Mkwawa University College of Education

Mkwawa University College of Education Mkwawa University College of Education offers academic and professional studies in education. The College is located in Iringa Municipality.

MUCE Strengthens Postgraduate Education Through ADVANCE WorkshopMkwawa University College of Education (MUCE) on 11 Augu...
14/08/2026

MUCE Strengthens Postgraduate Education Through ADVANCE Workshop

Mkwawa University College of Education (MUCE) on 11 August 2026 hosted a Professional Development Workshop on the ADVANCE Methodology, Content and Quality Assurance, under the Advancing Social Innovation and Entrepreneurship through Postgraduate Education in East Africa (ADVANCE) project.

The workshop strengthened participants’ capacity in delivering quality postgraduate education, integrating social innovation and entrepreneurship, enhancing curriculum and instructional content, and promoting effective quality assurance.

The workshop contributes to MUCE’s commitment to advancing innovative, entrepreneurial and high-quality postgraduate education in East Africa.

🌾 HERI YA NANENANE – 8 AGOSTI 2026 🌱🇹🇿Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) kinawatakia Watanzania wote, hususan wakuli...
08/08/2026

🌾 HERI YA NANENANE – 8 AGOSTI 2026 🌱🇹🇿

Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) kinawatakia Watanzania wote, hususan wakulima, wafugaji na wadau wa sekta ya kilimo, Heri ya Nanenane 2026.

Today’s site meeting at Mkwawa University College of Education (MUCE) brought together the project team to assess the pr...
06/08/2026

Today’s site meeting at Mkwawa University College of Education (MUCE) brought together the project team to assess the progress of ongoing construction and development activities. The meeting focused on reviewing the quality of work, addressing implementation challenges, and ensuring that all activities remain on schedule to support the University’s commitment to providing a conducive learning and working environment.

Kitengo cha Ushauri na Unasihi cha Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) kimeendesha semina ya kuwajengea uwezo Waelimi...
03/08/2026

Kitengo cha Ushauri na Unasihi cha Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) kimeendesha semina ya kuwajengea uwezo Waelimisha Rika wapya na Wanasihi Wasaidizi, ikiwa ni jitihada za kuimarisha huduma za ushauri na unasihi kwa wanafunzi.

Semina hiyo imelenga kuwajengea washiriki uelewa, maarifa na stadi za msingi zitakazowawezesha kutoa msaada wa awali wa kisaikolojia, kuhamasisha afya ya akili, na kuchangia ustawi wa jamii ya chuo. Mafunzo hayo pia yanatarajiwa kuimarisha mfumo wa usaidizi kwa wanafunzi kupitia Waelimisha Rika na Wanasihi Wasaidizi, ili kujenga mazingira salama, jumuishi na rafiki kwa maendeleo ya kitaaluma na kijamii.

#

  | Kumbukumbu zinazojenga historia.Picha hii inatukumbusha safari ya kujitolea, mshik**ano na huduma bora kwa Chuo Kish...
30/07/2026

| Kumbukumbu zinazojenga historia.
Picha hii inatukumbusha safari ya kujitolea, mshik**ano na huduma bora kwa Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE). Wengine waliopo kwenye picha hii bado wanaendelea kulitumikia chuo kwa bidii, huku wengine wakiacha alama isiyofutika katika historia ya MUCE. Tunawathamini kwa mchango wao. 💙📚

Wanafunzi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) wanaendelea na UE Week ya pili kwa kujituma katika maandalizi ya mit...
27/07/2026

Wanafunzi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) wanaendelea na UE Week ya pili kwa kujituma katika maandalizi ya mitihani. Ari, nidhamu na bidii wanazoonyesha katika kujisomea ni msingi wa mafanikio yao ya kitaaluma. Tunawatakia kila la heri wanapoendelea na safari ya kuelekea kwenye mitihani yao. 📚✨

Mbunge wa Iringa Mjini, Mhe. Fadhili Ngajilo, leo tarehe 27 Julai 2026 amefanya mazungumzo na Menejimenti ya Chuo Kishir...
27/07/2026

Mbunge wa Iringa Mjini, Mhe. Fadhili Ngajilo, leo tarehe 27 Julai 2026 amefanya mazungumzo na Menejimenti ya Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) katika ofisi ya Mkuu wa Chuo.

Katika mazungumzo hayo, pande zote mbili zimejadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Chuo, huku zikikubaliana kuimarisha ushirikiano na kubuni mbinu za pamoja za kutafuta rasilimali zitakazochangia kuboresha miundombinu ya MUCE na kuinua mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

Aidha, Mhe. Ngajilo ameahidi kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya maadhimisho ya Miaka 20 ya MUCE na Miaka 71 ya Taasisi za Mkwawa, yatakayofanyika mwezi Novemba 2026, ikiwa ni sehemu ya kuenzi historia, mafanikio na mchango wa taasisi hiyo katika maendeleo ya elimu nchini.

Je, unatamani kujiunga na *Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa?* Tunapenda kukufahamish...
23/07/2026

Je, unatamani kujiunga na *Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa?* Tunapenda kukufahamisha kuwa dirisha la kwanza la udahili kwa Mwaka wa Masomo 2026/2027 limefunguliwa *kuanzia tarehe 10 Julai hadi 10 Agosti 2026*. Mbali na programu za ualimu, Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa kimeanzisha programu mpya ambazo zitaanza kufundishwa Mwaka huu wa Masomo.

Na k**a unahitaji msaada wa kufanya maombi ya kujiunga, usihangaike peke yako! Kuanzia *tarehe 21 hadi 26 Julai 2026*, MUCE itatoa Huduma ya Msaada wa Udahili bure. Huduma hiyo itatolewa *mbele ya Maktaba ya Mkoa wa Iringa*, kuanzia *saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni*, kila siku. Pia, unaweza kutembelea *Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kampasi ya Mwalimu J. K. Nyerere (Mlimani), Viwanja vya Maktaba Mpya ya UDSM*.

Wataalamu wetu watakusaidia:
•⁠ ⁠Kujaza maombi ya udahili,
•⁠ ⁠Kuchagua programu inayokufaa,
•⁠ ⁠Kuelewa vigezo vya udahili,
•⁠ ⁠Na kujibu maswali yote kuhusu kujiunga na MUCE au Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

*Usisubiri dakika za mwisho. Omba sasa na jengea kesho yako msingi imara kupitia MUCE. Tukutane MUCE Novemba 2026*

*Kwa maelezo zaidi, piga simu 0763 382 233.*

Address

Iringa

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mkwawa University College of Education posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share