Namirah Islamic Seminary Secondary School

Namirah Islamic Seminary Secondary School Namirah Islamic ni shule ya kiislamu, kwa wavulana na wasichana , kutwa na bweni. Shule ipo Korogw

13/05/2026
13/05/2026





06/05/2026

*MAELEZO YA GULIO LA BIDHAA ZA UBUNIFU*
*KWA WANAFUNZI WA MASOMO YA BIASHARA*
*SHULE YA NAMIRAH* *ISLAMIC SEMINARY SECONDARY SCHOOL*

Gulio la bidhaa za ubunifu ni shughuli ya *kielimu* inayolenga kuwajengea wanafunzi wa masomo ya Biashara ujuzi wa vitendo katika kubuni, kuandaa na kuuza bidhaa au huduma mbalimbali. Shughuli hii inatekelezwa kwa kuzingatia mwelekeo mpya wa *mtaala wa masomo ya Biashara pamoja na maboresho ya mitaala ya amali,* ambayo yanasisitiza zaidi ujifunzaji kwa vitendo *(competence-based learning).*

Kupitia gulio hili, wanafunzi wanapata fursa ya:

●Kuibua mawazo ya kibiashara (ubunifu na ujasiriamali)

●Kutengeneza bidhaa au huduma kwa kutumia rasilimali zilizopo

●Kujifunza mbinu za masoko na mauzo

●Kukuza uwezo wa kupanga bei, kufanya mahesabu ya faida na hasara

●Kujenga stadi za mawasiliano na huduma kwa wateja

Aidha, gulio hili linawasaidia wanafunzi kuunganisha nadharia wanazojifunza darasani na hali halisi ya soko, hivyo kuwaandaa kuwa *wajasiriamali* na watendaji bora katika jamii.

Shughuli hii ni sehemu muhimu ya utekelezaji wa mtaala mpya unaolenga kumjenga mwanafunzi mwenye ujuzi, ubunifu, na uwezo wa kujitegemea.

*Wazazi, Walezi na wadau,* MNAKARIBISHWA kuja kujionea na kufanya manunuzi ya bidhaa za Ubunifu siku ya *GULIO*. INSHALLAH {mtajulishwa}. Pia tutakuja pia na maonesho ya ubunifu wa *kisayansi na Kisanaa* Inshallah.

  ‘     .Kwa heshima na furaha kubwa, napenda kuwapongeza nyote katika maadhimisho ya   ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi...
01/05/2026

‘ .

Kwa heshima na furaha kubwa, napenda kuwapongeza nyote katika maadhimisho ya ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi. Tunatambua kwa dhati mchango wenu mkubwa katika kuendeleza elimu yenye maadili ya Kiislamu, kujenga tabia njema kwa wanafunzi, na kusimamia majukumu yenu kwa uaminifu na kujituma.

Kazi mnayoifanya si tu ajira, bali ni ibada yenye malipo makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Kila juhudi mnayoweka katika malezi, nidhamu, na utoaji wa elimu bora ni sehemu ya sadaka yenye kuendelea.

Nawahimiza kuendelea kufanya kazi kwa bidii, uadilifu, na mshikamano, tukilenga kuleta mabadiliko chanya katika jamii kupitia elimu ya Kiislamu.

Mwenyezi Mungu awabariki katika kazi zenu, awaongezee afya njema na mafanikio zaidi.

_Heri ya Sikukuu ya Wafanyakazi!_

S.O Mwangu.

22/03/2026

Nasaha za Mkuu wa Shule Kwa

na
wote

09/12/2025

#“Amani ni msingi wa mafanikio ya mwanafunzi.”

“Shule yenye amani hujenga wahitimu wenye hekima.”

“Heshima, upendo na ushirikiano ndiyo njia ya kudumisha amani miongoni mwa wanafunzi.”

“Tuchague amani ili tuendelee kusoma kwa utulivu.”

Address

Korogwe

Telephone

+255659320365

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Namirah Islamic Seminary Secondary School posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to Namirah Islamic Seminary Secondary School:

Shortcuts

Share

Category