Afya Ya Mahusiano

Afya Ya Mahusiano Elimu ya mahusiano. Hatua ³ muhimu >>> ¹Urafiki | ²Uchumba | ³Ndoa.

29/09/2020

MAOMBI YA KAZI
~~ Nakuletea k**a nilivyoipata
👇👇

Anaandika Faza James,
_______________________
Wiki iliyopita nilipata nafasi ya kuchakata maombi ya kazi ya taasisi moja binafsi hapa nchini. Maombi takribani 450 yalipokelewa ya wahitimu wa vyuo mbali mbali.

Ninashauri tufikirie namna tunavyoweza kujipanga na kuelimishana namna sahihi ya kufanya maombi ya ajira. Yapo makosa madogo madogo yaliyofanya tuwatoe katika ushindani takribani 50% ya waombaji wote bila hata kuangalia CV au vyeti vyao.

Baadhi ya makosa niliyoyaona ni k**a ifuatavyo;

1. Emails nyingi zilitumwa bila heading. Yani email haisemi ni ya nini. Au mtu anaandika "Application", au anaandika "My cv", au "Dear sir". Hayo yote ni makosa. Kwa kawaida unapaswa kuandika heading ya email yako in a title cased format ikitaja nafasi unayoomba. Kwa mfano "Application for Tutorial Assistant in Mathematics"

2. Emails nyingi zilizokosewa heading. Yani heading na kilichomo ni tofauti. Mtu ameandika "Application for Tutorial Assistant in Mathematics" lakini ukifungua barua yake ya maombi ameomba nafasi ya Estate Manager. Mara nyingi hutokea ikiwa ofisi imetangaza nafasi zaidi ya moja.

3. Kulikua na "blank emails". Yani mtu ametuma email anasema "please see the attachments" lakini hajaambatanisha attachment hata moja.

4. Kuna mtu ametuma email yenye attachments tu bila kuandika chochote sehemu ya ujumbe. Hilo ni kosa. Andika sentensi mbili au tatu. Kwa mfano "Dear sir/Madam, please see my attached credentials applying for the Tutorial Assistant post"

5. Weka attachment ulizoelekezwa tu. K**a mwajiri anataka CV na Cover letter usiattach certificate unless awe anataka na certificate pia. Na hata ukiambiwa attach certificate weka zile za muhimu tu. Sio unaweka cheti cha primary, cha ubatizo au Living certificate ya form four/six.

6. Attachments zote lazima uzipe majina kabla ya kuattach. Mfano cv inatakiwa isomeke Peter Elia CV - Tutoria Assistant Post au vinginevyo ili mradi mtu akiidownload asihitaji kulazimika kui-rename. Elewa kwamba waombaji ni wengi na anayefungua hizo attachment ni mtu mmoja au wawili. Fanya maisha yawe mepesi. Hakuna mtu ana muda wa kufungua attachment yako na kuirename wakati wapo walioattach kwa kuzipa majina attachment zao.

7. Poor scanned documents. Tuache uvivu. Usiscan kwa kutumia simu ya mkononi. Andaa copy nzuri ya nakala ya vyeti vyako tumia scanner nzuri, na ikiwezekana save kabisa kwenye "email" yako ili siku yoyote ukivihitaji uvipate.

8. CV format. Kuna watu wanafanya utani na CV zao. Yani unakutana na CV ina font size tofauti kila section, font types tofauti, spelling errors hadi kwenye majina yako. Hapa ukikosa kazi huna wa kumlaumu.

9. Usitumie majina tofauti na yaliyopo kwenye vyeti vyako. K**a vyeti vyako vimeandikwa Peter Elia Mosha usiandike Peter Elia au Peter Mosha. Hao ni watu wawili tofauti.

10. Acha kutumia email uliyofungua ulipokuwa "teenager" enzi ukiwa na miaka 16. Unakuta mtu anaitwa Peter Elia lakini email yake ni [email protected] AU [email protected]. Tengeneza email yenye majina yako na isajili kwa majina yako halisi. Kwa mfano k**a unaitwa Peter Elia unaweza kutumia [email protected]

11. Usitumie email ya mtu mwingine kutuma maombi. Tuache uzembe. Yaani k**a natafuta mtu mmoja kati ya watu 450 niambie kwa nini nimchukue mtu ambaye hana hata email address? Tengeneza email yako na hakikisha unatuma maombi kwa email yako mwenyewe, sio email ya mtu. Siku hizi dakika 5 tu zinatosha kutengeneza email account.

