02/10/2025
MAKOSA YANAYOFANYWA NA WAFUGAJI WA KUKU (Broiler, Layers na Kienyeji)
Haya ni makosa yanayorudisha nyuma mafanikio ya wafugaji wengi wa kuku:
---
π 1. Kutofata Ratiba ya Chanjo na Tiba
Wafugaji wengine hawachomi chanjo kabisa.
Wengine wanachoma chanjo bila kufuata mpangilio sahihi au muda wake.
Matokeo: Kuku huathirika na magonjwa k**a Gumboro, Newcastle, Ndui, n.k.
---
π 2. Kutokufuata Usafi na Biosecurity
Banda halifagiliwi mara kwa mara.
Hakuna kuosha mikono kabla ya kuingia bandani.
Wageni wanaruhusiwa kuingia ndani ya banda bila tahadhari.
---
π 3. Kukosa Maarifa ya Msingi Kabla ya Kuanza Ufugaji
Wengi wanaanza kufuga bila elimu.
Hawajui jinsi ya kutambua magonjwa, kuchanganya chakula, au kuchagua vifaranga bora.
---
π 4. Kutumia Chakula Kisicho na Ubora
Wengine hununua chakula cha bei rahisi bila kuangalia virutubisho ndani yake.
Au wanachanganya chakula bila verterinari au mtaalamu wa lishe ya kuku.
---
π 5. Msongamano Mkubwa Bandani
Kuku wanawekwa wengi sana kwenye banda dogo.
Hii huongeza magonjwa, kupigana, kudonoana, na vifo.
---
π 6. Kutozingatia Muda wa Mwanga (Layers na Kienyeji)
Hasa kwa layers, mwanga ni muhimu kwa utagaji.
Wengine hawatumii taa usiku au hawajui muda sahihi wa kutoa mwanga.
---
π 7. Kutotambua Haraka Dalili za Magonjwa
Dalili k**a kukaa, kutetemeka, macho kufunga, au kuharisha huzingatiwa wakati kuku tayari yupo taabani.
---
π 8. Kuchanganya Makundi ya Kuku wa Umri Tofauti
Hii hupelekea kuambukizana magonjwa, hasa vifaranga kuwa katika hatari kubwa.
---
π 9. Kutofanya Kumbukumbu
Wengi hawana daftari la rekodi za:
Chanjo
Ugonjwa
Mapato na matumizi
Vifo na uzalishaji
---
π 10. Kutotenga Muda na Banda
Wafugaji wengine hawatembelei banda mara kwa mara.
Wanategemea wafanyakazi pekee, hali inayosababisha uzembe au wizi wa mayai/chakula.
---
π 11. Kufuga Bila Lengo Maalum (Commercial Focus)
Wengine hufuga bila kujua wanauza lini, kwa bei gani, au wanamlenga mteja