10/07/2024
Kisa cha "Pango la Plato"
Je, umeshawahi kupingwa, kuchukiwa ama kuwa adui kwa kuwa tu unaongea kitu ambacho wengi hawakijui ama hawakiamini?
Soma kisa hiki cha “Pango la Plato”
Pango la Plato ni kisa kilichosimuliwa na Mwanafalsafa mashuhuri wa Kigiriki aliyefahamika kwa jina la Plato. Kisa hiki kinapatikana katika kitabu chake mashuhuri kinachofahamika k**a “The Republic”. Ni kisa cha kubuni lakini kina hekima na mafunzo ndani yake.
Katika hadithi hii , Plato anawazungumzia watu waliozuiliwa pangoni tangu kuzaliwa kwao. Yani, watu hawa hawajawahi kuwa nje ya pango hili kwa maisha yao yote. Wachambuzi au wasimulizi wengine wamekuwa wakiwaita watu hawa wafungwa. Wakiwa pangoni, wafungwa hawa walitazama upande mmoja. Pata picha ya watu wanaotazama sinema huku nyuma yao wakitenganishwa na ukuta ambao mwanga uliweza kupenya kupitia uwazi mdogo katika ukuta huo.
Kwa miaka yote, mara kadhaa moto🔥 ulichomwa na mwanga kupita moja kwa moja hadi kwenye ukuta ambao ulitazamwa na wafungwa ndani ya pango. K**a haitoshi, vitu kadhaa ,k**a vile, wanyama, sanamu n.k. vilipitishwa nyuma yao , na kutengeneza vivuli au taswira kwenye ukuta walioutazama.
Kwa kuwa wafungwa hawa hawakuwa na taarifa zozote zaidi ya zile walizoziona ukutani, huu ndiyo ulikuwa ulimwengu wao. Ulikuwa ndiyo ukweli wa maisha yao. K**a waliona taswira ya jua, basi lile ndiyo jua lao, k**a waliona taswira ya tembo, huyo ndiyo tembo wao. Lakini , ukweli ni kwamba watu hawa hawakuona vitu halisi bali taswira ya vitu hivyo.
Siku moja mmoja wa wafungwa wale aliachiwa huru na kutolewa nje. Kutokana na “mawenge”, ilimchukua muda kidogo kutambua alichokiona. Siku hiyo aliweza kuviona vitu katika uhalisia wake na kwakweli alishangaa mno! 😲 🙀. Aliporudi pangoni na kuwasimulia wenzake alichokiona na kuwaambia wanavyoviona si vitu halisi, wenzake walimpinga, kumshambulia na kumuona msaliti aliyedhamiria kuwatoa “kwenye reli”.
Japo si katika mazingira yote, upinzani tunaokutana nao pindi tunapowakilisha mawazo mapya miongoni wanajamii hutokana na watu kuishi pangoni. Katika kisa hiki, mfungwa aliyetolewa nje anafananishwa na mwanafalsafa, mwanazuoni au mtu yeyote mwenye mawazo mapya ambayo kwa kiasi kikubwa yanakinzana na kile jamii, familia au kikundi chake huyaamini. Kwa maneno mengine, Plato anadai kuwa mambo tunayoyaona au kuyasikia ni taswira tu ya vitu halisi. Hivyo, pango katika muktadha huu, ni mazingira tunamoishi ambayo hutawaliwa na taarifa zisizo sahihi au zisizo kamilifu. Katika mazingira ya namna hii, Plato anaona kuwa ukweli wa mambo hupatikana kupitia tafakuri tunduizi.
Udadisi
1.Katika mazingira k**a haya ya pangoni ambapo watu hupangiwa cha kufanya na uhuru wao kudhibitiwa, wahusika watawezaje kufikiri nje ya kile wanachoamini? Wana kipi kipya kitakachosababisha wajiongeze?
2. Katika kisa hiki, tunaona mfungwa mmoja aliachiwa huru kwa kutolewa pangoni. Waliomtoa walikuwa ni watesi wao bilashaka. Je, iwapo watesi wale wasingeamua kumtoa mmoja wao, nini kingetokea kwa wafungwa wale? Ukombozi katika mazingira k**a hayo hufanyikaje? Ninashauri tumsome Paulo Freire katika “Pedagogy of the Oppressed” kisha tukutane kwenye muendelezo wa kisa hiki.
Shukrani
Kuhusu Pango la Plato:👇
https://www.youtube.com/watch?v=1RWOpQXTltA
MindMingle, Kijiwe cha tafakuri
View full lesson: http://ed.ted.com/lessons/plato-s-allegory-of-the-cave-alex-gendlerTwenty four hundred years ago, Plato, one of history’s most famous think...