Kwale Secondary School

Kwale Secondary School Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Kwale Secondary School, School, Korogwe.

25/05/2024

Ahsante sana mama yetu Samia Suluhu Hasan Kwa kutuletea mradi wa madarasa manne na matundu nane ya vyoo. Mungu akulipe na akuepushe na Kila baya la Dunia hii. Pichani ni kuanzia hatua za kusafisha eneo hadi kupaua. Kwa upande wa madarasa na hatua ya msingi Kwa upande wa vyoo.

Matokeo ya kidato cha nne-2017
11/02/2018

Matokeo ya kidato cha nne-2017

Matokeo ya kidato cha pili-2017
11/02/2018

Matokeo ya kidato cha pili-2017

Heshima ya Kwale sec. imeanza kurudi. Matokeo ya Mock Mkoa iliyofanyika May-2017 tulikuwa wa kwanza kwa ngazi ya WILAYA....
10/09/2017

Heshima ya Kwale sec. imeanza kurudi. Matokeo ya Mock Mkoa iliyofanyika May-2017 tulikuwa wa kwanza kwa ngazi ya WILAYA...........Matokeo ya mock Wilaya iliyofanyika Agosti-2017 tumendelea kushika namba moja kwa ngazi ya wilaya. Tuwaombee watoto wetu wafanye vizuri zaidi kwenye mtihani wa Taifa.

Nimepata fursa ya kwenda kwenye maonyesho ya mkoa wa Tanga kwa kupitia onyesho letu la kutengeneza SABUNI. Nilichojifuza...
04/05/2017

Nimepata fursa ya kwenda kwenye maonyesho ya mkoa wa Tanga kwa kupitia onyesho letu la kutengeneza SABUNI.

Nilichojifuza:

Kwa upande wa walimu:-

Nimegundua Taifa linajengwa na watumishi wenye moyo kwelikweli,wanaoyatoa maisha yao kwa ajili ya TAIFA lao. Ukiona mtu kachaguliwa kuwa mkuu sehemu fulani. Huyo ni MASHINE tata, k**a huamini mfuatilie, atakuwa amefanya MAAJABU kwelikweli. Ukipewa UKUU kwa upendeleo huwezi kufika mbali, lazima UTAKERA watu.

Ni lazima MTUMISHI makini ajiulize nimeifanyia nini KWALE SEKONDARI, mf. Nimefanya mpango wa kuanzisha DUKA la kwale ss, lazima watu wakutambue, huyo aliyeacha familia yake akaamua kuanzisha DUKA la Kwale ss ni nani? .......Huyo kweli anaipenda KWALE. Uwalimu ni zaidi ya kufundisha. Wakati unafikiri utaifanyia nini KWALE SS, yupo anayefikiria ataifanyia nini WILAYA, mwingine anafikiria ataufanyia nini MKOA, mwingine anafikiri atalifanyia nini TAIFA. Ndiyo maana watumishi wengine wananyofolewa wakafanye majukumu mengine........... Hakika nimeona watanzania wanaofanya MAAJABU.

Kwa upande wa wanafunzi nilichojifunza:-

Elimu yetu ya TANZANIA nilifikiri ipo KINADHARIA zaidi kuliko kivitendo, sio kweli, elimu iko vizuri sana. Inapaswa wanafunzi WAJIONGEZE. mf. Shuleni umefundishwa ukichanganya SUKARI,MAJI na MAJANI unapata CHAI. Jukumu lipo kwa mwanafunzi, inatakiwa akifika NYUMBANI afanye jaribio. Aone kweli anapata CHAI? Taifa linajengwa na hao hao wanaojaribujaribu.

Nitafurahi sana endapo KWALE SS itafanya mapinduzi ya kifikra. Tuipende shule yetu. Umeme upo, tunatamani kweli kuwa na stationary ya KWALE SS, tujiuzie vitu muhimu vya ofisini, wanafunzi wasihangaike kwenda mjini kununua mahitaji yao, tuburuze mitihani hapahapa shuleni lakini mwisho wa siku mfuko wa SHULE utune.

Tunahitaji mabweni ( bweni la wasichana na lingine la wavulana) angalau tuanze FORM2 na FORM4 wakae shuleni. Yote haya yanahitaji watu wanaokimbia KIFIKRA sio wanaotambaa.

Kwale sekondari ilianzishwa kwenye mazingira magumu. Majengo haya ya Madrasa ndiyo yaliyoanza kutumika.
13/03/2017

Kwale sekondari ilianzishwa kwenye mazingira magumu. Majengo haya ya Madrasa ndiyo yaliyoanza kutumika.

Address

Korogwe

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kwale Secondary School posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category