21/07/2024
Wanafunzi waliomaliza Shule ya msingi Mkoani mwaka 1996 wametimiza ahadi yao waliyotoa tarehe 3.2.2024 kwa kuikabidhi uongozi wa shule Kompyuta Tano zitakazosaidia katika ujifunzaji na ufundishaji kwa wanafunzi na walimu.
Aidha Mwalimu mkuu Adelhema Shawa kwa niaba ya wafanyakazi wa Shule ya msingi Mkoani amewashukuru sana wanafunzi hao kwa uzalendo waliounyesha kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji kwa njia ya TEHAMA.