St.bosco Nursery School and daycare

St.bosco Nursery School and daycare ST.BOSCO NURSERY SCHOOL AND DAYCARE
,
St.Bosco ni kituo cha malezi ya mtoto wako ,Tunatumia

30/12/2025
30/12/2025

ST.BOSCO SCHOOL CHILDCARE AND KINDERGARTEN

Maono si tu kile unachokiona, bali kile unachokiamini kinaweza kutokeaST.BOSCO SCHOOL MASASI _0673285305
19/11/2025

Maono si tu kile unachokiona, bali kile unachokiamini kinaweza kutokea

ST.BOSCO SCHOOL MASASI _0673285305

UJUMBE WA LEO: USILALAMIKE, MUNGU ANAJUA ZAIDIKulikuwa na mtu mmoja aliyenusurika kwenye ajali ya ndege. Baada ya ajali ...
12/11/2025

UJUMBE WA LEO: USILALAMIKE, MUNGU ANAJUA ZAIDI

Kulikuwa na mtu mmoja aliyenusurika kwenye ajali ya ndege. Baada ya ajali hiyo, alijikuta ametupwa peke yake katika kisiwa kisicho na watu. Usiku alikuwa akitetemeka kwa baridi, lakini baada ya wiki mbili akiwa peke yake, alianza kujifunza jinsi ya kuishi porini. Alijifunza kuwasha moto kwa mawe, kuvua samaki, na kuwinda chakula.

Siku moja alipokuwa amevua samaki na kuwasha moto ili apike chakula cha jioni, alilala akiwa amechoka. Alipoamka usiku, alishtuka kuona hema alilojenga likiwa linateketea kwa moto. Kwa uchungu mkubwa alianza kulalamika:
“Mungu kwa nini mimi? Kwa nini mimi Mungu wangu? Kwa nini?”

Asubuhi yake, alipokuwa bado na huzuni, alisikia sauti ya kifaa kikubwa angani — ilikuwa helikopta! Ilipokaribia, marubani walimwona na wakamwokoa. Kwa mshangao aliuliza, “Mlijua vipi niko hapa?”
Wakajibu, “Tuliuona moshi mkubwa wa moto, tukajua lazima kuna mtu anahitaji msaada.”

Ndipo akatambua kitu kikubwa: wakati mwingine tunapolalamikia Mungu kwa mambo yanayotokea maishani mwetu, tunasahau kwamba huenda Mungu anatumia jambo hilo hilo kutuokoa au kutupeleka kwenye jambo bora zaidi.

Usilalamike kuhusu hali uliyo nayo leo — Mungu anaona mbali kuliko wewe. Kile kinachoonekana k**a hasara leo, kinaweza kuwa mlango wa baraka kesho

11/11/2025
06/11/2025

*KARIBU ST. BOSCO SCHOOL* *MASASI!_ 📞 0673 285 305*

Shule ya Malezi na utoaji elimu Bora kwa Mtoto Wako.

*Habari mpendwa mzazi* 👋

Uongozi wa St. Bosco School Masasi unapenda kukujulisha kuwa usaili wa watoto kwa muhula mpya wa masomo 2026 unaendelea.

Tunakaribisha watoto wenye umri kuanzia miaka 2 na kuendelea , kwa huduma ya malezi na elimu.

🎯 . *KWA NINI UCHAGUE ST. BOSCO SCHOOL?*
✅ Walimu wenye upendo, uzoefu, na ubunifu
✅ Mtaala wa Cambridge International school unaojenga maadili ,ubunifu na vipaji.
✅ Mazingira salama, safi, na rafiki kwa watoto
✅ Elimu bora kwa mfumo wa English Medium

*RATIBA YA USAILI*
Usaili unaendelea kila siku ya kazi (Jumatatu hadi Jumamosi)

🕘 Saa 2:00 Asubuhi – 9:00 Jioni

📍 Mahali: St. Bosco School, Masasi

Wazazi wanakaribishwa kufika shuleni kupata:
✅ Utaratibu wa usaili
✅ Maelezo ya ada na sare
✅ Mwongozo wa maandalizi ya sare za mwanafunzi

*KWA MAELEZO ZAIDI TUPIGIE, 📞 Simu: 0673 285 305*

“Mtoto wako anastahili mwanzo bora — St. Bosco ni mahali ambapo tunajenga msingi wa maarifa, nidhamu na kuibua ndoto za Mtoto WAKO .”

*MAHALI: REST CAMP MKOMAINDO*

💙 Karibu St. Bosco School –

Tuandae kesho bora ya mwanao 💙

Address

Mkomaindo
Masasi

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00
Saturday 08:00 - 17:00

Telephone

+255673285305

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when St.bosco Nursery School and daycare posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to St.bosco Nursery School and daycare:

Shortcuts

Share

Category