02/11/2016
WANAFUNZI WALIOSOMA TOSAMAGANGA WAANZA MCHAKATO WA KUBORESHA SHULE YAO.
Wanafunzi waliosoma Tosamaganga High School, wameanza mchakato wa kuboresha shule yao.
Pichani chini: Ni ujenzi wa vyoo (maarufu k**a "halfmile"). Mradi utakaogharimu zaidi ya fedha za kitanzania milioni ishirini (20,000,000+). Huu ni mchango mkubwa sana. Michoro na ujenzi unasimamiwa na Alumni wenyewe.
Huu ni mwanzo wa safari ndefu ya kuifanya Tosamaganga kuwa shule ya mfano, kuna changamoto kadhaa zipo shuleni ikiwemo.
i) Matumizi ya nishati ya kuni kupikia
ii) Kuzuiwa kutumika kwa bweni la Mandela ambalo limeachwa lianguke.
iii) Ukosefu wa walimu hasa wa masomo ya Sayansi
iv) Kukosekana kwa vyoo, kufuatia uchakavu na kuanguka kwa vyoo vya zamani.
v) Mgogoro wa Ardhi, kati ya Wizara na Kanisa katoliki juu ya umiliki wa eneo hilo.
vi) kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa watahiniwa
vii) Uchakavu wa miundo mbinu kwa ujumla.
Kwa kuwa tumedhamiria tutalienda moja baada ya jingine kuhakikisha shule hii inakuwa ya mfano.
Mweka Hazina wetu Dr. Erasto Mbugi ( +255 759 352504 MPesa: Jima Erasto Vedastus MBUGI ) anaendelea kukusanya michango. Pongezi za dhati kabisa kwa kazi nzuri anayofanya.
Kwa maelezo zaidi juu ya harakati hizi na kupata maelezo zaidi wasiliana na Danford Mbilinyi, tumemteua kuwa Mwenyekiti wetu na msemaji wa Alumni kwa sasa.
Shukran za pekee kwa Mnyitafu, Shack Noel, Maulilo KIPANYULA, Arch Yusuf, Kwame Lutangilo, Isaack Mboma Greyson Nyamoga na Eng Nickie M kwa kujitoa na kuhamasisha.
Tafadhali wa"tag" wanafunzi waliosoma Tosamaganga ili tushirikiane nao kwenye kuboresha shule yetu ili iweze kupanda kitaaluma.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Tosamaganga!!
| MWERANGI, Iddy |
| Tosamaganga PCB1 1996/1998 |