21/07/2021
Kipindi cha ujana kinachukua hatua ya kipekee katika maisha ya kila mtu.
Ni kipindi cha mpito kutoka utoto hadi utu uzima. Vijana wengine huyamudu mabadiliko haya kwa mafanikio wakati wengine wanapata shida kubwa na kujikuta wanajihusisha na tabia ambazo zinahatarisha ustawi wao hasa wakiwa Shuleni ikiwa ni pamoja na Wasichana kupata mimba katika umri mdogo na bila kutarajia na Wavulana kujiingiza katika makundi ya mienendo mibovu.
K**a Vijana wanahitaji kupata malezi sahihi kutoka kwa Wazazi na Jamii kwa ujumla ili kuwawezesha kufikia ndoto zao Kielimu.
Elimu ya Afya na Uzazi ni Elimu sahihi inayohitajika kumfikia kila kijana ili kumpatia taarifa sahihi zinazomuwezesha kufanya maamuzi sahihi na kumsaidia kupambana na changamoto mbalimbali za makuzi ya ujana.
Korogwe Five ni mradi wa Jamii unaofanya kazi na jamii, shule za sekondari na Vyuo vya Ualimu ili kuboresha Ufikiaji na Utoaji Bora wa Elimu ya Afya ya Ujinsia na Uzazi.
Ukiwa k**a mdau tunakukaribisha kushirikiana nasi kwa kadiri utakavyoweza.
Karibuni sana | Like and Share Ukurasa WETU. Asante