Walimu na Ualimu

Walimu na Ualimu Walimu na Ualimu inawezesha upatikanaji wa Maarifa kwa Walimu na Wadau wa Elimu ili kusaidia uboreshaji wa Elimu na mchakato wa kujifunza na kufundisha.

Elimu ni nyenzo muhimu katika kuimarisha ustawi wa jamii kwa kuwa na maarifa sahihi ya jambo. Maendeleo katika jamii yeyote yanahitaji elimu bora ili Wananchi wake waweze kushiriki kikamilifu katika kutatua na kupambana na changamoto mbalimbali zinazowakabili kila uchao. Uandaaji wa Walimu unahitaji uwepo mzuri wa vifaa vya kufundishia, vitabu, njia bora na mazoezi ya kutosha. Kuliona hilo Gunda F

oundation imeandaa ukurasa huu ili walimu tarajali na wale walio kazini waweze kuutumia kupata baadhi ya mambo ambayo kwa namna moja au nyingine yatasaidia katika ufanisi wa masomo yao na kazi zao kwa ujumla. Usisite kutembelea ukurasa huu mara kwa mara kwani patakuwepo na mambo muhimu ya kujifunza. Aidha k**a utakuwa na Maswali au dukuduku lolote tafadhali usisite kutuandikia kupitia anuani zetu hapo chini. Mingoni mwa mambo yatakayokuwa yakijadiliwa kwa undani na ufasaha ni pamoja na namna bora ya;
∗ kuandaa Maazimio ya kazi na Maandalio ya Somo;
∗ kufuata Hatua za somo katika ufundishaji;
∗ Ujuzi na Maarifa ya Somo;
∗ Njia na Mbinu za kufundishia;
∗ Ufaraguzi na Matumizi bora kwa Vifaa vya kufundishia;
∗ Namna ya kujieleza;
∗ Matumizi ya ubao;
∗ Utoaji wa Kazi kwa wanafunzi;
∗ Kudhibiti Nidhamu ya Darasa;
∗ Haiba ya Mwalimu;
∗ Utoaji wa Maoni kuhusu somo;
Usikose safu hii tembelea mara zote ujipatie maarifa na taarifa za kielimu.

Habarini Ndugu Walimu,Kutokana na Maombi Mengi ya Wadau wa Elimu, tumeamua kulirudisha Kundi la WHATSAPP la Walimu na Ua...
12/01/2025

Habarini Ndugu Walimu,

Kutokana na Maombi Mengi ya Wadau wa Elimu, tumeamua kulirudisha Kundi la WHATSAPP la Walimu na Ualimu - Elimu Msingi.

Lengo ni kupata taarifa, kujifunza mbinu na njia mbalimbali za kuimarisha ujifunzaji na ufundishaji ikiwa ni pamoja na kuimarisha mshik**ano. Karibuni sana,

Jiunge sasa kwa kubofya link hii hapa chini:

https://chat.whatsapp.com/CPkIPk8wFbV5zFS0s0kT94

Leo Terehe 25/11/2024, Mkurugenzi Elimu ya Ualimu Mhe. Huruma Mageni amefanya Uzinduzi wa Vitabu vya Ziada katika Vyuo v...
25/11/2024

Leo Terehe 25/11/2024, Mkurugenzi Elimu ya Ualimu Mhe. Huruma Mageni amefanya Uzinduzi wa Vitabu vya Ziada katika Vyuo vya Ualimu nchini, hafla iliyofanyika katika Chuo cha Ualimu Korogwe, Tanga.

11/07/2024
Kutoka OR-TAMISEMI Jumla ya watahiniwa 1,384,340 wameanza mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi nchini huku idadi ya ...
05/10/2022

Kutoka OR-TAMISEMI Jumla ya watahiniwa 1,384,340 wameanza mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi nchini huku idadi ya watahiniwa kwa mwaka 2022 ikiongezeka ukilingalinisha na mwaka 2021 ambapo jumla ya watahiniwa walikuwa 1,132,084 sawa na ongezeko la watahiniwa 252,256 katika mwaka huu. Naibu Katibu Mkuu (Elimu OR - TAMISEMI) Dr. Charles Msonde Hayo yamebainishwa Septemba 5,2022 na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu Dr....

Kutoka OR-TAMISEMI Jumla ya watahiniwa 1,384,340 wameanza mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi nchini huku idadi ya watahiniwa kwa mwaka 2022 ikiongezeka ukilingalinisha na mwaka 2021 ambapo ju…

Leo 05-10-2022 ni siku ya Walimu Duniani, Tunawatakia kheri na fanaka Walimu Wote.
05/10/2022

Leo 05-10-2022 ni siku ya Walimu Duniani, Tunawatakia kheri na fanaka Walimu Wote.

Kwa habari za Elimu, Ualimu na Walimu fuatilia ukurasa huu ili ujifunze mambo mbalimbali pia tembelea ukurasa wetu wa Yo...
05/10/2022

Kwa habari za Elimu, Ualimu na Walimu fuatilia ukurasa huu ili ujifunze mambo mbalimbali pia tembelea ukurasa wetu wa Youtube (www.youtube.com/jiandae) kwa Mafundisho ya Kukujengea ufundishaji bora. WhatsApp?: 0674141209.

https://jiandae.wordpress.com/2022/10/05/bashungwafuatilieni-malalamiko-ya-posho-za-kujikimu-kwa-waajiriwa-wapya/

Kutoka: OR –TAMISEMI (page) Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amemuagiza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI anaye…

Timu nzima ya Walimu na Ualimu tunawatakia kila la kheri vijana wetu ambao wanaenda kuanza Mtihani wao wa kumaliza Daras...
04/10/2022

Timu nzima ya Walimu na Ualimu tunawatakia kila la kheri vijana wetu ambao wanaenda kuanza Mtihani wao wa kumaliza Darasa la Saba leo tarehe 05/10/2022.

Mungu awe pamoja nanyi, awafanyie wepesi myakumbuke yote mliyojifunza na wote mpate kufaulu mitihani yote, Amen.

Hellooo, Habari Njema kwa Wanafunzi wa Ualimu Ngazi ya ChetiTumeandaa Group la WhatsApp litakalokua linatumika k**a njia...
30/09/2022

Hellooo, Habari Njema kwa Wanafunzi wa Ualimu Ngazi ya Cheti

Tumeandaa Group la WhatsApp litakalokua linatumika k**a njia ya kuwasaidia Walimu Tarajali na Masomo yao Vyuoni.

Huduma tutakazotoa ni;
1. Maswali na Majibu
2. Maswali ya Kujipima
3. Video mbalimbali za masomo ya kufundisha
4. Mijadala ya Kielimu

Tunawakarobisha.
Tumia hio code za QR scan kwa kutumia cm yako ili kujiunga na Kundi la Walimu na Ualimi.

Address

533
Korogwe
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Walimu na Ualimu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share