Buhare Community Development Training Institute

Buhare Community Development Training Institute Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Buhare Community Development Training Institute, College & University, Buhare, Musoma.

Buhare CDTI is the public institute under the MINISTRY OF HEALTH, COMMUNITY DEVELOPMENT, GENDER, ELDERLY AND CHILDREN in Tanzania.We are here to show what we are doing in the community to catalyzes social and economic development of Tanzania

17/02/2024

Kwa maitaji ya chuo kwa ngazi ya cheti mpaka degree piga number 0754338911 upate maelekezo zaidi. Karibuni

Karibuni chuo Cha mipango campus ya Mwanza hapa kisesa nyie tuna degree hapa na masters zipo hapa. Niulize piga 07543389...
28/07/2023

Karibuni chuo Cha mipango campus ya Mwanza hapa kisesa nyie tuna degree hapa na masters zipo hapa. Niulize piga 0754338911 nikueleweshe. Be wise be professional!

29/06/2021

Sorry this page is no longer useful to users please contact the institute direct by phone or other means.
Thank you

02/05/2020

Chukueni tahadhari popote mlipo Corona inaua tufuate maelekezo ya wataalamu wa Afya. Na tumwombe Mungu atuhurumie.

#

19/03/2020

TANGAZO
Mkuu wa chuo anawatangazia wanafunzi wote kwamba baada ya Field Kwisha! Wabaki au waende kwao hadi itakavyoamuliwa vinginevyo, watapewa taarifa lini Chuo kitafungua. Pia Special Exams zilizotarajiwa kuanza tarehe 30 Machi hazitakuwepo tena. Watatangaziwa lini zitafanyika. Hii ni baada ya maamuzi ya serikali kufunga vyuo ili kupambana na ugonjwa wa mlipuko wa corona

Asanteni.

By
Utawala

Mkuu wa chuo kwa niaba ya watumishi wote anatoa pole kwa wazazi, jumuiya ya chuo na wanafunzi woote kwa msiba wa mwanafu...
25/02/2020

Mkuu wa chuo kwa niaba ya watumishi wote anatoa pole kwa wazazi, jumuiya ya chuo na wanafunzi woote kwa msiba wa mwanafunzi wa NTA Level 5 anaitwa Rachel Juma(picha chini) aliyefariki tarehe 24/2/2020 huko nyumbani kwao. Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake libarikiwe.

Imetolewa na:

Mr. Paschal Mahinyila,
Mkuu wa Chuo, Buhare CDTI

SIDO mkoa Wa Mara kwa kushirikiana na Chuo cha maendeleo ya jamii Buhare imeendesha mafunzo ya utengenezaji sabuni za Ma...
27/01/2020

SIDO mkoa Wa Mara kwa kushirikiana na Chuo cha maendeleo ya jamii Buhare imeendesha mafunzo ya utengenezaji sabuni za Maji na mche kwa siku5 kuanzia tarehe 20-24 mwezi January, 2020. Jumla ya wahitimu 6 kutoka Buhare CDTI ambao ni wanafunzi Wa NTA level 5 walishiriki kwa gharama zao na kujipatia vyeti vya mafunzo kutoka SIDO. Zana ya kujiajili inapenya ubongo kwa wanafunzi wetu tunapowaandaa kutokutegemea kuajiriwa, na bado kuna wengi wataenda wapatapo fedha ya kulipia ada ya ushiriki. Mafunzo yatolewayo mengine ni pamoja na utengenezaji wa vyakula na mifuko mbadala.
Mafunzo haya yana ratibiwa na mratibu Wa kituo cha ubunifu na maarifa "Digital innovation Center" na pia Mwalimu Wa somo la Ujasiriamali. Ndugu, Jackson Bulili.

"We transform the mindset of the Youth for self reliance"

Chuo cha maendeleo ya jamii Buhare leo kimekabidhi matofali 400 na mifuko 8 ya sementi kwaajili ya kufanikisha ujenzi wa...
17/01/2020

Chuo cha maendeleo ya jamii Buhare leo kimekabidhi matofali 400 na mifuko 8 ya sementi kwaajili ya kufanikisha ujenzi wa madarasa na vyoo ktika shule za sekondari na Msingi Buhare,Manispaa ya Musoma. Mratibu Wa program ya ushirikishwaji jamii Ndugu Kahama ameongoza zoezi la uchangishaji fedha kwakuwatumia wanafunzi wa chuo pamoja na jamii hatimae pesa ya tofali na simenti hizo zikapatikana.