12. Epuka kuchanganya herufi. Hata k**a una shida ya lafudhi, jitahidi iwe kwenye kuongea tu lakini sio kwenye kuandika. Mfano hela - ela, rejea - lejea, afadhali - afazali. Sasa hivi kuna mtindo mpya wa xa badala ya sa. Na hawakubali kurekebishwa. Mwisho wa siku utasikia "my wangu nimekutumia ujumbe mpaka xaxa ujanijibu jomoni"
_____
TAKE A SERIOUS NOTE. Maombi ya kazi ni jambo serious sio mambo ya JOMONI.!

28/09/2020

Miaka 6 ya Ndoa nilichojifunza so far...

1:Bado siamini ile ndana ya Ndoa ni ya mtu mmoja
( Wale wanaoweka emphasis kwa mwanamke tu, na kwamba Ndoa nzima inabebwa na mwanamke, naamini mwanamke ana nafasi kubwa kwenye Ndoa, ila Ndoa ya mke na mume ambao wote wanaitaka iyo Ndoa na kuifanya ikue, Ni Ndoa nyepesi na nzuri Sana)

2: Haijalishi unajua vitu kiasi gani kuhusu mahusiano, Haijalishi ni kiasi gani uko open minded, Haijalishi ni kiasi gani you are willing to extend an olive branch, haijalishi Ni kiasi you are willing to forgive, Haijalishi unajua Nini na umefundwa na kungwi au mama Mchungaji, Haijalishi, narudia Tena haijalishi, they only way, you are going to be truly happy and have a successful marriage, is if both of you, I mean both of you are willing to put the work.
If both of you love each other and respect each other as much.
If only both of you, are afraid of loosing that relationship as much.
If only both of you.

It's takes two to tangle.
There is a reason Ndoa ni ya watu wawili...

Vinginevyo, utakua msindikizaji katika maisha ya Ndoa, utasaidia mwenzie akue wakati wewe ukidumaa...utatengeneza chuki ndani yako towards your husband and all men utawaita mbwa.

Ombea ilo.

3:Ndoa za jinsia

Ndoa za jinsia, Ndoa zisizo na hisia
Ndoa tulizokulia, Ndoa tulizoziingia...

Bado siamini katika hii dhana pia.
Natamani tungepunguza K**a sio kuacha kabisa hii dhana.

Dhana ya kuweka urobot katika mwanamke na Umalaika katika wanaume.
Kwamba kwa kila wanachofanya wasamehewe kwakua ni Wanaume.
Na katika kila tunachofanyiwa, hatutakiwi kuweka emotions, ila kwakua sisi ni wanawake we deserve all the rubbish thrown to us.

Funny enough hata katika uzazi kipindi kigumu ambacho unahitaji all the support you can get, Bado unabidi ujikatae na mtu wa Kwanza unaesisitizwa kumkumbuka ni mwanaume.

Acheni kutumia hizi Gender shenanigans k**a fimbo.
Ndoa inabebwa na upendo..
Upendo ambao unaweza kukua au kupungua kutokana na namna mnaamua kuishi maisha yenu.
Ndoa inabebwa na hisia, hisia ambazo inabidi tuziheshimu na kuzijali.

Mwangalie mkeo K**a mtu unaempenda, na sio k**a mwanamke ambae jamii imeamua kumuweka sehemu Fulani.

Love is beautiful
Marriage life is magical
Tuache Ndoa za jinsia kwenye Ndoa.
You are what she is.
She reflects you, if you look at her and see a Gorrila, just know you are a Gorrila too.

( Hii topic ni ndefu, ila nitaishia hapa kwa Leo)

4: Choices.

Trust is a choice.
Love is a choice
Respect is a choice.
Cheating is a choice.

Kwa kila kitu tunachoamua kufanya na njia gani tunaamua kuchukua vyote viko ndani ya uwezo wetu.
You can choose to build or destroy.
Eg.
When I got married I made a choice to trust my husband, not influenced by anyone, I made that choice...not because I trust him 100%, and not because there hasn't been a time when I questioned that.
But I made a choice, a choice which I stand with.
That includes not going through his phone whether he is around or not.
Why because,
1)I believe he is grown man with sane mind.
2) I believe he respects what we have
3)I want his commitment to us to not be forced or influenced, I want him to make that decision.
Never regretted that decision, imenisaidia kutokukurupa, kuropoka au kufanya maamuzi mabaya.

