Stella Maris Mtwara University Students' Organisation

Stella Maris  Mtwara University Students' Organisation Stella Maris Mtwara Students Organisation (STEMMUSO)

HABARI ZILIZOTUFIKA HIVI PUNDE   KWA NIABA YA JUMUIYA YA WANA STEMMUCO KWA MASIKITIKO MAKUBWA NATOA TAARIFA YA KIFO CHA ...
02/10/2016

HABARI ZILIZOTUFIKA HIVI PUNDE

KWA NIABA YA JUMUIYA YA WANA STEMMUCO KWA MASIKITIKO MAKUBWA NATOA TAARIFA YA KIFO CHA NDUGU YETU Martin Myombe AMBAYE ALIKUWA MWANACHUO SHAHADA YA ELIMU (BAED) MWAKA WA MASOMO 2013/2016.
MAREHEMU AMEUGUA GHAFLA AKAPELEKWA HOSPITALI YA WILAYA HUKO KWAO MBEYA SIKU YA IJUMAA TAR.30/09/2016, AMBAPO ALIPATIWA VIPIMO NA KUGUNDULIKA NA UGONJWA WA TYPHOID.ALIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HADI JANA JIONI TAR.01/10/2016 HALI YAKE ILIPOBADILIKA NA KUFARIKI!!!
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA!
R.I.P NDUGU MARTIN MYOMBE!!!

24/01/2015

Matoke ya uwanjan jana na leo. Jana kwenye mechi ya nusu fainali washindi wa pili wa mwaka jana Fighters FC walilala kwa kichapo cha goli moja bilaaaa dhidii ya mahasimu wao Alliance FC. Goli lilifungwa na Benjamini Bagowe mnamo dak ya 5 ya mchezo. kecho tar 25/01/2015 kutakuwa na mechi ya fainali kati ya mwaka wa tatu A na mwaka wa pili A ( Alliance FC) majira ya saa 10 jioni kwenye viwanja vya TTC. Mechi ya mshindi wa 3 kati ya mwaka wa kwanza na mwaka wa pili B (Fighters FC ) itafanyika saa 8 mchana.
BASKETBALL
Wale mabigwa watetezi mwaka wa pili waendelea na rekodi ya kutofungwa baada ya kutoa kichapo kwa kaka zao wa mwaka wa tatu. Mwaka wa pili walitoka vifua mbele kwa point 49 kwa 38.

23/01/2015

TANGAZO TANGAZO TANGAZO
Ni kwa mara nyingine mashindano ya BIG SCORE yanafikia kilelee siku ya jumamosi baada ya hatua ya makundi kumalizika. Kwenye football leo tar 23/01/2015 siku ya ijumaa kutakuwa na mechi ya nusu fainali kati ya mwaka wa pili B a.k.a Fighter’s FC dhidi ya mwaka wa pili A a.k.a Alliance FC, mechi itachezwa majira ya saa 8:00 mchana kwenye kiwanja cha jeshini. Mida ya saa 10:00 jioni vijogoo wa mwaka wa tatu watapambana wa mwaka wa kwanza kwenye kiwanja cha jeshini. Fainali itachezwa tar 25/01/2015 kwenye viwanja vya TTC
Netball:
Baada ya mzunguko kumalizika sasa wadada wa mwaka wa pili wanakutana uso kwa uso na wadada wa dip&cet katika mechi ya fainali tar 25/01/2015
Katika viwanja vya TTC . Je wadada wa dip&cet watalipa kisasi kwa kichapo cha mara ya kwanza walichopata kutoka kwa dada zao wa mwaka wa pili? Karibu ujioneee
Basketball
Baada ya mzunguko sasa mwaka wa pili ambao ndo mabingwa watetezi wataminyana na mwaka wa tatu katika mechi ya fainali itakayofanyika siku ya Jumamosi katika kiwanja cha Bandari Club majira ya saa 10:00 jioni. Je mwaka wa pili wataendeleza ubabe wao wa kutofungwa na madarasa mengine? Karibu ujionee
WOTE MNAKARIBISHWA SANAAAAAA .

Basketball Team wakijiandaa kwenye mechi ya fainali ya SU-SAUT yaliyofanyika Moshi kwenye viwanja vya CCP
02/01/2015

Basketball Team wakijiandaa kwenye mechi ya fainali ya SU-SAUT yaliyofanyika Moshi kwenye viwanja vya CCP

STEMMUCO Basketball team ikijiandaa kwenda kushangiliaa timu ya netball kwenye viwanja vya CCP Moshi
02/01/2015

STEMMUCO Basketball team ikijiandaa kwenda kushangiliaa timu ya netball kwenye viwanja vya CCP Moshi

14/10/2014

Karibuni sana mwaka wa kwanza mliochaguliwa kujiunga na mwaka wa masomo 2014/2015. Kwa tulio wenyeji tuwasaidie wadogo zetu kukifahamu chuo na mambo wanayopaswa kuyafanya kwa wakatii. Mungu atubariki tufikie malengo yetu salama

13/07/2014

KWA WANACHUO AMBAO BADO WAPO CHUON BADO WAPO MAENEO YA MTWARA NA WALEO WALIO KARIBU NA MTWARA, SHUGHULI ZA KUAGA MWILI WA MAREHEMU ZITAFANYIKA CHUONI MIDA YA SAA MBILI KAMILI ASUBUHI ENEO LA CHUO. WANACHUO WOTE TULIOKO KARIBU TUNAOMBWA KUFIKA KWENYE SHUGHULI HII.

12/07/2014

R.I.P MADAM KOPOKA, TULIKUPENDA ILA MUNGU KAKUPENDA ZAIDI. UCHUNGUZ UNAFANYIKA KUJUA CHANZO CHA KIFO CHAKE

26/06/2014

Wizara ya Habari pamoja na serikali ya wanachuo tunawatakia kila la kheri katika maandalizi ya UE, kwa wale tunaoenda field kijijin Mungu atutangulie

15/06/2014

Hayawi hayawiii sasa yakuwaaaa, kweli hamna historia ambayo haiwezi kuvunjwa. Wale vigogo wa soka katika Chuo Kikuu Cha SAUT The White Eagle waharibu rekodi ya kutofungwa baada ya miamba ya soka ya mwaka wa kwanza The Fighters walipo wanyuka goli moja bila (The Fighters 1 - White Eagle 0 ). Goli hilo lilifungwa katikati ya kipindi cha kwanza. kipindi cha pili White Eagle walijaribu kulinda heshima lakin wakatoka vichwa chini k**a kuku mwenye mdondo.
Baada ya mechi kulitokea jambo la kushangaza kweliii, binadamu wengi hatuna tabia ya kuwakubali wenzetu pale wafanyapo mema. White Eagle walijikusanya na kuanza kuimba nyimbo za kukubali kufungwa, walikuja walipokuwa The Fighters na kuwapongeza kwa kuwafunga, waliwapa maneno ya ushauri ili kuendeleza vipaji vyao wawapo chuoni. Pia baadhi ya wachzaji wa White Eagle waligawa jezi zao kwa wacheazi wa The fighters k**a ishara ya upendo.

Address

Shanagani
Mtwara
P.O.BOX674

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Stella Maris Mtwara University Students' Organisation posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category