Maneno Ya Ushindi

Maneno Ya Ushindi Kufundisha Neno la MUNGU watu wote likalowapata ushindi katika maisha ya mwanadamu

Zaidi ya Mungu, wazazi... Hakuna mtu mwingine anayependa ndoa ya mtu iwe na amani, upendo na kudumu muda mrefu.Hivyo, hu...
13/10/2025

Zaidi ya Mungu, wazazi... Hakuna mtu mwingine anayependa ndoa ya mtu iwe na amani, upendo na kudumu muda mrefu.

Hivyo, hufanya vyovyote ili kuhakikisha amani, furaha, upendo na kudumu kwa muda mrefu wa ndoa kutofikiwa.

Unajua hakuna mtu ambaye anapenda ndoa yake ivunjike, hakuna mwanaume anayetamani kutoka nje ya ndoa, hakuna mwanamke anayetamani kumchiti mume wake

Pasipo kujua;.

Wako wanaopambana usiku na mchana kuhakikisha mnafarakana.
Wanaotafuta kila namna kumroga mume au mke wako.
Wanafanya chochote ili mume wako atembee nao.
Wako tayari kufanya lolote ili kuhakikisha kuwa ndoa haidumu

Kila mmoja kwenye ndoa anapaswa kupigana vita zake vizuri ili mipango yao isifanikiwe.

Kila mmoja anapaswa kumwombea mwenzake kwa mzigo sana endapo anaitaka ndoa

Kuacha kidogo tu kusimama kwenye nafasi ambayo unapaswa kuwa ni nafasi nzuri ya adui kutimiza lengo lake.

Kusema nimeshaolewa ndo basi haujishughulishi na lolote, utaipoteza ndoa.

Mpende, mlinde na kumtunza mukeo

Mpende, mheshimu, mtii, mwombee mumeo.

04/09/2025
04/09/2025

Umesoma machapisho mengi sana, Umesoma Biblia yote na kuimaliza yote, umesikiliza audios nyingi sana, umehudhuria makongamano mengi na ya kutosha na umefanya kila kitu kupata maarifa.

Lakini hadi sasa hauoni uhalisia wa kile ambacho imekuwa ukijifunza kwa siku zote hizo!

Neno la Mungu bado halijawa halisi kwenye Maisha yako bado!

Ahadi za Mungu hazijawa halisi katika Maisha yako bado!

Na unajua kuwa "Hakuna maana Ikiwa utimilifu wa kazi ya Yesu Msalaba hauko halisi kwenye maisha yako"

Hivyo haijalishi umesoma Neno la Mungu kiasi gani, Ikiwa hakuna uhalisi kwenye maisha yako "hakuna maana kabisa"

Sasa! Inakuwaje sioni uhalisia kwenye maisha yangu?

Inakuwaje ile "tumebarikiwa kwa baraka zote za rohoni" si halisi kwenye maisha yangu?

"Personalisation of the Word of God" [Kubinafsisha Neno la Mungu]

Usomapo Neno la Mungu, mafundisho au chochote unachojifunza, nifanye kuwa cha kwako na kukisema kila siku na kila wakati.

Unapoendelea kusema na kukiri kila siku na kila wakati, itafanya kuwa halisi kwenye maisha yako.

Itaendelea.

Mwl. Joshua Golyama

+255 764 257 495
Morogoro, Tanzania.

Address

Kididimo
Morogoro

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Maneno Ya Ushindi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to Maneno Ya Ushindi:

Shortcuts

Share