10/11/2025
Ilikuwa siku njema sana katika kituo cha hija cha kitaifa kiabakari jimbo katoliki la musoma ambapo kidato cha nne pamoja walimu wote wa shule ya sekondari Nyegina walikutana kwa ajili ya mafungo kuelekea mitihani ya mwisho ya kumaliza elimu ya sekondari inayotarajia kufanyika tarehe 17 November 2025. Meneja wa shule Fr. Robert Luvakubandi pamoja na fr. Avitius walishiriki kutoa semina pamoja na kuongoza mafungo hayo. Matumaini pamoja na uungwana ndo silaha zetu katika wakati huu. Mungu ni mwema