usipende kuwa mtu wa kulalamika sana kwa kila jambo) , Katika maisha kila binadamu hukumbana na changamoto zenye viwango vya aina mbalimbali japokuwa si vyema kuweka wazi kwa kila mtu Magumu unayo kutana nayo katika maisha yako kwani wengi wao hawana msaada kwako tofauti na kukupa maneno yatakayo kukatisah tamaa zaidi; Hakuna mwanadamu anayependa jamii ijue undani wa maisha yake nikiwa na maana ya kuwa k**a ni maskini hakuna anayependa jamii iatambue yeye ni maskini kwa kiwango gani maana inaweza kumpunguzi thamani yake katika jamii, ukiwa Mtu wa kulalamika na kumweleza kila mtu matatizo yako inakupunguzia thamani yako katika jamii na kuifanya jamii inayo kuzunguka itambue kiwa ngo cha umaskini ulionao hali ambayo ianaweza kukukatisha tamaa ya kusonga mbele na kujiona usiye kuwa na thamani na usiye faaa katika jamii, Hivyo jifunze namna ya kutatua matatizo na changamoto unazo kumbana nazo.

Jambo la nne;Epuka kujilinganisha na wengine; Kujilinganisha na watuflani katika maisha yako ni sumu kali sana juu ya mafanikio yako kwani jambo hili limewaathiri watu wengi sana na hata mafanikio yao pia, Katika maisha jenga msingi wa kujiamini na kujikubali kwa vile ulivyo na kwa kile unacho kifanaya, watu wengi wanshindwa kufanikiwa katika misha kwa kushindwa kuzipokea fulsa mbali mbali zenye msingi bora juu ya mafanikio yao kwa kigezo cha kuhofia Marafiki zao watawaona je, Wachumba zao watawaona je ama ndugu zao watawaona je. Katika maisha jenga msingi wa kuishi pasipo kuiga wala kutazamia maisha ya jirani ama rafiki yako, ishi wewe k**a wewe kwani hata hao unao wahofia hawana msaada wowote juu ya mafanikio yako.

Jambo la tano: Epuka kuwa mtu wa kusubiri; Watu wengi wamekuwa ni waoga wa kuchukuwa maamuzi sahihi hata wakati fulsa zinapo jitokeza, yaani wao kila kitu wanapanga majira na nyakati ambazo hata zinapofika nyakati hizo hawana utayari wa kutekeleza mipango waliyo jiwekea, kwamfano ulipanga mwakani utajifunza ushonaji kwa kigezo cha kuwa bize na masomo ama shughuli za kifamilia, lakini siku zinapo wadia hamna unachofanya na nyakati zinazidi kusonga, Hatimaye inafikia wakati ambapo kila kitu autakacho plani kufanya unajikuta wakati umekwisha kukuacha. Hivyo katika maisha jifunze kuwa mtu wa vitendo na siyo mipaango kwani ni bora umefanya ukafeli kuliko kutofanya kabisa.

BY MWINJILISTI. YUSUPH GENI.

09/06/2018

Address

Musoma

Telephone

+255764181726

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Vijana tz jitambue34 posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to Vijana tz jitambue34:

Shortcuts

Share

Category