27/07/2026
Picha ya pamoja ya vyuo vilivyoshiriki kwenye MAONESHO na Mgeni Rasmi, Mheshimiwa Lela Muhamed M***a, Waziri mwenye dhamana ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, katika hitimisho la kilele cha Maonesho ya Saba (7) ya Wiki ya Elimu ya Juu yaliyofanyika katika Uwanja wa Gombani, Pemba.
Akihitimisha maonesho hayo, Mheshimiwa Waziri alitoa hotuba fupi ya kuvishukuru vyuo na taasisi zote zilizoshiriki, akieleza kuwa ushiriki wao ni ishara ya mshik**ano na jitihada za kuwawezesha Watanzania kupata fursa za elimu ya juu kupitia vyuo vinavyotoa fani mbalimbali.
Aidha, alivitaka vyuo kuimarisha ushirikiano na taasisi za elimu ya juu za ndani na nje ya nchi ili kupanua wigo wa kubadilishana uzoefu, kuboresha ubora wa elimu, na kuongeza ushindani wa wahitimu. Alisisitiza kuwa ushirikiano huo utasaidia kuzalisha wahitimu mahiri wenye uwezo wa kuchangia maendeleo ya Tanzania kwa kutoa huduma bora katika sekta mbalimbali.
π Je, ungependa kuifahamu zaidi TTCIH?
Tunakukaribisha kutembelea banda letu ili ujifunze zaidi kuhusu Chuo cha TTCIH, kozi mbalimbali tunazotoa, sifa za kujiunga, pamoja na huduma nyingine zinazopatikana chuoni.
Aidha, utapata fursa ya kujionea Mfumo wa Mafunzo kwa Njia ya Masafa (National eLearning Platform for Health) unaopatikana kupitia www.elearning.moh.go.tz, mfumo uliasisiwa na TTCIH kwa ushirikiano na Wizara ya Afya kupitia Idara ya Mafunzo.
Wahudumu wetu wapo tayari kukuelekeza kuhusu kozi mbalimbali zinazotolewa, sifa za kujiunga na chuo, pamoja na kukusaidia hatua kwa hatua katika kujaza fomu za kujiunga na CHUO kwa mwaka wa masomo 2026/2027.
π Chuo Kinatoa Kozi Zifuatazo:
π Stashahada ya Ufamasia (Diploma in Pharmaceutical Sciences) β Miaka 3
π©Ί Stashahada ya Utabibu (Diploma in Clinical Medicine) β Miaka 3
ποΈ Stashahada ya Optometria (Diploma in Optometry) β Miaka 3
π Kwa maelezo zaidi
π± 0781 845 374
π± 0718 552 164
π Tembelea tovuti yetu : www.ttcih.ac.tz
π§ Tuandikie barua pepe: [email protected]
π KWA NINI UCHAGUE TTCIH?
π¨ββοΈ - Wakufunzi wabobezi katika fani ya afya na tafiti
π₯ - Hospitali kubwa ya Rufaa kwa ajili kujifunzia kwa vitendo
π - Internet ya uhakika
π - Hostel za kisasa na salama zenye huduma zote muhi