5: usiruhusu negativity katika maisha yako ya Ndoa.
Kwasababu hata kwa udogo wake it can destroy, na positivity hata kwa udogo wake it builds.
Dhibiti Aina ya vitu unavyotaka kuona na kusikia..

6: Don't do things for her, Do things with her.

Ndoa nyingi wanaume hawafanyi vitu na wake zao.
Wanaweza kuwanunulia vitu, ila hawawezi kufanya nao maendeleo.
Tumelimit sana maana ya usaidizi.( Mke K**a msaidizi)
Nimechoka, kuandika😅😅😅...

Ok, nafupisha, wanawake wanahitaji kukua kiakiri na kifikra katika Ndoa, washirikisheni na muwafanye sehemu ya maisha yenu, ili mkue pamoja, na inasaidia kuongeza upendo na ukaribu wenu....

Kuosha vyombo, kupika na kufua, is not all there is to being a wife....

😅😅😅😅....

Love y'all...

Hayo ni maoni yangu tu, na sio sheria.😂😂😂



11/02/2020

Ni Ombi langu,
Mungu wangu akukumbuke na wewe.

08/01/2020

Umri haupimwi kwa idadi ya mvi wala makunyanzi usoni Bali Nini umefanya.

31/12/2019

2020 ukavikwe uwezo k**a TAI.
Nakutakia mafanikio mema unapouanza mwaka 2020.

24/12/2019

Kwenye maisha kuna vipindi viwili muhimu sana ambavyo unahitaji kuwa navyo makini ili USIPISHANE navyo.Katika kila LENGO,WITO,KIPAJI au UWEZO ambao MUNGU amekupatia kutakuwa na kipindi cha “KUFICHWA” na kutakuwa na kipindi cha “KUDHIHIRISHWA”.Hii ni kanuni ambayo kila mtu lazima aipitie.Ukisoma kwenye Biblia utakuta mahali pameandikwa “Na yule Mtoto akakua katika Nguvu na KUKOMAA Kiroho na akakaa JANGWANI hadi wakati WAKATI wake wa KUDHIHIRISHWA kwa Israel ulipofika”(Luka 1:80).
Moja ya presha ambayo utakutana nayo kwenye maisha yako ni kusukumwa UJIONYESHE kabla ya wakati wako.Kuna wakati kila anayekuzunguka ataona umechelewa KUWA vile anavyodhani unatakiwa kuwa,KUFIKA pale anapodhani unatakiwa kufika ama KUPATA kile wanachodhani ulitakiwa uwe UMESHAPATA.Kumbuka wakati WAO wa KUDHIHIRISHWA inawezekana ikawa ni wakati WAKO wa KUFICHWA.
Wakati ambao hauonekani k**a unapiga hatua haimaanishi HAUPIGI hatua:Inawezekana ni wakati wako wa Kufichwa ili Ujenge UWEZO unaotakiwa,ujenge TABIA muhimu na ujengewe MISULI itakayohitajika.Kumbuka hakuna kudhihirishwa hadi UMEKOMAA katika maeneo MUHIMU.
Inawezekana kila mtu anakuambia mbona wewe ndio unatakiwa upate kile cheo?Mbona wewe ndio unatakiwa kushika ile nafasi?Mbona wewe unatakiwa uwe umeshafanya hivi?Mbona umechelewa kufanya hiki?.Hapo ujue UNAKOMAZWA.
Maneno haya yasikufanye UANZE “kuforce” vitu ambavyo baadaye utavijutia kwenye maisha.Kumbuka unapokuwa wakati wa KUFICHWA ni wakati wa KUWEKEZA kwenye mambo muhimu YASIYOONEKANA na wakati wa kudhihirishwa ni wakati wa kila mtu KUONA ulichonacho,USICHANGANYE NYAKATI!
Usijilazimishe KUDHIHIRISHWA ikiwa ni majira yako ya KUFICHWA.Umeshawahi kupitia wakati wa KUFICHWA?
See You At The Top

20/12/2019

FURSA YA KAZI.

MAREKANI KUNA UHABA SANA WA MANESI.

WAMEAMUA KUANZA KUTEMBELEA AFRIKA KUTAFUTA WAFANYAKAZI.
JAPO KUNA GHARAMA NA MIPANGO MIREFU.

NIMEANZA MUDA KUFUATILIA NA KUWAJULISHA WENGI, MPAKA SASA NIMEPATA WATANZANIA WAWILI TU LAKINI WAKENYA MAELFU..
Inasikitisha.

JAMANI JAMANI😭😭 MPAKA KWENYE MAGROUP NAPOST MAADMIN HATA POST ZANGU HAWAPOST.

