14/09/2024
KANUNI ZA MAISHA KATIKA KUWAJIBIKA MBELE ZA MUNGU (Lk. 11:9-10)
1. Kupewa kwa kuomba
2. Kupata kwa kutafuta
3. Kufunguliwa kwa kubisha
1. Usipoona matokeo ya maombi yako, chunguza wapi maombi yako
2. Maombi ni mawasiliano yanayotengeneza mahusiano ya mtu na Mungu.
3. Boresha mahusiano hayo kwa kuwasiliana na Mungu kwa njia ya maombi.
4. Maombi hujenga mahusiano baina ya mwanadamu na Mungu. Maombi ni kiungo, ni daraja la kumfikia Mungu.
5. Usichoke maombi kwakuwa ukiacha adui atapanda uharibifu ndani ya maisha yako (Mt. 13:25)
6. Huu ni wakati ambao Mungu amekupa ili uweze kumtafuta kwa bidii kwakuwa utamwona. (Yak. 4:8)
7. Unahitaji kuwa na nguvu ili kupata mambo yaliyoko katika Ufalme wa Mungu (Mt. 11:12) kwa Kusoma Neno, Kuomba, Utakatifu na kuishi katika haki.
8. Faida ya kutafuta Ufalme wa Mungu kwanza ni kupata FURAHA, AMANI NA MEMA (Rum. 14:17)
MAMBO YANAYOZUIA MAOMBI YASIJIBIWE
1. Kutokuomba kwa bidii
2. Kuomba kinyume na mapenzi ya Mungu (Yak. 4:3)
3. Dhambi/Uovu (Yh. 9:31)
4. Mazuio ya Ufalme wa Giza (Dan. 10:12)
MAMBO YA MUHIMU KUTAFUTA/VIPAUMBELE
1. Ufalme wa Mungu na haki yake (Mt. 6:33-34; Rum. 14:17-18)
2. Uso wa Bwana (Zab. 105:4)
3. Unyenyekevu (Sef. 2:3)
4. Kuwa na amani na watu wote (Ebr. 12:14)