02/06/2025
Siku ya jumamosi Mei 31, 2025 tulifanikiwa kuwa na Dkt. Benny Kimaro, Daktari Bingwa wa uzazi na magonjwa ya wanawake kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili.Tuliweza kujifunza kuhusu hedhi salama na mabadiliko yanayotokea kwa mwanamke/binti wakati wa hedhi. Pia tulipata nafasi ya kuwa na mjadala huru kuhusu hedhi na nafasi ya wanaume kwenye kutoa elimu ya hedhi.
Shukrani zetu ziende Kwa Dkt. Benny Kimaro, waratibu wa mdahalo ambao ni waelimishaji rika kutoka SAUT na IRDP Mipango Mwanza. Pamoja na wasimamizi na waandaji Vijana Mabalozi wa miradi ya Elimu kwa Afya na Ustawi UNESCO.