MWEZI WA NNE TUNAKWENDA KENYA KUWA INTERVIEW. ...

KWELI WA KUKOSA NI WA KUKOSA HATA AKICHANGIWA😭😭

Nitafute inbox WhatsApp No. 0653 100 100🙏 endapo Wewe unayo Degree kwenye Unesi

Naomba tuma/sambaza ujumbe huu.

Degree holder straight away without delays nitakuelekeza cha kufanya.
______________________________

HATA K**A WEWE HUNA DIGRII YA UNESI, MSHIRIKISHE MWENZAKO MWENYE DIGRII YA UNESI NAYE ATAKUSHUKURU SANA.

12/12/2019

ᴊɪғᴜɴᴢᴇ ᴋᴜsʜᴜᴋᴜʀᴜ ᴋᴀʙʟᴀ ʏᴀ ᴋᴜʟᴀʟᴀᴍɪᴋᴀ

Ali alirudi kutoka kazini akiwa amechelewa sana, kichwa kilikua kinamuuma sana na alitaka tu kupumzika, alipiga honi na mkewe kumfungulia geti,akaingiza gari kisha kuelekea moja kwa moja chumbani.

Aliingia chumbani na kuanza kuvua nguo, lakini kabla hata hajapanda kitandani kupumzika mkewe aliingia, alimuangalia na kuanza kuongea.“Hujasahu kitu wewe?” Mkewe alimuuliza kwa hasira, Ali alikua mtupu hakua akikumbuka kitu. “Yaani hukumbuki kabisa hivi k**a angekua Mama yako ungemfanyia hivyo kweli?”Mkewe aliongea kwa hasira, uso kaukunja. Hapo alikumbuka kitu alichokua amesahau, Mama mkwe wake alikua anaumwa amelazwa hospitali na siku ile aliruhusiwa hivyo mchana Ali alitakiwa kwenda kumchukua na kumleta nyumbani.“Yaani sisi ndiyo watu wa kusumbuka na Tax wakatiwewe upo, juzi Mama yako kaja hata alikua hata haumwi ukanipa gari nimzungushe kwa ndugu zako wote, hata sikulalamika wewe tu kwenda kumchukua Mama yangu hospitalini na kumleta hapa nyumbani unaona kazi?”

Ali alijua kwamba amekosa, nikweli aliahidi kwenda kumchukua Mama mkwe wake lakini alikua amesahau kabisa, alishindwa hata chakuongea kwani alijua mkewe atazidi kukasirika.
Aliomba sana msamaha lakini mkewe hakumsikia, alitoka na kumuacha. Usingizi wote uliisha ikabidi kutoka na kwenda kumsalimia Mama mkwe wake.

Alimuomba msamaha kwa kushindwa kwenda kumchukua hospitalini. “Mwanangu msamaha wa nini, mbona tumekuja vizuri, yaani mwanangu uache kazi zako uje unichukue wakati magari mjini yapo mengi..”Mama mkwe alionyesha kumuelewa, lakini bado Alialijisikia vibaya kwa kile kitendo. Hakudhamiria lakini kuna matatizo yalitokea ofisini yakamfanya kusahau hata k**a kuna mgonjwa.

*****“Si heri hata ungenipigia simu nikajua, lakini wala na simu umezima kabisa!” Mkewe aliendelea kulalamika wakati wa chakula.Hapo ndipo Ali alipostuka kua kumbe hata simu yake ilikua ishazima chaji muda mrefu, alijaribu kujielezea lakini mkewe hakuelewa.Wakati huo Mama mkwe alikua amelala kwenye kochi pale sebuleni akiangalia TV.

Aliwaacha wazozane bila kusema chochote.Baada ya chakula waliingia ndani na mkewe alimuingiza Mama yake chumbani. “Mwanangu mbona mume wako kashakuomba msamaha, kwanini usimsamehe…”“Hapana Mama amezidi, angekua Mama yake angemsahau hospitali, tena anatuzimia na simu kabisa..”“Lakini mwanangu si tumefika salama, hembu achahaya mambo. Utaharibu ndoa yako bure!”“Naiharibike, hawezi kukudharau wewe Mama yangu, mbona wakwake hamdharau, Mama yake akija hapa nikuzungushwa na gari k**a mfalume lakini wewe unaumwa hata kukuchukua hospitalini hataki?”Mkewe aliongea sana mpaka Mama yake alimua kunyamaza, wakati anatoka chumbani Mama yake alimuomba kalamu na karatasi.Alimuuliza ni za nini akamuambia hapana ampe tu, kuna kitu anataka kuandika. Mkewe aliondoka na kwenda kumletea Mama yake kalam na karatasi kisha akaenda chumbani kwake kulala.

