Kanawa Primary School

Kanawa Primary School This page create with the aim of reconnecting former workers and students of Kanawa primary school,

15/04/2018

C&P
______________________________
Wanaume wenzangu, tufanye kazi kwa bidii tutafute hela ili uzee wetu tuwe na uwezo wa kujitegemea. Hakikisha kwenye uzee wako una pesa zako mwenyewe za kukufanya usurvive. Sahau kuhusu watoto, na mama yao kwamba watakutunza. Wewe ndiye stranger pekee kwenye hiyo familia unayoiita ya kwako. Hiyo nyumba ni ya huyo mwanamke na watoto wake. Not yours.!

Babu yangu aliniambia kwamba mwanaume aliyeoa ni sawa tingatinga, ambalo linatengeneza barabara, lakini ikishakamilika linabebwa juu juu kwenye lori na kuondolewa, eti likitembea litaharibu barabara. Yani barabara ambayo tingatinga lenyewe limeitengeneza haliruhusiwi kutembea juu yake.

Vivyo hivyo kwa mwanaume aliyeoa. Atajinyima, atajishughulisha, atajizuia kufanya anasa, atakopa, atavaa mitumba ili tu watoto wake waishi vizuri, wale vizuri na kusoma shule nzuri. Siku hizi urithi pekee uliobaki ni elimu bora coz mashamba ziliishaga. Lakini pamoja na yote hayo, bado ukizeeka hao watoto sio wako, ni wa mama yao. Wewe watakuita "kamzee".

Watoto wakiwa na umri wa miaka 10 ndipo mama yao anaanza kuwajaza taarifa zisizovutia kuhusu wewe. Kadri wanavyokuwa ndivyo wanavyoelezwa mambo mengi. Wakifika utu uzima atawaambia "isingekua mimi hamgesoma, yeye alikua ni pombe tu na wanawake" Ukisikia hivyo ujue tingatinga limemaliza kazi yake sasa linakaribia kuondolewa barabarani.

Watoto wanapoanza kazi, mzee anakua amestaafu. Wanapokuja kutembelea wazazi, wakiondoka wanampa baba elfu 5 mbele ya mama. Halafu wanaenda jikoni na mama, wanampa hela kwa siri bila mzee kujua. Wakiondoka mama anamfuata mzee na kumwambia sukari imeisha. So ni suala la mzee kuamua kutoa ile elfu 5 aliyoachiwa na watoto ikanunue sukari, otherwise anywe chai isiyo na sukari. Hii ni moja ya sababu inayowafanya wazee kufa mapema baada ya kustaafu na kuacha wake zao wajane.

Nimeshuhudia wazazi wenye watoto ng'ambo wakimchukua mama yao akaenjoy life majuu, na kumuacha baba yao nyumbani akilisha ng'ombe zao mbili, na kutafuta chakula cha kuku.!

Wanaume work hard and save something for yourself at old age. Tafuta pesa kwa bidii, wape watoto elimu bora, wape mahitaji yao muhimu, jenga nyumba nzuri waishi vizuri, lakini ukizeeka dont expect too much from them. Enjoy maisha ya uzee kwa pesa zako mwenyewe ulizochuma ujanani. K**a huna hela utaumwa hata na mbwa yako mwenyewe.!!

Likizo kwa kheri...Majukumu karibu...Ualimu twaupenda ...Chaki tumezimiss....Hatimaye kesho tutazishika tena...Mwaka mpy...
08/01/2017

Likizo kwa kheri...
Majukumu karibu...
Ualimu twaupenda ...
Chaki tumezimiss....
Hatimaye kesho tutazishika tena...
Mwaka mpya wa masomo unaanza kesho mola atuongoze tufikishe hili jahazi salama salimini

20/08/2016
19/06/2016

DEAR LADIES
1. Ngono haimfanyi mwanaume asikuache, hata
ukukuruke vipi, jikwatue kiasi gani k**a hajaona quality
za kuwa mke atakuacha tu.
2. Mwanaume anaekupata kwa vile alitumia pesa zake
kwako hatakaa na wewe milele. Wanaume halisi
hawawezi wakatoka na wanawake feki wanaopenda
pesa. Ukibahatika sana atakufanya daraja la pili yaani
mchepuko!
3. Uzuri wa mwanamke unaweza ukampelekea
akaolewa ila tabia yake ndio itakayoamua ni kwa muda
gani atadumu katika ndoa. Uzuri huvutia wanaume, ila
tabia hufanya wanaume wadumu na wewe.
4. Pesa kiukweli ina faida sana na ni muhimu kwa mtu
yoyote kuwa nayo ila pesa peke yake haiwezi kuleta
ukweli wa maana halisi ya furaha na maisha.
6. Kuwa mzuri bila tabia njema hakuwezi kukakupa
mume bora, sana sana utapata Boyfriends na wanaume
za watu.
6. Tendo la ngono linaleta faraja ila haliwezi kuleta
upendo. S*x ni zao la mapenzi, mapenzi sio zao la s*x.
7. S*x inaweza kufanya mwanaume alale na wewe
usiku kucha, na asubuhi akaondoka zake ila upendo
hufanya mwanaume aishi na wewe daima.
8. Kuna mambo mengine pesa haiwezi nunua k**a
tabia na heshima, k**a ulikubali kuolewa nae kisa
pesa zake. Usidhani kupitia pesa zake ataweza
badilika.
9. Uvaaji wako siku zote ndio utakaoamua ni nini
wanaume wazungumze na wewe!
Ni ukweli fulani hivi ambao ni mchungu!

18/06/2016

Ratiba ya uhakiki ni k**a ifuatavyo
Tarehe 20 tarafa ya kishapu,
Tarehe 21 tarafa ya negezi (ukenyenge),
Tarehe 22 tarafa ya mondo (mipa)

Bitu vinavyohitajika ni
pasport size moja
kitambisho cha kazi original na copy
salary slip december 2015 - march 2016

mnasisituzwa kuwambusha watumishi wa idara zenu na vitengo

21/05/2016

k**a kuna mwana member tafadhali mu-add kwa page hii ,, niya wanakanawa woooote

Kanawa on the move
21/05/2016

Kanawa on the move

17/05/2016

kesho ni ck nyingine tena ..... vijana wa drs la sita watakuwa na mtihani wa kitaifa kupima uwezo wao......dua na sara zetu kwetu.....Mungu awatangulie

09/05/2016

kesho kuna ukaguzi wapendwa tuwe tayari kwa lolote

Address

Negezi/ukenyenge
Kishapu
1288KISHAPU

Opening Hours

Monday 07:30 - 14:30
Tuesday 07:30 - 14:30
Wednesday 07:30 - 14:30
Thursday 07:30 - 14:30
Friday 07:30 - 14:30
Saturday 02:00 - 18:30
Sunday 02:00 - 18:30

Telephone

+255657764101

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kanawa Primary School posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to Kanawa Primary School:

Shortcuts

Share

Category