Kwapamoja tunaleta maendeleo"

MKUTANO WA MAENDELEO KATA YA BUHARE WAFANYIKAWakufunzi Wa chuo ndugu AVITY ACHARD na Ndugu LUIS KAHAMA na baadhi ya wana...
15/01/2020

MKUTANO WA MAENDELEO KATA YA BUHARE WAFANYIKA

Wakufunzi Wa chuo ndugu AVITY ACHARD na Ndugu LUIS KAHAMA na baadhi ya wanafunzi leo wamewezesha kufanyika kwa mkutano wa wananchi na viongozi wa serikali Wa kata ya Buhare kujadili jinsi ya kupata pesa za kumalizia ujenzi Wa madarasa Wa shule ya sekondari Buhare. Mkutano huu ni nizao la zoezi la amsha ari linalotekelezwa na chuo kwa wananchi Wa manispaa ya Musoma kuchangia maendeleo yao wenyewe kwa rasilimali walizonazo.

ZOEZI LA UKUSANYAJI TAARIFA KWENYE JAMII MANISPAA YA MUSOMA (Community Profiling)Chuo cha maendeleo ya jamii Buhare Leo ...
14/01/2020

ZOEZI LA UKUSANYAJI TAARIFA KWENYE JAMII MANISPAA YA MUSOMA (Community Profiling)

Chuo cha maendeleo ya jamii Buhare Leo tarehe 14/1/2020 kimefanya zoezi la ukusanyaji Wa taarifa za jamii kwa kutumia dodoso la kaya ili kuweza kubaini matatizo ya jamii na kutambua matatizo yapi ya kuyapa kipaumbele katika kuyatatua na mambo mengineyo yahusuyo jamii kwa ujumla.
Taarifa hizi zitasaidia kuanzisha kanzi data ya matatizo yanayokabili jamii na kuweza kuyatafutia suluhisho kwa kushirikisha wadau wote Wa maendeleo.
Zoezi hili limefanywa na wanafunzi wa ngazi ya Diploma ya maendeleo ya jamii wakisimamiwa na walimu wao chini ya uratibu wa Mratibu wa programu ya Ushirikishwaji Jamii (Community Engagement) Ndugu. Luis Kahama. Pia zoezi limehusisha uongozi wa serikali za mitaa katika kata za Kigera na Buhare ndani ya Manispaa ya Musoma.

Mtaalamu na mratibu Wa somo la ujasiriamali Ndugu Jackson Bulili akiwa katika picha ya pamoja na vijana Wa NTA Level 5 b...
13/01/2020

Mtaalamu na mratibu Wa somo la ujasiriamali Ndugu Jackson Bulili akiwa katika picha ya pamoja na vijana Wa NTA Level 5 baada ya mafunzo mafupi ya kutengeneza sabuni ya Maji ambayo yaliendeshwa na Ndugu Romward ambae na mwanafunzi Wa NTA level 6, huyu ni zao la mafunzo yaliyoendeshwa mwaka 2019 kwa kushirikiana na wataalamu kutoka SIDO Ofisi ya mkoa Wa Mara ambapo waanafunzi zaidi ya 350 walishiriki na kupata ujuzi huo Wa kutengeneza sabuni pamoja namna ya kuuza bidhaa sokoni "Marketing skills".
Program hii imesaidia kubadiri fikira za wanafunzi wengi kujitengenezea ajira zao badala ya kusubiri kuajiriwa na hivyo kusaidia kupunguza tatzo LA ukosefu Wa ajira kwa vijana wahitimu Wa vyuo Nchini.
Bidhaa hizi bora kabisa zinapatikana hapa Chuoni mpaka sasa na zinaendelea kutengenezwa, karibuni.

Address

Buhare
Musoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Buhare Community Development Training Institute posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share