******Asubuhi mke wa Ali alikua bado kanuna, hivyo waliagana bila hata mumewe kunywa chai. Baada ya kuondoka mkewe aliingia chumbani kwa Mama yake kumuangalia.Alimkuta ameshaamka, walisalimiana kisha Mama yake akamkabidhi kakaratasi na kumuambia aende akasomee chumbani kwake, haraka haraka alitoka na kuenda chumbani kwake.Alikafungua ile kakaratasi na kisha kuanza kusoma, ilikua imeandikwa.

MAMBO ALIYONIFANYIA MUMEO TANGU NIANZE KUUMWA.
1. Alikuja kijijini na gari kunichukua, angeweza kunitumia tu nauli lakini akasema hapana, Mama hawezi kupanda basi, akachukua gari akaja kunichukua, akiacha kazi zake mjini.

2. Kijijini alikuta hali si nzuri sana kwani Baba yako alishatumia akiba kwajaili ya matibabu, alienda sokoni na kununua mahitaji yote ya nyumbani kisha akamuchia Baba yako pesa ya matumizi ya siku zote nitakapokua mjini huku akimuambia akipata shida ampigie simu.

3. Alinileta mjini na kunipeleka hospitalini, aligharamia matibabu yangu na kuhakikisha natibiwa katika hospitali nzuri akilipa gharama kubwa bila kulalamika.

4. Niliishiwa damu na hospitali hakukua na group langu akalazimika kwenda kazini na mtaani kutafuta watu wakunisaidia damu na Mwenyezi Mungu alisaidia akapata nikapona.

5. Kila siku asubuhi kabla ya kwenda kazini kwa mwezi mzima ambao nililazwa hospitalini alikua anakuja asubuhi kuniona.

6. Mara kadhaa alijitahidi kutoroka kazini mchana na kuja kuniona hospitalini kuniangalia. Namshukuru Mwenyezi Mungu nimepona.

MAMBO AMBAYO MUMEO HAKUYAFANYA TANGU NIANZE KUUMWA.
1. Alisahau kuja kunichukua hospitalini baada ya mimi kupona kabisa hivyo mimi kulazimika kupanda Tax kuja nyumbani kwake ambapo naishi na ananihudumia kwa kila kitu.Sijui alichomfanyia Mama yake alipokuja hapa ila mwanangu k**a mtu akimfanyia Mama yangu hivi,ningemlamba miguu kwa kumshukuru.

Mwanangu k**a umeshindwa kumvumilia huyu mwanaume, k**a amekuudhi sana huna haja ya kuendelea kuvumilia mateso yake, kesho turudi wote nitakutafutia Malaika wa kukuoa.

***MWISHO...

Copy & Paste

09/12/2019

KAULI YA RAIS UHURU KENYATTA KWENDA KWA WAZAZI.

Amesema hata K**a watakasirika wakasirike lakini huu ndio ukweli wanaopaswa kuupokea.

Kumuamsha mdada wa kazi saa 11 alfajiri na kuwaacha binti zako wamelala Ni kumuandaa binti wa kazi kuwa mke Bora kuliko wanao.

Eti kumtumikisha dada wa kazi apige deki, apike, afue nguo, aoshe vyombo wakati wanao wanaangalia TV. Ni kumuandaa mdada wa kazi kuwa mwanamke anayewajibika kuliko wanao.

Kumuacha binti wa kazi aandae watoto kwenda shule, awaandalie uji mapema, awalishe, awasafishe wakati wanao wanacheza gemu kwenye simu au computer Ni kumuandaa binti wa kazi kuwa mama na mlezi bora kwa watoto kuliko wanao.

Na kwakuwa yote hayo unayafanya kwa masimango na manyanyaso unamfanya mdada wa kazi kuwa jasiri mwenye kuzikabiri changamoto za ndoa yake kuliko wanao.

Ukimaliza kwa kusema mwanao akiwa hajui hayo yote, ndoa ikiharibika mnazungukuka kutafuta maombi kwa wachungaji kumbe ninyi mmeharibu ndoa za watoto wenu.

Msiwasumbue wachungaji.

Address

Mlandizi
Kibaha

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Afya Ya Mahusiano posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to Afya Ya Mahusiano:

Shortcuts

Share

Category