21/02/2022
Mjue Dr. Mark Dean....... Huyu ni mwanasayansi ama mhandisi wa teknolojia ya kompyuta .. ndiye alieweza kuunda kompyuty za desktop na kuzileta majumbani.. na pia ndiye mtengenezaji wa kwanza wa "circuit" zilizotumika kuunganisha "printers" na "moderms" . Dr. Dean aliongoza timu ya wahandisi waliotengeneza kifaa kidogo cha kuhifadhia kumbukumbu kwenye kompyuta chenye ukubwa wa "gigahertz" moja (1_gigahertz chip?) Kilichokadiriwa kuwa na uwezo wa kukokotoa mahesabu bilioni kwa sekunde moja na baadae aliweza kugundua na kuunda mfumo bora wa kompyuta yenye ubora zaidi kuliko zote duniani uliokuwa na uwezo wa kukokotoa mahesabu zaidi ya trilioni kwa sekunde moja( world's most powerful supercomputer systems). Katika kugundua na kuunda teknolojia hii .. aliwahi kusema... " K**a unaweza kuzungumza kuhusu hicho, ina maana unakiweza" " if you can talk about it, that means it's possible" lakini pia aliwahi tania akisema " k**a hatutatatua tatizo hili , baadhi ya bidhaa zetu zitatumika kupikia na kukokotolea kwa muda huo huo" " if we don't solve this problem, some products coul be used for cooking as well as computing" .
Kwa sasa Dr. Dean anaongoza maabara za utafiti wa kisayansi unaolenga kuvumbua mawanda mapana ya vikokotozi duniani.. ambavyo vina "range" kutoka uwezo mdogo hadi uwezo mkubwa zaidi.. lakin pia wanajaribu kutafuta njia bora za kutumia vikokotozi katika kurahisisha biashara na maidha kwa ujumla.... Na Dr. Dean siku hizi anatumia msemo.. " k**a ukifanya kazi kwa bidii, unaweza kuwa vyovyote utakavyo . Maana panaweza kuwa na vizuizi lakini hakuna mwisho" " If you work hard, you can be whatever you want to be. There may be obstacles , but there are no limits"...
Tunajifunza nini kupitia huyu mwanasayansi mashuhuri duniani katika teknolojia tunayoitumia hata sasa? K**a taifa tufanye nini ili maarifa tuliyonayo ambayo hayajawahi kutumika kufanya jambo lolote yatumike na yafanye jambo?
Mungu mwema ametupa akili , uwezo na ubunifu...k**a alivyo Dr. Dean Ndivyo tulivyo na sisi....mafanikio yanaanza na wewe..Anza..