Jesus Disciple Organisation J.D.O

Jesus Disciple Organisation J.D.O Yohana 17:3,
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.! Karibu kwaajiri ya uzima wa milele.!

Kwa waimbaji
08/04/2022

Kwa waimbaji

🟠🟢 MUZIKI WA INJILI [ SEHEMU YA 1 ]

K**a ulikuwa unapata shida kuielewa tathnia hii ujumbe huu ni kwa ajili yako, naamini hutabaki k**a ulivyo, kuna badiliko kubwa mno linaenda kutokea siku ya leo.

Hapa kuna maneno mawili, yaani “MUZIKI” na “INJILI”; tutakuwa huru kujifunza endapo tutatoa tafsiri ya INJILI kibiblia (Neno la Mungu), zipo tafsiri mbali mbali.

1) MANA YA KWANZA YA INJILI

INJILI:- ni habari njema za ufalme wa Mungu; Injili imekuwa ikihubiriwa toka torati na manabii, YESU mwenyewe na Mitume wake (wanafunzi); malaika Gabriel ni mjumbe wa Mungu, hupeleka habari njema.

Ametumika kila mara tunaona kwa Daniel Malaika anakuja kumpasha habari (Daniel 9:21-23) na kwa bikra maria (luka 1:26-38) na sehemu zingine katika biblia. Kwahiyo ni Dhahiri kuwa INJILI NI HABARI NJEMA ZA UFALME WA MUNGU.

2) MAANA YA PILI YA INJILI

INJILI:- ni uweza wa Mungu uletao wokovu (warumi 1:16). Mtume Paulo anasisitiza kuwa hataionea haya injili kwa sababu ni uweza wa Mungu uletao wokovu (kwa tafsiri rahisi ni kwamba; hatupaswi kuogopa kuhubiri/kupeleka injii kwa sababu siyo sisi tunaookoa bali injili peke yake inaouweza ndani yake wa kuleta wokovu).

Ila ni muhimu anayehubiri awe na nguvu za Mungu/uweza wa Mungu ndani yake ndipo injili itakuwa na uwezo vinginevyo hizo ni lectures tu. DON’T BE ASHAMED OF THE GOSPEL

K**a Mungu alikuwezesha kuishinda dhambi Fulani kupitia injili yake, na wewe umepakwa mafuta (ANOINTING) ya kumsaidia Mwingine, fanya kwa nafasi yako usisubiri mpaka mchungaji aje, hata hivyo huko kazini kwako yeye hawezi kufika ila wewe ndiye muwakilishi, usione kazi/Ajira pekee tu, ona kusudi la Mungu kwenye hiyo kazi/Ajira/Biashara.

3) MAANA YA TATU YA INJILI

INJILI (Kingdom Gospel), ni uwezo wa kumfunua KRISTO YESU (MUNGU) ambaye haonekani kwa macho ya kawaida, na kumuumba ndani ya mioyo ya watu kwa jinsi ya rohoni, usihubiri injili ukiwa mwilini pekee. (kiingereza wanasema Kingdom Gospel is the appearance of invisble God)

BWANA YESU alisema hivi “Juu ya Mwamba Huu Nitalijenga Kanisa Langu”, najua utajiuliza Je, MWAMBA GANI? Je, kabla ya kauli hii kulikuwa na nini hapo juu? utagundua kulikuwa na mdahalo wa YESU NI NANI?

Wapo waliosema ni eliya wapo waliosema mojawapo ya manabii wa kale, lakini petro kwa uweza wa Roho Mtakatifu akasema “WEWE NDIWE KRISTO, MWANA WA MUNGU ALIYE HAI.”

Yesu alijibu heri wewe maana damu na nyama hazikuweza kuwafunulia, ooh! Kumbe aliyemfunua ni Roho Mtakatifu aliyekuwepo Ndani mwa petro. (Mathayo 16:13-18)

Kwa andiko hili, kanisa (mwamini) litakalomfunua kristo ambaye ndiye Mwamba hapo ndiposa Yesu atajenga makazi yake, angalia kanisa ambalo halimjui Kristo Jinsi alivyo, Lilivyo Nyonge na kuizoelea Injili, kuizoelea dhambi na uchafu wa dunia hii.

Bwana Yesu alisema mkiniona mimi mmemuona Baba (YOHANA 14:7-10), na Yesu ndiye ule Mwamba, kumbe Ukimfunua Kristo kwa uwezo wa Roho Mtakatifu basi Kristo atamfunua Baba, hapo ndipo tunasema;...
... “Kingdom Gospel is the appearance of Invisible God ( ni Kumfunua Mungu asiyeonekana kwa Macho ya kawaida)”.

✓✓ MHUBIRI WA INJILI

Mhubiri wa Injili lazima apititie vigezo hivi vitatu, k**a injili hiyo haiokoi pamoja na kuwa na elimu nzuri ya theolojia wewe ni lecturer tu (mkufunzi) unakaririsha watu NOTIS.

K**a injili haihusu Habari Njema za Ufalme wa Mungu, uwezo wa Kristo kubadilisha Maisha, wokovu, Nguvu ya kushinda ulimwengu, kushinda dhambi na takataka zingine za dunia, jitathimini mahubiri yako huenda hukutumwa, unajibebea Biblia na kusoma mathayo tu.

kuna mahali Mungu anagombana na wahubiri, kitendo cha kufahamu maandiko haina maana ubebe na kwenda KUHUBIRI popote tu, la! HASHA inahitaji kukaa na Mungu kwenye maombi kwanza, kupata maelekezo upeleke ujumbe gani.

Anasema “… sikuwatuma, … Ni heri wangalisimama katika baraza yangu, … ngaliwasikizisha watu wangu maneno yangu…” (YEREMIA 23:21-29)

K**a injili haimfunui Krsito na kuwasogeza watu kwa Mungu kuna kitu kimepelea, jitafakari mara nyingi Zaidi.

By the way, Hongera kwa kusoma ujumbe huu mpaka Mwisho, ruhusa Kushare baada ya kuuelewa Kwanza, endelea kufuatilia Ukurasa Huu, tutaendelea Sehemu ya Pili kuhusu "VIPAWA VINAVYOTUMIKA KATIKA INJILI".
[March 18, 2022]
© Paul Jeremiah 🌲

True
02/01/2022

True

02/01/2022

Inua mikono

12/02/2021

Jifunze acha uvivu

Address

Mkalama

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jesus Disciple Organisation J.D.O posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category